AKILI TATU
JF-Expert Member
- Feb 10, 2016
- 2,659
- 2,827
Bill Shankly
KILA mtu aliamini hatuendi popote, wengi walitarajia kuona tunashindwa kufuzu hatua ya 16 ya michuano ya Ligi ya Mabingwa msimu wa 2004/05.
Njia yetu ilikua ni ngumu, kundi letu lilishageuka shubiri kwetu, hatukua na matumaini tena.
Tulikua tupo na Monaco, Olyimpiacos na Deportibo LA Coruna. Ngoma ilikua ngumu kweli kweli.
Mpaka michezo ya mwisho ya kumaliza hatua ya makundi inafika bado Liverpool hatukua na uhakika wa kufuzu.
Olympicos walikua kileleni na alama 10, Monaco wakifuata na alama Tisa, sis tukishika nafasi ya tatu tukiwa na pointi saba wakati Deportivo wakishika mkia na zao mbili.
Hivyo mchezo wa mwisho ilituhitaji Liverpool tushinde idadi ya magoli mawili ili tufuzu.
Na tulikua tunawakabili Olyimpiacos katika dimba letu la Anfield.
Tuliwachapa goli 3-1 na kumaliza wapili nyuma ya Monaco tukiwa na alama 10 tukiwaacha Olyimpiacos kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa.
Baada ya hapo hatukushikika, breki yetu ilikua katika jiji la Instabul tulipoibuka mabingwa mbele ya Milan.
Kutoka kuwa timu isiyopewa nafasi ya kufuzu kwenye makundi hadi kuwa mabingwa wa Ulaya.
TUELEWANE SASA
Nini nataka kusema? Kwanini nimeongea yote hayo huku juu!? Sisi Liverpool hatupitagi njia nyepesi hata Siku moja.
‘ The Liverpool Way, The Hard Way’ Njia yetu ni ngumu siku zote.
Jumatano ya juzi tumefungwa goli 2-1 na PSG katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa.
Kabla ya hapo tulitoka kuchapwa na ‘watoto’ Red Star Belgrade mabao 2-0. Lakini kichapo cha PSG kilimaanisha kuwa sasa nafasi yetu ya kwenda hatua ya 16 bora ni ngumu.
Tayari Napoli anaongoza kundi akiwa na pointi Tisa, PSG anazo nane sisi tuko na alama zetu sita wakati Red Star wako na nne.
Hali ni ngumu kwetu na wapinzani washaanza kutukaribisha Europa.
Wanashindwa kuelewa kwamba sisi njia zetu ni ngumu, kama utatuambia tuchague tupite njia yenye swala au Simba basi sisi tutachagua hiyo yenye Simba.
Anfield patakua ni sehemu chungu sana kwa Napoli watakapokuja kwa ajili ya mchezo wetu wa mwisho.
Tutawafanya kitu ambacho Dunia nzima itatikisika, nawaonea huruma maana PSG wamechokoza mzinga wa nyuki halafu msala wamewaachia Napoli.
Tunafahamu Carlo Ancellot ni kocha imara na mzoefu wa Uefa lakini yeye mwenyewe ni mhanga wa falsafa ya ‘The Liverpool way The Hard way’.
Ugumu wa njia tuliyopita 2005 tukaenda kubeba kombe mbele ya Ancellot ndio huu huu ambao tunakutana nao msimu huu.
Ili tufuzu hatua ya 16 bora inatubidi tumchape Napoli idadi ya magoli mawili bila au 3-1 au 4-2 yaani utofauti lazima uwe magoli mawili.
Ni sawa na hali ilivyokua 2005, Napoli wamesogea karibu na mdomo wa Mamba.
Ni vema wakawapigia simu Olyimpiacos wawaulize hali ilikuaje Anfield.
Liverpool mahala pake ni fainali ya Ulaya na kwetu usiku wa Ulaya huwa na maana kubwa sana hatutakagi kuipoteza hiyo nafasi.
Hizo ndizo mechi ambazo mashabiki wa Liverpool hugeuka vichaa, wachezaji huvua ngozi zao za kibinadamu.
Hatutosikia la mnadi swala wala sauti za kanisa tunahitaji alama tatu na magoli ya kutuvusha hapa tulipo.
Uzuri Liverpool na Jurgen Klopp tumekutana wote tunapenda michezo yenye presha, wote njia zetu za mafanikio huwa ni ngumu.
Mechi na Napoli ndiyo utayaona macho ya Klopp yalivyo makali, sura yake ya kikuli kutoka Stuggart hujionesha dhahiri.
Ni mchezo ambao hatutojali sana kuhusu ‘fair play’ shida yetu ni kushinda na kufuzu.
Mizimu ya wazee wetu John Holding, Bill Shankly na Bob Paisley yote imetuhakikishia kwamba tutafuzu hatua ya 16 bora.
Niwaambie ukweli tukifuzu hatua hii basi ujue mwisho wenu umefika hatutokua na wa kutuzuia hadi fainali.
Tukifuzu hapa breki yetu itakua fainali na safari hii hatutokubali tupishane nalo kwa gharama yoyote litarudi Merseyside.
0683015145