Morning_star
JF-Expert Member
- Apr 21, 2018
- 6,042
- 17,320
Hayo ni maneno katika kibwagizo cha wimbo wa Marekani. Marekani ni taifa ambalo pamoja na makandokando yake lakini kama umetembea duniani lakini hujafika Marekani huwezi kusimama mbele ya watu ukasema umetembea!
Sasa katika kibwagizo cha wimbo huo wa Marekani yanayosema "marekani ni ardhi ya watu huru na nyumbani kwa majasiri"
Maana pana ya neno "home au nyumbani" kwa kiingereza ni kwamba: "a home is a sanctuary where we feel safe and comfortable" au kwa kiswahili "nyumbani ni mahali patakatifu ambapo mtu ujisikia salama na mstarehe". Kwa mukutadha huu tunaweza kuishi nyumba moja, mtaa mmoja, mji mmoja, nchi moja lakini tukawa tunaishi ulimwengu tofauti.
Kinachotofautisha maisha ya mtu na mtu ni "ujasiri" wako wa kupambana na changamoto za maisha mpaka ufikie ndoto zako. Kawaida mtu aliyefikia ndoto za maisha yake hafichiki! Jamii itamjua na atakuwa "role model" au "mfano wa kuigwa" kwa walio wengi!
Kuna watu wako mikoani wanatamani kuja Dar es Salaam! Wengi wanakuwa na shauku kubwa ya kuona jiji hili ambalo ndilo linalohakisi utajiri na maendeleo ya Tanzania. Sasa wakiingia jiji hili, tafsiri ya kila mtu atakayoipata itategemea mwenyeji wako ulikofikia, au na uwezo wa kiuchumi ulivyojipanga kabla ya kuja Dar es Salaam. Kama mwenyeji wako ni tiamaji-tiamaji au ulikuja kwa kuzamia, huwe na uhakika ya kupata tabu saana uingiapo jiji hili! Utaishi kulingana na maisha ya mwenyeji wako au kulingana na mfuko wako. Nina ujasiri kusema Wamarekani walikuwa na akili sana kusema "marekani ni ardhi ya watu huru na nyumbani kwa majasiri".
Kwahiyo nyie wageni mnaokuja Dar zingatia hili! Dar es Salaam ni mahali patakatifu na mstarehe kwa majasiri ambao hawajakaa kihasarahasara na kizembezembe!
"tukutane sheli" 😊😊😊