Hapo awali mapema Asubuhi ya Leo Vyombo vya habari, Media za Kijamii, mitandao na wataalam walivyobashiri hotuba ya Rais:
Baadaye Leo jioni:
22 April 2021
Dodoma, Tanzania
Hotuba ya Rais Leo Bungeni 22 April 2021
Mh. Samia Suluhu Hassan akilihutubia bunge mjini Dodoma Leo amesema serikali yake itaweka mazingira mazuri zaidi kuvutia uwekezaji kwa kuondoa urasimu usio na ulazima.
Mh. Rais wa awamu ya sita wa serikali ya Muungano wa Tanzania aliambia Bunge kuwa sekta binafsi ndiyo utii wa mgongo ktk kukuza uchumi na kutengeneza nafasi za ajira nyingi na soko kwa bidhaa za kuchakata mazao ya wakulima, wafugaji na kuongeza thamani madini.
Sekta binafsi kupitia uwekezaji wa ndani na toka nje, itachochea tija na ukisasa ktk uzalishaji mashambani, ufugaji na uvuvi kwani nchi hii Tanzania imejaliwa ardhi ,mabonde, maziwa, mito na ukanda mrefu wa bahari ya Hindi. Bila kusahau madini na utalii.
Bandari maalum za uvuvi kuanzishwa na meli nane za kisasa kununuliwa ili kufanya uvuvi katika bahari kuu.
Maeneo mahususi ya viwanda kujengwa kulingana na mazao yanayozalishwa ili kuwezesha mazao kuchakatwa kuzuia upotevu au uharibifu wa mazao baada ya kuvunwa na kutengeneza ajira ktk maeneo hayo ya nchi.
Maendeleo laini kupitia TEHAMA teknolojia ya habari na Mawasiliano kukuzwa ili kuwezesha Mapinduzi ya viwanda na uwekezaji kuweza kupatikana Tanzania unasisitizwa na serikali ya awamu ya sita kuelekea mpango wake wa Maendeleo ya miaka mitano inayoishia 2025.
Serikali Itatia mkazo Nishati mchanganyiko kama kutoka vyanzo vya mwanga wa Jua, thermal, gesi kujazia pale umeme wa nguvu za maji wa Rufiji JNHPP, Mtera, Kidatu n.k ambayo inaokabiliwa na tishio la mabadiliko ya tabia-nchi ili taifa liwe na uhakika wa nguvu za nishati kuendesha uchumi wake.
Kuna changamoto ktk Upatikanaji wa maji hivyo juhudi zaidi zinatakiwa. Pia elimu bure itazingatiwa ila mtaala wa elimu utalenga zaidi kuwa wa elimu-ujuzi ili kuendana na mazingira ya nchi na kuwezesha wahitimu kujiajiri tofauti na mitaala ya elimu ya sasa inayotoa wahitimu wasio na ujuzi wanaolilia kuajiriwa.
Mh. Samia Suluhu Hassan aliambia Bunge na taifa anakusudia kukutana na viongozi wa vyama vyote vya siasa nchini ili kwa pamoja wakubaliane mustakhabali wa muelekeo nchi yetu.
Mh. Rais Samia Suluhu Hassan aliasa Bunge kujikita kufanya kazi ya kuwasemea wananchi ambao wamewatuma kuwa wawakilishi wao na kuachana kupoteza muda kuzungumzia yaliyo nje na yale waliotumwa na wananchi.
Pia Mh. Rais ameirai Bunge kuikosoa serikali na mawaziri hata inapobidi ukosowaji uwe mkali wafanye hivyo vikali sana, Mh. Rais anasema ni ruksa katika awamu yake ya sita ili kuleta ufanisi kwa shughuli za serikali kuwatumikia wananchi na nch vizuri..