The Greatest Man in Universe: Kijana mdogo aliyefanya makubwa na kuacha alama akiwa na umri mdogo

The Greatest Man in Universe: Kijana mdogo aliyefanya makubwa na kuacha alama akiwa na umri mdogo

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2016
Posts
35,812
Reaction score
107,628
Salute
Mnamo mwaka wa 4BC jijini Galilaya katika kitongoji kiitwacho Nazareth kulikuwa na familia ya Bw. Joseph na mkewe Maria; walipata mtoto wa kiume wakamwita Jina Yeheshua au Yesu.

Ilikua ni moja ya kaya ya kimaskini, Bw. Joseph alikua anajishughulisha na shughuli za uchakataji wa mbao yaani useremala pia mkewe Bi. Maria alikuwa anajihusisha na shughuli ndogo ndogo za mikono. Yesu alifundishwa kusoma na kuandika tu maana wazazi wake hawakuweza kumudu gharama za kumpeleka shule zaidi, lakini alisoma pia masomo ya dini kwa walimu wa kiebrania waitwao “Rabi”. Kijana huyu alikuwa akisaidiana na baba yake kufanya shughuli za uchakataji mbao.

Alipotimiza miaka 30 kijana huyu ndio nyota yake ya mafanikio ilipoanza kung’aa, alianza kazi zake za kufundisha watu kama “Rabi” mambo mbalimbali yahusiyo falsafa ya maisha. Alifundisha kwa muda wa miaka mitatu tu, so alipokua na miaka 33 alifariki dunia kwa kuwambwa msalabani na dola ya Rumi iliyokua inatawala nchi nyingi kipindi hicho.

Kosa lake lilikua ni uhaini kwa kujiita mfalme wakati nchi hiyo ilikuwa ina mtawala ambaye ni Herode na Gavana Pilato wakiwa chini ya mtawala Kaisari Tiberius, pia kuweka maandamano yasiyo na kibali.

Japo aliishi miaka 33 na kufanya kazi yake kama rabi kwa mmuda wa miaka 3 aliweza kufanya mengi makubwa ambapo mpaka leo hii ulimwengu hautamsahau kamwe. Japo kafariki takribani miaka 2000 iliyopita lakini kila siku wafuasi wake wanazidi kuongezeka, hapo zamani kulikuwa na watu mashuhuri na maarufu wengi sana waliofanya mambo mengi kama vile Mose, Imhotep, Caesar Augustus, Archimedes, Pharaoh Rammiress II, Socrates, Spartacus, Leonidas, Plato, Alexander the Great, Aristottle, Ibrahim, Nebucadnezar na wengineo wengi. Lakini kijana mdogo sana ndani ya miaka mitatu tu aliweza kuvunja rekodi za watuwote hao mashuhuli na kubaki yeye ndiyo kinara.

Miaka imepita lakini mpaka leo hakuna mtu ambaye ameweza kuvunja rekodi yake, anafahamika kama mwanafalsafa, mtabiri na mwanasayansi nguli aliyewahi kuishi na hatokuja kutokea kama yeye.

Vitabu vyenye mafundisho yake ndio vinaongoza kuuza kuliko vyote, ni binaadamu ambae jina lake linazidi kukua kila siku badala ya kufifia japo ni miaka 2000 imepita. Wafuasi wake wengi wamekuja kuwa ni watu mashuhuri na wanafalsafa wakubwa kama vile Paulo, Thomas aquinus, Francis of Assis, Ignatus Luyola, St Luke, Francis Xvery, John Paul II, nk.

Kaacha miongozo ambayo ilikuja kutengeneza taasisi kubwa yenye nguvu na washirika wengi ambayo ni Catholics. Inaonyesha watu wengi mashuhuri duniani wamepita kwenye taasisi hii au ni wafuasi wa mafundisho ya huyu kijana mdogo. Yeye ndiyo binaadamu zaidi maarufu ulimwenguni. Kaacha historia ambayo haiwezi vunjwa maisha yote maana jina lake limeshindwa kufutika. Hebu fikiria kama alifanya mambo yake kwa muda wa miaka 33 tu ila umaarufu wake unazidi kukua na wafuasi wanazidi kuongezeka siku baada ya siku.

