Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Mwishoni mwishoni mwa hotuba ya Rais Samia kazungumzia mambo ayaonayo mitandaoni.
Mambo ya kizushi, ya kuchonganisha, na kila aina ya uzandiki.
Ni jambo jema. Ni jema kwa sababu linaonyesha haishi peke yake kwa kujitenga kwenye puto alimo yeye tu mwenyewe.
Anafuatilia kinachoendelea na kinachojiri kupitia yale wayasemayo watu awaongozao.
Ila, haya mambo inabidi awe makini nayo sana. Ni mara kadhaa ameyazungumzia haya yajiriyo kwenye mitandao.
Ni kana kwamba naye ‘anademka’ kwa yale yajiriyo huko.
Natumaini hataendelea kuyapa umuhimu kivile, la sivyo ataishia kucheua tu kwani the internet is still undefeated.