Hii shule ilifunguliwa kabla haijapevuka. hadi sasa bado haijapevuka. Kabla ya hii shule mtu akitaka kuwa wakili ilimlazimu aende internship. Mawakili wa internship ni wazuri zana. Mawakili waliopitia law school ni wabovu (sio wote tafadhali). kuna wengine wanatia aibu mahakamani hadi utawaonea huruma, hawajui chochoteHii ni Shule ya Muhimu sana katika Sekta ya Sheria. Hata hivyo, Shule hii haijawahi kupewa Umuhimu unaostahili katika Jukwaa hili. Ni katika muktadha huo, kumeonekana umuhimu wa Shule hii kupata Fursa hapa Jukwaani, ikiwezekana kupewa maoni,ushauri, ili kuiboresha shule hii. Karibuni Wadau
Nakubaliana na wewe ingawa si kwa kiwango kikubwa. Nimeona Mawakili wengi wale wa Internship waki recommend kazi nzuri inayofanywa na vijana waliopita hapo. Kwa wanaoaibisha,tatizo ni shule au watu wenyewe?Hii shule ilifunguliwa kabla haijapevuka. hadi sasa bado haijapevuka. Kabla ya hii shule mtu akitaka kuwa wakili ilimlazimu aende internship. Mawakili wa internship ni wazuri zana. Mawakili waliopitia law school ni wabovu (sio wote tafadhali). kuna wengine wanatia aibu mahakamani hadi utawaonea huruma, hawajui chochote
Nchi za wenzetu kila chuo kinachotoa shahada ya sheria kina shule yake ya sheria (law school). hata hapa tanzania kulikuwa na haja hiyo, tena ingerahisisha zaidi. mwanzo ungekuwa mgumu lakini hadi sasa hali ingekuwa imestabiliseNakubaliana na wewe ingawa si kwa kiwango kikubwa. Nimeona Mawakili wengi wale wa Internship waki recommend kazi nzuri inayofanywa na vijana waliopita hapo. Kwa wanaoaibisha,tatizo ni shule au watu wenyewe?
Ni kweli pia naona Shule bado ipo kwenye Try n Error, sijui hadi lini. Maoni yako, nini kifanyike.
Umenena vyema kabisa mkuu, sina cha kuongeza wala kupunguzaKuna mapungufu makubwa kwenye sharia iliyoanzisha LST, kwanza muda wa mafunzo ni mfupi sana, muda huu hata ungerefushwa mfano kuwa mwaka mmoja na nusu kama Kenya bado isingetosha kuwafanya wahitimu kuwa mawakili wabobezi mara tu baada ya kuhitimu mafunzo yao. Tofauti na hapa kwetu, sehemu nyingi na mfano wa karibu ni hapo kwa jirani zetu Kenya, mhitimu wa Law School akumaliza bado ni lazima akae na wakili (pupilage) kwa kipindi Fulani kabla hajaruhusiwa kuanza practice, kwa Kenya ni miaka miwili. Walioandaa sharia hii wangeiga kinachofanyika kwenye fani nyingine mfano uhasibu ambapo mfano mtu aliyehitimu CPA hawezi kufanya Public Practice mpaka baada ya kipindi Fulani kupita ambapo katika kipindi hicho anakuwa anaendelea kujifunza toka kwa waliomtangulia.
Nakubaliana kabisa na hoja kwamba baadhi ya mawakili waliopitia LST hawapo kwenye viwango stahiki, hii kwa upande mmoja inasababishwa na nilichokieleza hapo juu lakini pia tukubali au kukataa kumekuwa na shida sana ya ubora wa mafunzo ya shahada ya kwanza ya sheria yanayotolewa na vyuo mbalimbali hapa nchini, hii inapelekea kuwepo kwa utofauti mkubwa wa uelewa wa wanafunzi, na kwa sasa kuna tabia kwamba waalimu wanaburuza tu wanafunzi na kuwaambia kuwa mtajifunza zaidi mkienda Law School bila kujali kwamba mtu anayesajiliwa Law School anapaswa kuwa na uelewa wa kutosha wa nadharia, na pasipo kuwa na msingi mzuri wa nadharia ni ngumu sana kujifunza kwa vitendo.
Natambua kwamba si wanafunzi wote wanaokwenda Law School of Tanzania wanakwenda kwa sababu wana malengo ya kupractice sheria, wengi wao wanakwenda kwa kuwa mfumo umewalazimisha kwenda huko, ingekuwa vyema Law School ingebaki tu kwa wale wanaotaka kufanya kazi ya uwakili wa kujitegemea au labda wanaoutazamia uwakili wa serikali na wengine wote wasingelazimishwa kwenda Law SChool.
Law School of Tanzania bado ipo katika changamoto za ukuaji, naamini kabisa baada ya muda Fulani changamoto hizi zitaoungua kama sio kwisha kabisa, ikumbukwe kuwa mpaka sasa ni takribani miaka 7 tu tangia ilipoanza kupokea wanafunzi, lakini kuna mengi mazuri yaliyofanyika ambayo yanapaswa kupongezwa. Ni rai yangu kuwa uzi huu utumike kuainisha changamoto zinazokabili Taasisi hii zaidi kuliko kutumika kama ubao wa kumalizia hasira za wale ambao kwa bahati mbaya hawajafanikiwa kumaliza mitihani yao.
Mkuu Dragoon,Hii shule ilifunguliwa kabla haijapevuka. hadi sasa bado haijapevuka. Kabla ya hii shule mtu akitaka kuwa wakili ilimlazimu aende internship. Mawakili wa internship ni wazuri zana. Mawakili waliopitia law school ni wabovu (sio wote tafadhali). kuna wengine wanatia aibu mahakamani hadi utawaonea huruma, hawajui chochote
Mwenye kitabu cha anson's law of contract katika soft copy anisaidieWateja mahakamani wanalalamikia sana mawakili waliosoma vyuo vya MIAKA MITATU ,tofauti na St .Augustine(RUCO)-Iringa & Udsm ambapo wanasoma MIAKA 4 na wapo vizuri upstairs!
Kwa mwenemdo huu hata ajira imekuwa hawapewi hawa wanafunzi wanaosoms miaka 3.
Ndalichako tuokoe na hivi vyuo vya miaka mitatu!
Take action madame,please rescue us,we humbly pray so!
Pia wanapinga ada ya dola 50 kwa EALS