The Official Azam FC Thread

[h=3]AZAM NA WA MOROCO 5000[/h]
Mchezo wa awali wa raundi ya pili ya kombe la shirikisho kati ya azam fc na AS FAR Rabat ya Moroco utakaochezwa jumamosi ya april 20 katika uwanja wataifa jijini Dar es salaam kiingilio cha chini ni tsh 5000.Tsh 5000 ni kwa viti vya blue na green wakati vya orange vinatozwa kwa Tsh 10000, VIP C ikiwa Tsh 15000 wakati VIP B ni Tsh 20000 na VIP A ni Tsh 30000.
Kikosi cha wa Moroco hao kimewasili nchini jana.
 
Habari nzuri kwetu sisi Watanzania wapenda soka kuwa Azam FC itafanya vizuri dhini ya timu kutoka Morocco AS FAR RABAT :

:msela:Friday, April 19, 2013


KALLY; TUMEPATA DVD ZAO NA TUMEZIFANYIA KAZI



Kocha msaidizi wa azam fc, Kally Ongala leo katika mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa kesho wa kombe la shirikisho, amebainisha kuwa wamepata DVD ya michezo mitatu ya AS FAR RABAT, wakati wa kocha wa AS FAR RABAT akibainisha yakuwa hawaifahamu azam fc.

Ongala amesema wamepata DVD za mechi tatu za mwisho za AS FAR Rabat, moja ikiwa dhidi ya timu ya Al Nasir ya Libya ambayo waliitoa katika raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho na nyingine mbili za ligi ya Morocco ambazo wanazifanyia kazi kuhakikisha wanashinda kesho.

Naye Ouadani amesema hawaifahamu vizuri Azam, lakini wanaujua mpira wa Tanzania baada ya kuangalia mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Morocco uliochezwa machi 23 mwaka huu na kumalizika kwa Tanzania kuibuka na ushindi wa goli 3-1.

Kesho saa 10 alasiri azam fc watawakaribisha AS FAR Rabat katika mchezo wa awali wa raundi ya pili katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

AS FAR Rabat inawachezaji 6 katika kikosi cha Moroco kilichopokea kichapo cha goli 3-1 toka kwa Tanzania, wakati azam fc wakiwa na wachezaji wa 5 katika kikosi hicho cha Tanzania lakini alibahatika kucheza ni mmoja kiungo mchezeshaji Salum Aboubakary 'Sure Boy'.
Source: Azam Fans Club
 
Azam FC Jana imevunja rekodi iliyowekwa miaka 13 iliyopita na Simba SC wakati walipofika fainali za kombe la CAF kwa kucheza Mechi tano za awali bila kupoteza, Hadi sasa Azam FC imecheza Mechi 5, imeshinda 3 na kwenda sare 2
 
Timu ya Azam FC itasafiri kuelekea Morocco Jumapili hii tarehe 28/04/2013, itakaa Morocco kwa siku sita ili kuzoea hali ya hewa kutokana na ratiba ya mchezo wa marudiano kuonesha kuwa mchezo huo utachezwa Jumapili tarehe 05/05/2013.... Azam FC itasafiri na wachezaji wote waliosajiliwa kwa mashindano haya isipokuwa Abdulhalim Humoud aliyehamia Afrika ya kusini na Samih Nuhu aliye na Majeruhi, pia benchi lote la ufundi litasafiri... kiujumla msafara wa Azam FC utakuwa na watu 55.... Tumedhamiria kushinda kwao na kuwatoa.

Mungu ibariki Azam FC, Mungu ibariki Tanzania
 

Asante Mkuu (Ndetichia),
Lazima tuwaonyeshe wakongwe kuwa kila kitu Azam FC kinakwenda kisanyansi maana hali ya hewa huko Morocco mwezi Mei huwa : [h=2]Location: Rabat/Salé, Morocco[/h]
This report describes the typical weather at the Rabat-Salé Airport (First Royal Air Force Base) (Rabat/Salé, Morocco) weather station over the course of an average May. It is based on the historical records from 1974 to 2012. Earlier records are either unavailable or unreliable.
Rabat/Salé has a mediterranean climate with dry hot summers and mild winters. The area within 40 km of this station is covered by oceans and seas (40%), forests (29%), croplands (21%), and grasslands (8%).


