Ubingwa wa Azam kombe hili la Mapinduzi na mwenendo mzuri wa timu hii katika mashindano mengine including ligi ni mapinduzi ya kweli kwa soka la Tz hasa kwa watanzania wenye mawazo mgando kuhusu usimba na uyanga.
Pamoja na yote, bado ni mapema sana Azam FC kuongea kwa majivuno . . . . . .
Simba na Yanga zina matatizo kutwa nzima ambayo Azam FC hawana, lakin Azam wana nin cha kujivunia zaid ya hapo mbele ya Simba na Yanga??
Tatizo moja kubwa ninalolihofia ambalo Azam FC wanalo na linaweza kuiua timu yao ni umiliki wa mtu binafsi/kumilikiwa na kampuni. Kama ilivyotokea kwa Reli, Kajumulo FC, Sigara, Pamba, CDA, Biashara Shinyanga, Ushirika Moshi, Bandari Mtwara n.k.
Uzoefu unaonyesha kuwa timu nyingi zenye umilikiwa wa aina hii huwa hazidumu. Zinazodumu ni timu zilizojibadilisha ZENYEWE kuwa kampuni then zikaja kumilikiwa na wawekezaji wengine.
So Azam FC kwa sasa naiweka ktk kundi moja na timu hizo hapo juu ambazo nazo kwa nyakati tofauti ziliwahi kuzidunda Simba na Yanga mara kibao, hasa hasa Reli, Sigara na Pamba . . . . lakin Hata Kagame hazijawahi kugusa.
Kumiliki mabasi makali, viwanja vikali, n.k. haitakuwa na maana yoyote kama games zao ni kuzifunga Simba na Yanga huku ikifungwa au kupata sare na Villa Squad, African Lyon, Moro Utd, Polisi Dodoma, Coastal Union n.k.
Pamoja na yote, bado ni mapema sana Azam FC kuongea kwa majivuno . . . . . . Simba na Yanga zina matatizo kutwa nzima ambayo Azam FC hawana, lakin Azam wana nin cha kujivunia zaid ya hapo mbele ya Simba na Yanga??Tatizo moja kubwa ninalolihofia ambalo Azam FC wanalo na linaweza kuiua timu yao ni umiliki wa mtu binafsi/kumilikiwa na kampuni. Kama ilivyotokea kwa Reli, Kajumulo FC, Sigara, Pamba, CDA, Biashara Shinyanga, Ushirika Moshi, Bandari Mtwara n.k.Uzoefu unaonyesha kuwa timu nyingi zenye umilikiwa wa aina hii huwa hazidumu. Zinazodumu ni timu zilizojibadilisha ZENYEWE kuwa kampuni then zikaja kumilikiwa na wawekezaji wengine.So Azam FC kwa sasa naiweka ktk kundi moja na timu hizo hapo juu ambazo nazo kwa nyakati tofauti ziliwahi kuzidunda Simba na Yanga mara kibao, hasa hasa Reli, Sigara na Pamba . . . . lakin Hata Kagame hazijawahi kugusa.Kumiliki mabasi makali, viwanja vikali, n.k. haitakuwa na maana yoyote kama games zao ni kuzifunga Simba na Yanga huku ikifungwa au kupata sare na Villa Squad, African Lyon, Moro Utd, Polisi Dodoma, Coastal Union n.k.
Mkuu wangu CPU ni kweli lakini tutofautiane kidogo...Azam hawana cha mno cha kujivunia kwa sasa hasa linapokuja suala la ushindi kwa idadi ya vikombe kwa sababu kadhaa lakini kubwa ikiwa ni upya wa timu yenyewe na ukweli kwamba ili itambe katika soka la bongo kwa huko tuendako ni lazima izishinde Simba na Yanga kwa kila kitu, ni dhahiri kwa sasa wamewashinda kiuchumi na mipango thabiti ya kuendeleza soka lakini bado kuwashinda kwa fitina.
Hili la mwisho la Fitna litawasumbua sana Azam hasa kwa vile Simba na Yanga ni zaidi ya timu za soka, Simba na Yanga ni dini, kabila na utamaduni. Zimechangia ku-polarize soka la Tanzania katika kambi hizo mbili na kwa kweli hii imekuwa ni changamoto kwa soka letu na maendeleo ya michezo kwa ujumla wake.
Ni imani yangu kuwa hii polarization itakuwa kifo cha kawadia kadiri maendeleo ya sayansi na teknolojia yanavyokuwa na influence ya European football hapa Tz. Tunaelekea kuwa na kizazi ambacho hakitosumbuliwa na mzimu wa Simba na Yanga na hapo ndipo azam itakuja kuwa timu kubwa na ya kupigiwa mfano.
Naamini kwamba wakati watu watakapokuja kugundua potential iliyopo katika football kama entertainment lakini pia kama ajira, fitina hazitokuwa na nafasi na azam itakuwa timu ya kwanza kufaidika, na bila shaka hii ndiyo long term idea ya tajitri wa azam bwana Abubakar Bakhresa. Ingawa ni ndoto kwa sasa na kwa asili si rahisi kuwashawishi watanganyika wengi juu ya uwezekano kama huu, maana kwa asili ashakum si matusi watz tuna sifa ya kuwa short sighted, mwisho wa fitina za Simba na Yanga hauko mbali sana na kama wenzao wa Gor Mahia na AFC Leopard walivyoteketea na kulazimika kuanza upya huku klabu kama Sofapaka, Tusker zikiibuka, nao hawana mwisho mwema hasa nguzo zao katika maeneo ya kufanyia maamuzi zitakapoanguka iwe ni katika TFF, BMT au Sirikalini.
Kuhusu Azam kufungwa na vitimu vidogo huku wakiwatoa jasho simba na yanga, nadhani ni suala la kisaikolojia zaidi kwa azam players lakini pia tunarudi kwenye kipengele cha fitina. Mfano kuna tetesi kuwa kipa wa Azam wa msimu uliopita, mrundi Vladmir Niriyonku alihongwa na yanga ktk mechi za mwishoni ili kuhujumu timu ifungwe hovyo ili kuwanusuru Yanga walau wapate nafasi ya pili. Unaweza kujiuliza ilikuwaje kwa mrundi huyo kuachwa wakati alikuwa ni kipa namba moja...sababu ni hiyo. ni vigumu kuthibitisha lakini kama ilivyo kwa kesi zote zinazohusu rushwa, mazingira yalimkamata na hatimaye kutemwa. Na hapo unaweza kujua kwa nini azam walimsajili Cirkovich, ni kwa sababu walidhani kwamba b'se yeye aliachwa na yanga kwa fedheha basi itakuwa vigumu kwa aidha yanga au simba kumhadaa kwa virushwa vya milioni wakati hapo azam anapata zaidi ya hizo.
Anyway...tuwape muda Azam, they look very promising...Achana na hizo timu ulizozitaja, enzi hizo football ilikuwa ni ridhaa wakati kwa azam football ni profession. as for kajumulo siwezi kusema sana bse simfahamu vizuri zaidi ya kuwa alikuja na mbwembwe nyingi akijidai ni player/sponsor, akaichukua timu ya sigara na biashara ikaishia hapo.Mwisho naomba niwe mtabiri, kati ya simba na yanga, nadhani itaanza kufa yanga na kufuatiwa na simba. lakini simba inaweza isife bali ikajivua gamba na kwenda na upepo ila yanga..its more or less like ccm...sidhani kama ina maisha marefu sana.