Elections 2010 The Heat is hitting

Luteni

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
2,274
Reaction score
302
Walisema maoni ya wanaJF haya-reflect hali halisi ya wananchi wakasema tena hata polls zao haziwatishi, refer hotuba ya JK kwenye ufunguzi wa kampeni ya CCM kabla ya kuanguka alisema hababaishwi na mitandao kwa sababu wanaoshiriki ni sehemu ndogo tu ya watanzania mil.40, wakasema vijijini hawana komputa na hata wakiwa nazo hakuna umeme huko. Hatimaye umeme wa mitandao umeanza kufika vijijini maoni ya wanamitandao na polls zao zimeanza kupenya kwa wahusika leo hawapendi tena kuziona wala kuzisikia. The Heat is hitting.
 

Labda walikuwa hajui kwamba walioko kwenye mitandao ndio wanao support maisha ya watu wengi walio na wanaoishi vijijini... na walio vijijini kila kukicha hawakosi kuwasiliana na watu walio kwenye internet kwa namna moja au nyingine (hasa txt msgs) iwe ni kuomba school fees, mchango wa harusi au kutaka tu kusalimiana na ndugu zao baada ya muda fulani hivi...

Hawajui pia kwamba watu wa internet wana influence kubwa ya kuuwaambia ndugu zao kwamba wasifanye makosa kumchague yule atakayeendeleza sera za kulipia school fees sekondari.... watu wa mtandaoni wanaweza pia kuwaambia ndugu zao mchagueni fulani na kama hamta mchagua basi acheni kuniletea za Matonya kila siku kuomba michango ya matibabu, school fees na msaada wa kumalizia ujenzi wa nyumba au hata kuweka solar power.. Mungu kawapeni tayari mtu atakayewaleta neema za shule bure hadi form six na matibabu bure hadi private.. sasa tena wanataka kuwa Matonya kwa mambo hayo ili iweje wakati kuna mtu kesha waambia kwamba wamchague na awape... Wasimpompa watatukuwa na mapungufu fulani ya kutoelewa mambo ya Free!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…