[h=2]Temperature[/h]The month of May is characterized by gradually rising daily high temperatures, with daily highs increasing from 21°C to 23°C over the course of the month, exceeding 27°C or dropping below 18°C only one day in ten.
 
Mechi ya Leo Kati ya Azam FC na Coastal Union itarushwa live na star tv na kutangazwa na Kiss FM, usikose!!

forza azam fc
 
Kikosi cha Azam FC ambacho kitashuka Dimbani jioni ya leo kwenye uwanja wa C.C.M Mkwakwani kumenyana na Coastal Union. Mechi itaanza saa kumi na robo na kama kawaida, Star TV Africa na Radio Free Africa pamoja na Kiss FM watakuwa hewani kuwaletea mpambano huo.

1. Mwadini Ali
2. Himidi Mao
3. Erasto Nyoni
4. David Mwantika
5. Aggrey Morris
6. Ibrahim Mwaipopo
7. Brian Umony
8. Jabir Aziz
9. Gaudence Mwaikimba
10. Humphrey Mieno
11. John Bocco (C)

Wa akiba ni;
Aishi Manula
Malika Ndeule
Saidi Mourad
Abdi Kassim
Seif Karihe
Kipre Tchetche

VIJANA WAMEAHIDI KUTOA ZAWADI YA MIAKA 49 YA MUUNGANO!
 
full time CUSC 1 - 1 Azam moris aggrey 58' D lyanga 68'
 
[h=3]AZAM WATUA SALAMA CASABLANCA[/h]

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kombe la shirikisho Azam fc wametuwa salama jijini Casablanca, Moroco kwa ajili ya mchezo wa kombe la shirikisho hatua ya tatu dhidi ya AS FAR Rabat.Kwa mujibu wa taarifa iliyowekwa katika ukurasa wa azam fc ndani ya facebook, inaeleza kuwa wamefika salama na wamepewa basi walilotumia kusafiria toka Casablanca mpaka Rabat.

"Azam FC imetua salama Casablanca na kusafiri kwa basi umbali wa kilometa 100 hadi Rabat na kufikia katika hoteli ya Golden Tulipo mjini
Rabat," ilieleza taarifa toka katika ukurasa wa azam fc.
Msemaji wa Azam fc Japhari Iddi Maganga akizungumza na moja ya redio hapa nchini, akiwa huko Moroco amesema kuwa wenyeji wao AS FAR Rabat waliwapokea vizuri katika uwanja wa ndege wa Casablanca na kuwapatia basi lililowafikisha katika mji wa Rabat.
Maganga aliongeza kuwa wachezaji leo watapewa mapumziko kutokana na uchofu wa safari ulichuku takribani masaa 15 na kesho wanataraji kuendelea na program ya maandalizi dhidi ya mchezo huo utakao chezwa jumamosi.
Msafara wa pili wa Azam fc uliondoka nchini jana mida ya jioni wakitumia ndege ya Emirates wakipitia Dubai ambapo walilala jana kabla ya kuunga safari ya kuelekea Casablanca, Moroco.
Azam fc wanaitaji sare ya magoli katika mchezo huo baada ya mchezo wa awali kumalizika kwa sare ya bila kufungana.
 