Wakuu mimi kiukweli namuonea sana wivu huyu kijana, haiwezekani kwa muda wa miaka 20+ niliyoishi hapa duniani sijawahi kufanyiwa Happy birthday, sidhani kama kuna mtu mwingine tofauti na mama anayekumbuka siku yangu ya kuzaliwa. Lakini kijana mdogo aliyekufa miaka mingi sana iliyopita karibia dunia nzima wanajua siku ya kuzaliwa kwake na hua wanasherhekea nyumbani huwa wanapika wali kabisa na kuchinja yule mbuzi mnene tuliemchunga muda mrefu halafu mimi first born kwenye kumbukumbu yangu ya kuzaliwa sijawahi pewa hata andazi.

Kinachoniumiza zaidi najua siku nikifa tu watu watanisahau mara tu baada ya kutandua msiba wangu, sitakumbukwa na yoyote kama yesu tunavyomkumbuka labda nyie wa huku JF mtanikumbuka kwa posts zangu.

Kiukweli mimi sikubali, kwanini Yesu atushinde watu wote wakati alikuwa binadamu sawa kama sisi? Tunakosea wapi? Kweli tumeshindwa kuvunja rekodi zake nasi basi tukumbukwe hata kwa muda wa miaka 10? Lakini je, huyu kijana mdogo alifanyaje hadi akaweza kufanya mambo makubwa yote haya ndani ya muda mdogo?

Maneno yote huko juu ni kuonyesha jinsi huyu kijana alivyoweza fanaya mambo mengi ndani ya muda mchache lakini kubwa la msingi ni kujua je aliwezaje? Alitumia nini?

Yesu aliwezaje?

Ukichunguza utajua kabisa huyu mtu alikuwa ana vitu anafanya ili kutimiza mipango yake hiyo yenye matokeo makubwa. Yesu alitumia vitu vitatu ili kufanya yote hayo. Kwanza kabisa alikua anajtambua (nilishaliongelea hili), pili alikuwa anafahamu kusudi lake (nitaliongelea hili panapo majaliwa) tatu alijali muda kuliko kitu chochote. Yes! Hapa ndiyo kwenye kiini cha mada yetu; Time Management. Jinsi nidhamu nzuri ya matumizi ya muda inaweza kukuletea mafanikio makubwa.

Japo Yesu hakuwa na elimu kubwa lakini alijitambua na alitambua kusudi lake mapema mno ndiyo maana alitumia muda wake vizuri sana akaweza kufanya mambo mengi makubwa. Alithamini muda wake alifanya kazi yake kwa nidhamu ya hali ya juu muda ukiwa ndio silaha yake kuu.

Kuna mtu aliwahi muuliza The Godfather Mwl. Julius Nyerere kwamba anawezaje kufanya mambo mengi kama vile kuhudhuria vikao, kuwa na familia yake, kuandika vitabu na makala kwenye magazeti, kuongoza nchi, kufanya ziara n.k kwa wakati mmoja? Nyerere alisema yeye anaheshimu muda. Muda wa kula anakula tu, muda wa kikako anakua kikaoni, kutembea anatembea tu, muda wa kulala analala tu n.k n.k

Najua humu wengi wetu hili ni ngumu sana. Unakuta mtu yupo anatembea kwenda mahali fulani lakini muda huohuo anasimama kuchat, muda wa kulala yeye anasoma kitabu, muda wa kusoma yeye anakula, muda wa kula ndiyo kwanza anaanza kuongea na simu, muda wa kazi yeye anaingia JF, muda wa kutafuta watoto yeye anapiga stori na mwenzi wake.

