Waandishi wengi wa sheria kuhusu ICT,wanalieleza hilo kwa mawazo tofauti.Kinacholeta ugumu na pengine kusababisha sheria isiwe wazi zaidi kwenye hilo,ni kwa sababu,watu wengi kwenye mitandao ya kijamii kama ulivyoitaja hawatumii majina yao halisi,hivyo inakuwa vigumu kujua uhalisia wa yupi amekufa au anaishi,mtu mwingine unakuta kwenye mtandao anatumia IDs tofauti.Uzuri kila ukijiunga na mtandao wowote wa kijamii,kuna terms and conditions ambazo zimewekwa,ila wengi wetu huwa tuna accept tu bila kusoma.Kwa uelewa wangu mdogo na kwa mawazo yangu,issue yako ni ngumu.