Kuna mapungufu makubwa kwenye sharia iliyoanzisha LST, kwanza muda wa mafunzo ni mfupi sana, muda huu hata ungerefushwa mfano kuwa mwaka mmoja na nusu kama Kenya bado isingetosha kuwafanya wahitimu kuwa mawakili wabobezi mara tu baada ya kuhitimu mafunzo yao. Tofauti na hapa kwetu, sehemu nyingi na mfano wa karibu ni hapo kwa jirani zetu Kenya, mhitimu wa Law School akumaliza bado ni lazima akae na wakili (pupilage) kwa kipindi Fulani kabla hajaruhusiwa kuanza practice, kwa Kenya ni miaka miwili. Walioandaa sharia hii wangeiga kinachofanyika kwenye fani nyingine mfano uhasibu ambapo mfano mtu aliyehitimu CPA hawezi kufanya Public Practice mpaka baada ya kipindi Fulani kupita ambapo katika kipindi hicho anakuwa anaendelea kujifunza toka kwa waliomtangulia.
Nakubaliana kabisa na hoja kwamba baadhi ya mawakili waliopitia LST hawapo kwenye viwango stahiki, hii kwa upande mmoja inasababishwa na nilichokieleza hapo juu lakini pia tukubali au kukataa kumekuwa na shida sana ya ubora wa mafunzo ya shahada ya kwanza ya sheria yanayotolewa na vyuo mbalimbali hapa nchini, hii inapelekea kuwepo kwa utofauti mkubwa wa uelewa wa wanafunzi, na kwa sasa kuna tabia kwamba waalimu wanaburuza tu wanafunzi na kuwaambia kuwa mtajifunza zaidi mkienda Law School bila kujali kwamba mtu anayesajiliwa Law School anapaswa kuwa na uelewa wa kutosha wa nadharia, na pasipo kuwa na msingi mzuri wa nadharia ni ngumu sana kujifunza kwa vitendo.
Natambua kwamba si wanafunzi wote wanaokwenda Law School of Tanzania wanakwenda kwa sababu wana malengo ya kupractice sheria, wengi wao wanakwenda kwa kuwa mfumo umewalazimisha kwenda huko, ingekuwa vyema Law School ingebaki tu kwa wale wanaotaka kufanya kazi ya uwakili wa kujitegemea au labda wanaoutazamia uwakili wa serikali na wengine wote wasingelazimishwa kwenda Law SChool.
Law School of Tanzania bado ipo katika changamoto za ukuaji, naamini kabisa baada ya muda Fulani changamoto hizi zitaoungua kama sio kwisha kabisa, ikumbukwe kuwa mpaka sasa ni takribani miaka 7 tu tangia ilipoanza kupokea wanafunzi, lakini kuna mengi mazuri yaliyofanyika ambayo yanapaswa kupongezwa. Ni rai yangu kuwa uzi huu utumike kuainisha changamoto zinazokabili Taasisi hii zaidi kuliko kutumika kama ubao wa kumalizia hasira za wale ambao kwa bahati mbaya hawajafanikiwa kumaliza mitihani yao.