In short, muda hatuuthamini hasa huku kwetu Afrika, ndiyo maana Wachina wanatuendesha sana na tunaona kuwa wanatunyayasa huko makazini maana wao wamekulia kwenye malezi ya kufanya kitu kutokana na muda unaruhusu kufanya nini, sasa ile silka yao wakiileta huku twaona hawa watu wapo kama mashetani.

Kijana amka jali muda wako ulionao. Kwani nyie wenzangu hamumuonei wivu huyo jamaa huko juu aliyefanya mambo mengi ndani ya muda mfupi? Moja kati ya utajiri mkubwa binaadamu alionao ni muda.

Kama umefanikiwa kuwa na leo basi wewe ni tajiri mkubwa, leo hii ndio muda wako amka ukafanye yale unayotamani kufanya. Usisubiri kesho, kesho haipo siku zote ipo leo tu! Achana na kupoteza muda wako kwa kwenda location kupiga picha za kupost Facebook upate like 300, unadhani siku ukifa kuna mtu atakukumbuka kwa kuacha picha zenye like nyingi na quality nzuri huko FB? Sahau hili.

Yesu alijitambua mapema ndiyo maana aliweza fanya mambo makubwa, jitambue kijana mwenzangu hautakumbukwa kwa kuweza kutaja kikosi kizima kinachocheza ligi daraja la tatu huko Italy au England. Tumia muda wako huu ulionao leo kwa kufanya mambo yatakayoacha alama isiyofutika hapa duniani.

Huyo ndio Yesu the Greatest man, hakuna mtu mwingine kama yeye, hakuna atakayeweza kuvunja rekodi zake alizoacha sana tunaweza fuata matendo yake ili kufanya mambo makubwa kwenye maisha ila kumpita tuache legacy kubwa kuliko yeye haitawezekana kamwe.

Tujali muda jamani, ipo siku tutajutia huu muda tuanaopoteza kufuatilia mwanamke mmoja miezi sita halafu kila siku unatumia zaidi ya masaa 4 kuwasiliana nae wakati muda huo ungefanya mambo mengi ya msingi ndani ya miezi hiyo 6 yakamfanya huyo mwanamke akajileta mwenyewe.

Utajiri wetu mkubwa sisi watoto wa maskini ambao tunaweza kuutumia kupunguza kiwango cha umaskini kwenye familia zetu kama Yesu alivyofanya kwenye familia yetu ni MUDA. Jali muda utakutunza uzeeni.

JE WEWE BINAFSI NI NANI UNAONA NI GREATEST MAN ALIYEFANYA VITU VIKUBWA AMBAE TWAWEZA KUJIFUNZA KUPITIA YEYE?
Ahsanteni.
Like & Share

Da’Vinci
El maestro.
 
Binafsi baada ya Yesu mtu mwingine ambae naweza kumuweka nafasi ya pili ni Wolfgang Amedius Mozart almaaurufu kama Mozart. Huyu jamaa nae kafanya mengi makubwa akiwa na umri mdogo tena ndani ya muda mchache.

Akiwa na miaka 5 tu tayari alikua ashakua maarufu sana kwa upigaji wa piano na utunzi. Aliishi miaka 35 tu lakini hakuna mtu aliye kwenye ulimwengu wa muziki hamjui huyu mtu.

Imagine nyimbo zake za miaka 1780s huko mwaka 2013 kawa ndie aliyeongoza kwa mauzo ya CD za nyimbo. Jamaa kafanya mengi sana. Kwa wanaomjua wanajua uwezo aliokua nao.
Cc Kichuguu
 
We Youths, tufanye mambo yatakayo acha sifa nzuri kwenye jamii na kuacha alama za kudumu. Sio mtu una miaka 50 halafu jambo kubwa ulilofanya kwenye jamii ni kuacha watoto wengi kwa mama tofauti tofauti ambao hawajui thamani yako kama baba.. Pengine wanajuta kuja duniani kupitia kwa baba usiejali kama wewe..Unadhani jamii itakukumbuka kwa kua na mademu wengi mtaani?

