Fabio Capello: "Unajua sipendi nini kuhusu [Pep] Guardiola? Kiburi chake. #UCL aliyoishinda na #ManCity ilikuwa ya pekee ambayo hakujaribu chochote cha ajabu katika mechi muhimu.
"Miaka mingine yote, akiwa Manchester na Munich, katika siku muhimu kila mara alitaka kuwa mhusika mkuu. Alibadilisha mambo, akaanzisha uvumbuzi ili aweze kusema, 'Wachezaji hawashindi, mimi ndiye ninashinda'. Kiburi hiki kilimgharimu Ligi kadhaa za Mabingwa..."
"Ingawa sasa si kosa lake tena, amefanya madhara makubwa kwa soka… Kila mtu amekuwa akijaribu kumwiga kwa miaka 10, jambo hilo limeharibu soka..."