The Official Azam FC Thread

mpira wanashambuliana sana timu zote mbili huku kocha wa lyon ndugu otieno amepigwa kadi na kuondolea kwenye benchi kwa kosa la kumfokea mwamuzi..
 
gooooooooo kipreeeeeeeeeeeeee

Dk 61 azam 3 - 1 a lyon
 
hili goli limemfanya kipre tchetche kuwa na magoli 15 kwenye ligi kuu tanzania..
 
Jacob masawe wa lyon yupo chini hapa..
 
kingwande amepeleka bonge la shuti na manula kalida duu huyu dogo hatari tupu..
 
Sub azam
Karihe seif in abdi kasim out
 
hapa mchezo leo wamecharukiana balaa maana hizi tatu sio mchezo..

sunday juma booked yellow card
 
Hapa naona aishi yupo chini kiaina..
 
Full Time: Azam FC 3 - 1 A Lyon kipre cheche 9' 61' mcha 32' na kingwande 36'
 
Wachezaji wote wanne waliosimamishwa kupisha uchunguzi wa tuhuma za rushwa dhidi yao wameripoti kambini tayari kuikabili Simba SC siku ya jumapili

Aggrey Morris na Erasto Nyoni wakifuatilia mchezo kati ya Azam FC na African Lyon, Picha kwa hisani ya Blogu ya Binzubeiry Kurejea kwa wachezaji hao kunamaliza mgogoro uliokuwepo na kudumu kwa takribani miezi mitano kufuatia shutuma za rushwa ambazo zilipelekwa takukuru kuchunguzwa ili kujua ukweli na uongozi wa Azam FC unaishukuru takukuru kwa kazi nzuri ambapo imegundulika kuwa wachezaji hao hawakuhusika na hivyo kusafishwa na chombo hicho chenye mamlaka ya kuchunguza tuhuma za rushwa.

Wachezaji hao wote wanatarajiwa kuwemo kwenye mchezo wa Jumapili dhidi ya Simba SC ikiwa mwalimu ataona inafaa na wapo katika hali nzuri kuweza kucheza. Mchezo huo wa jumapili ni muhimu sana kwa Azam FC kwani ikishinda itaizidi Simba SC pointi 14 huku simba ikisaliwa na michezo minne na hivyo kumaanisha kuwa Kagera Sugar atabaki kuwa mpinzani pekee wa Azam FC katika kuwania nafasi ya pili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…