Kila ukitaka kulala fikiria siku ukifa Jamii unayoishi itabaki inakukumbuka kwa lipi?
Ulikuja duniani kulewa tu kisha ufe au ulikuja ili uwe msaada na nuru kwa wanadamu wenzio?
Ishi vyema. Huku ukiiwazia siku utakayokua haupo ulimwenguni watu watadaidika nini na uwepo wapo huo.
 
Kuhusu 'Who is the most powerful person on earth'.
Hapa tutaweza kujua historia za watu kutokana na kila mtu anavyoona powerful person wake ni nani na ni kwanini.
Paula huyu ndie greatest man and most powerful person naemkubali mimi kutokana na mambo aliyoyafanya ndani ya muda mfupi.
Namsubiria wakwako
Cc
Paula Paul Mr Miller
 
We Youths, tufanye mambo yatakayo acha sifa nzuri kwenye jamii na kuacha alama za kudumu. Sio mtu una miaka 50 halafu jambo kubwa ulilofanya kwenye jamii ni kuacha watoto wengi kwa mama tofauti tofauti ambao hawajui thamani yako kama baba.. Pengine wanajuta kuja duniani kupitia kwa baba usiejali kama wewe..Unadhani jamii itakukumbuka kwa kua na mademu wengi mtaani?

Kila ukitaka kulala fikiria siku ukifa Jamii unayoishi itabaki inakukumbuka kwa lipi?
Ulikuja duniani kulewa tu kisha ufe au ulikuja ili uwe msaada na nuru kwa wanadamu wenzio?

Ishi vyema. Huku ukiiwazia siku utakayokua haupo ulimwenguni watu watadaidika nini na uwepo wapo huo.
Ukifanya mapema utakufa mapema, shauri yako, anzia kufanya uzeeni kama mzee wa KFC ndiyo utaishi kitambo kirefu kijacho.
 
Ukifanya mapema utakufa mapema, shauri yako, anzia kyfanya uzeeni kama mzee wa KFC ndiyo utaishi kimbo kurefu kijacho.
Haha.. haki kamsemo kakujipa moyo bila shaka.. Hakuna mtu anayekufa mapema au kuchekewa kufa. Point yangu iko pale pale siku zote..Time is relative. Nitachelewa kwakua wewe umewahi au kawahi kwakua wewe umechelewa. Muda wako ukifika umefika ILA Mungu hua anatoa neema kwa watu ili kuthibitisha ukuu na uweza wake ili kututia tumaini wengine. Moja ya waliopata neema hiyo ni bwana huyu wa KFC. Neno hilo la Mithali lilitimia kwake.

Mithali:9,11 Maana kwa msaada wangu siku zako zitazidishwa,na miaka ya maisha yako itaongezwa.
 
NDUKI
niliwahi kuandika humu..Orodha ya watu maarufu na wenye ushawishi zaidi.
10. Isac Newton
Alizaliwa mwaka 1642 na kufariki dunia mwaka 1727
Kama ulisoma sayansi walau kidato cha pili tu basi utakua unamfahamu.
Ameandikwa kwebye vitabu karibia 500,000 na inakadiriwa umaarufu wake hautaweza kupitwa na mtu labda baada ya miaka zaidi ya 250
Ni nguli wa Mechanical Physics na umaarifu wake mkubwa upo kwenye Newton's Law of
Pia ni mtaalamu wa Principles of Natural Philosophy

Kwa mwezi anafuatiliwa (searched) na watu zaidi ya X 2,000,000

9. Leonardo Da Vinci
Alizaliwa mwaka 1452 ni mtaalamu wa michoro ya Code Pictures. Ni mwiba mchungu kwa kanisa katoriki kutokana na michoro yake pamoja na maandiko yake kuhusu kanisa.
Japo hapendwi ila yeye ndo aliyechora sura ya bwana Yesu iliyopo makanisani kwani baada ya kuichora ndio wakatafutwa watu wanaofanana nayo na kuigiza filamu ya Yesu
PIa ana mchoro wa The Last Super ambao una code zinazoonesha Yesu alikuwa na Mahusiano na maria Magdarena.

