The iron law of oligarchy na ubawa wa demokrasia

The iron law of oligarchy na ubawa wa demokrasia

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Siku zote nimekuwa nasema kuwa demokrasia ni mfumo wa hovyo sana wa utawala. Sasa kuna mwanazuoni mmoja aliobserve kitu kimoja. Kwanza kwa kifupi oligarchy ni mfumo wa utawala wa matajiri wachache.

Matajiri wachache ndiyo wanaendesha nchi. Sasa kutika observation zake mwanazuoni huyo aligundua kuwa taasisi yoyote ya kidemokrasia mwisho wake huishia kuwa oligarchy.

Mwisho wa siku hutekwa na wachache ambao lengo lao kuu linakuwa si tena kusimamia maslahi ya taasisi bali kubaki madarakani na kufaidika nayo.

Angalia taasisi na nchi za kidemokrasia, utaona ni watu wale wale na watu wao wa karibu ndiyo wanashika madaraka. Na kadri muda unavyoenda ndivyo uoligarchy huo unavyozidi kukomaa.

Mwisho wa siku kunatokea misemo kama "CCM ina wenyewe." Hata kwenye vyama vya upinzani utaona ni watu wale wale na jamaa zao ndiyo wameshika madaraka.

watu wanaweza unda taasisi ya kidemokrasia kwa nia nzuri kabisa. Lakini suala la taasisi hiyo kuangukia kuwa oligarchy haliepukiki. Iron Lawa of Oligarchy inasema kuwa taasisi yoyote ya kidemokrasia mwishowe huwa oligarchy
 
Katiba mpya ni muhimu kuliko tunavyofikiria!
 
Back
Top Bottom