Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Utangulizi:
Mnamo June 2, 1978, serikali ya Tanzania chini ya uongozi wa Rais Julius Nyerere, uliamuru Umoja wa makampuni ya Kiingereza yaliyojulikana kama Lonrho Limited, kuondoka nchini. Sababu "maalum" iliyotolewa kwa kitendo hicho ilikuwa Lonrho kuendelea kupinga uamuzi wa Baraza la Umoja wa Mataifa lililoazimia kuiwekea viwakwazo vya uchumi Rhodesia na pia upanuzi wa biashara za Lonrho Limited nchini Afrika kusini. Kwa kutumia nyenzo mpya kutoka maktaba ya Kumbukumbu za Kihistoria London, makala hii inajaribu kuangalia kupanda kwa Lonrho ndani ya Tanzanania mpaka utaifishaji wake, dondoo zilizosababisha, mkakati wa ulipaji fidia kati ya Lonrho na serikali ya Tanzania na sehemu ya serikali ya Uingereza ilivyochangia katika swala zima.
Maneno muhimu: Lonrho Limited; utaifishaji, Serikali ya Tanzania, Serikali ya Uingereza, na Tiny Rowland.
Wakati wa ukoloni, ilionekana umuhimu wa kufanya biashara za nje, hizi zilifanyika baina ya mataifa yaliyokuwa chini ya himaya ya coloni moja, biashara hizo zilidharau matatizo madogo yaliyopo kati ya nchi na nchi. Hikushangaza pale utaifishaji wa kampuni ya kigeni ambayo iliwahi kuenea katika nchi Afrika kabla hazijapata uhuru. Bwana Robert Tignor, aliwahi kunukuliwa akisema "kila kona ya bara ilikuwa na kauli kuwa uhuru bila kuwa na maamuzi huru ya uchumi itakuwa kichekesho". Mwaka 1969 pekee nchi 15 za Afrika zilipata uhuru. Mpaka kufikia 1962, si chini ya nchi 17 za ki-Afrika zilikuwa zimepitisha sheria mpya iliyobadilisha mfumo mzima wa uwekezaji na kuunda mifumo yao mipya. Matokeo yake kati ya 1960-1974, Afrika ilirekodiwa kuwa na utaifishaji mkubwa sana wa biashara kuliko sehemu yeyote ile duniani.
Kutokana na asili ya mfumo mzima wa biashara za nje baada ya uhuru katika Afrika, haikushangaza kuwa swala hili limekuwa makini miongoni mwa mijadala ya chanzo na ufumbuzi miongoni mwa watafiti wengi. Miaka iliyopita mada hii iliwatia watu hasira na walitaka kujua vigezo vilivyotumika na serikali husika katika utaifishaji wa biashara za nje.