Mchoro wa Monalisa pia ambao ni mwanamke mwenye sura mbili.
Ila ja anadaiwa alikuwa shoga
Kaandikwa kwenye vitabu zaidi ya 6,000,000

Kwa mwezi anatafutwa zaidi ya X 4,000,000
...
8.William Shakespear
Ni Mwingereza aliyezaliwa mwaka 1564 na kufariki dunia mwaka 1616
Huyu ana mchango mkubwa kwenye lugha ya Kiingereza, kachangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa msamiati na kuenea kwa lugha ya Kiingreza
Ndio mwasisi wa misemo kama vile:
Food for the gods
It's all Greek to me
All that glitters is not gold
By love
All is well
N.k
Katajwa kwenye vitabu zaidi ya 1,000,000

Anafuatiliwa mara 7,500,000 kwa mwezi

7.Adrof Hitler
Alizaliwa mwaka 1889 na kufariki/kujiua mwaka 1945 baada ya kushindwa WW2
Pia ni mwanzilishi wa magari ya Volkswagen alitaka kila Mjerumani aendeshe gari badala ya baiskeli

Anskumbukwa kwa kunyanyasa na kuua mamilioni ya Wayahudi.
Alikuwa rafiki mkubwa wa Benito Mussolini na wote walikufa 1945 baada ya kushindwa vita
Msome zaidi kwenye kitabu chake cha mein Kempf [My Struggle]
Ameandikwa kwenye vitabu zaidi ya 200,000

Kwa mwezi anatafutwa X 6,500,000


6. Paul The Apostle of Tarsus
Alizaliwa mwaka 5C na kufa 67 AD
anajulikana kama Mtume Paulo na ndiye mtume aliyeipigania dini kwa kuweka miongozo na kanuni tunazozifuata hadi hii leo
Ameandika vitabu 13 vilivyopo kwenye Bible na vingi sanaaa ambavyo havijawekwa kwenye bible.
Anajulikana kwa wakristo kama mtu wa kwanza kujua kuandika
Kaandikwa kwenye vitbu takribani 7,000,000

Kwa mwezi anatafuta takribani X 4,000,000
.

5. Siddhartha Gautama

Aliishi kuanzia mwaka 563C hadi mwaka 483 AD
Huyu ni maarufu zaidi kwa jina la Buddha yaani kwa Wabudha kwao ni kama Yesu Kristo
Alizaliwa kwenye ile nchi isiyo na bendera ya mstatili Nepal
alikuwa ni mpiga mazoezi na mweneza imani mkubwa ya kuwafumbua watu huyu ndo mfalme wa mediation.
Fkawahi kupiga mediation ya siku 49 , inafahamika kama Noble Eightfold Path duniani kwa ujumla
Supreme buddha anfuatiliwa/abudiwa zaidi na Wahindu

Ameandikwa kwenye vitabu zaidi ya 7,000,000

Anatafutwa X 4,000,000 na ushee kwa mwezi

4. Moses
Huyu ndo Musa
Aliishi kati ya mwaka 1300C hadi mwaka 1080 BC
Huyu anaheshimiwa na Uislamu pamoja na Ukristo hivyo hafungamani na dini yoyote ndio maana jina la MUSA ni la Waislamu kwa Wakristo
Anakumbukwa zaidi kwa miujiza na safari yake ya kuwarudisha wana wa Israel. Yawezekana ni moja kati ya watu wanaochukiwa nchini misri akifuatiwa na Sergio Ramos.
Kaandikwa kwenye vitabu 8,000,000

Anatafutwa X 3,000,000 na ushee kwa nwezi

3. Ibrahim
Aliishi kati ya mwaka 1812C hadi 1537 BC
Abraham anajulikana zaidi kama Nabii Ibrahimu na Wakristo kwa Waislamu wanamfahamu
Anaaminika ndiye mtu wa kwanza wa Masharuki ya kati kuamini katika uwepo wa Mungu mmoja
Ameandikwa kwenye vitabu takribani 2,000,000

Anatafutwa zaidi ya X 10,000,000 kwa mwezi

2.Abu Al--Qasim Mu Ammad Ibn Abd Allah

Aliishi kati ya mwaka 570 hadi 67
Kwawasio waislamu Mtume Muhammad ndio mwanzilishi wa Uislamu ila kwa wenye dini yao wanaamini/wanasema hakuanzisha chochote.
Anatafutwa kwa mwezi X 14,000,000 ila hata

1. Jesus of Nazareth
Aliishi kati ya mwaka 5BC hadi 28 AD
Alizaliwa na Bikira Maria kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
Pamoja na kuishi bila shari na mtu akasalitiwa na bwana Yuda Eskariote na wenzake wachache kisha Pilato akatoa hukumu ya akasulubiwa akafa kisha akapaa mbinguni
Huyu ndie Genius, Phillosopher wa muda wote na hatokuja kama yeye tena mpaka mwisho wa dunia
Ameandikwa kwenye vitabu visivyo na idadi

Anatafutwa X 25,000,000+ kwa mwezi

Tchao.
Vinci...
 
Da'Vinci,

Aisee kwenye piano umenigusa, kuna dogo mmoja pale makuburi kanisani, ni mtoto wa mtunzi wa nyimbo ndugu Mukasa!
Yule mtoto ana umri mdogo sana lakini anavyopiga piano hata baba yake hamfikii kwa kweli! Akifikisha umri mkubwa nadhani atakuwa hatari sana!


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mnamo mwaka wa 4BC jijini Galilaya katika kitongoji kiitwacho Nazareth kulikuwa na familia ya Bw. Joseph na mkewe Maria; walipata mtoto wa kiume wakamwita Jina Yeheshua au Yesu.

Ilikua ni moja ya kaya ya kimaskini, Bw. Joseph alikua anajishughulisha na shughuli za uchakataji wa mbao yaani useremala
Uongo mtupu ulioandika Maria na Joseph hawakuwa Kaya maskini.

Wote walikuwa ukoo wa kifalme .Ukoo wa Mfalme Daudi..Kasome mathayo sura ya kwanza.Koo za kifalme hazijawahi kuwa Kaya maskini miaka hiyo Hadi Leo hii

Maselemala Sio watu maskini.Nenda keko dar es salaam kaangalie maselemala waliopo pale Wana magari ya mamilioni nyumba za uhakika na huuza funiture zao Hadi nje ya nchi.Aliyekuambia selemala ni mtu maskini Ni Nani?

Hata Yesu alizaliwa kwenye Holi la ng"ombe Sio sababu familia ya Joseph walikuwa Kaya maskini Bali sababu nyumba ya wageni ilikuwa imejaa.Pesa za kulipia walikuwa nazo
 
Sikuwahi kujua kama kazi ninazoziona alizofanya Yesu, zilifanyika ndani ya miaka mitatu tuu. Mitatu tuu? Hili nimelijua leo.

Kwa hiyo huyu Yesu ni mtoto wa Joseph?. Joseph ndio alikuwa biological father wa Yesu?.
That's interesting!!!.

Asante sana umetushauri vizuri kwenye jambo zima ya time mgt , kuutumia muda tulionao kwenye matumizi mazuri. Kufanya jambo kwa wakati wake.

Good Job!
 
Ahsante, Nina meengi yaliyonitatiza! Nianze na hili; "Mtu" Mahala kadhaa umemuelezea hivyo,una hakika ndivyo anavyotambulika mbele ya wafuasi wake halisi na wasiokuwa halisi?
Sikutaka nimzungumzie kiimani.
Nimemzungumzia kama mtu tu wa kawaida ndio maana namwita ni mwanafalsafa.
Yesu ana personality 2 ambazo ni Uanadamu kwa 100% na Uungu kwa 100%.
Mimi nazungumzia yule Yesu mwanadamu.
 
Back
Top Bottom