Azam FC ipo mjini Rabat ikijiandaa kukabiliana na AS FAR kwenye mechi ya raundi ya mwisho ya 16 bora za kombe la shirikisho. Azam FC imetua hapa na wachezaji 23, benchi lote la ufundi isipokuwa Ibrahim shikanda pekee aliye masomoni Nairobi na uongozi karibu wote na kwa pamoja kama timu Azam FC ina dhamira ya kuifunga na kuisukuma nje ya mashindano timu ya AS FAR.
Kuna sababu sita zinazoifanya Azam FC iamini na ijiamini kuwa inaweza kushinda kwenye mtanange wa jumamosi hii. Sababu hizo ni maandalizi bora, wachezaji wazuri, Uongozi Mzuri, benchi bora la ufundi chini ya Stewart Hall, Mipango mizuri na dhamira ya kupata mafanikio. Makala hii itakayowajia katika sehemu tatu itachambua vipengele vilivyoaninishwa hapa chini.
MAANDALIZI MAZURI
Timu za Tanzania kwa miaka mingi zimekuwa zikishiriki mashindano ya kimataifa yanayoandaliwa na CAF, kwa Azam FC hii ni mara yake ya kwanza kupata nafasi hii. Lakini unaweza kuona utofauti mkubwa wa maandalizi kati ya Azam FC na timu nyingi za Tanzania na utofauti huo ndiyo unaoifanya Azam FC hadi sasa kuweza kucheza mechi tano pasi na kupoteza mchezo hata mmoja.
Azam FC baada ya kujua kuwa itawakilisha nchi kwenye mashindano ya kimataifa iliamua kufanya juhudi za makusudi za kujiandaa kwa kiwango cha mashindano hayo yanayoandaliwa na CAF.
Azam FC ilifanya ziara na kucheza mechi nane za kimataifa za kirafiki nje ya ardhi ya Tanzania, ilikwenda Kinshasa Congo DRC na kushiriki Congo Charity Cup ambako ilitwaa kikombe kabla ya kusafiri tena hadi Nairobi ambako ilipata nafasi ya kucheza mechi nyingine tatu.
Lengo la ziara hizi ilikuwa ni kuwapa ukomavu na uzoefu vijana wake ili wanapokuwa kwenye mashindano ya CAF hasa wanapocheza mechi za ugenini wasiwe na hofu. Hakika matunda ya ziara hizi tunayaona kwani Azam FC imeshinda ugenini mechi zake zote mbili za awali hadi sasa.
Maadalizi ya Azam FC kwenye mashindano haya pia yalihusisha utafutwaji na usajili wa wachezaji wenye viwango vya kuweza kucheza na kuisaidia timu, uboreshwaji wa kambi ya mazoezi ya Chamazi mapema kwa ajili ya kambi ya nyumbani, ununuzi wa vifaa bora vya mazoezi na kadhalika.


UWEZO WA WACHEZAJI
Timu ni wachezaji, bila ya wachezaji bora wenye nidhamu, viwango bora na malengo ni sawa na bure. Azam FC ililitambua hilo mapema… Azam FC haikukurupuka kusaka wachezaji kwa mkupuo, usajili wa wachezaji kwa ajili ya mashindano ya CAF ulifanyika kwa umakini kwa muda mrefu huku klabu ikijiwekea malengo ya kuwa na kikosi bora kitakochoweza kupambana na kuvifunga vigogo vya soka la Afrika.
Leo ukiwaangalia wachezaji 25 wa Azam FC waliosajiliwa kwenye mashindano ya CAF utaungana nami kuwa ni wachezaji sahihi kwa mashindano haya.
Wachezaji wa Azam FC wana nidhamu na vipaji vya hali ya juu. Wote wana viwango vya kuweza kuwemo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania na kuanza kwenye kikosi cha kwanza. Hapa nitazungumzia sifa za wachezaji wa eneo la ulinzi tuu kwa ufupi… halafu muendelezo wa makala hii utawaletea wachezaji wa kiungo na baadaye washambuliaji.

MWADINI ALLY
; Golikipa chaguo la kwanza la kikosi cha timu ya Taifa ya Zanzibar na sehemu ya kudumu ya kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania. Ana uzoefu mkubwa wa michezo ya kimataifa akiiongoza Zanzibar kushika nafasi ya tatu mara mbili kwenye mashindano ya CECAFA. Ni golikipa hodari ambaye Azam FC tunajivunia kuwa naye

AISHI MANULA, utasemaje juu ya kipaji cha kijana huyu toka Morogoro? Wengi wanamfananisha na golikipa wa zamani wa Tanzania na Simba Mohammed Mwameja. Aishi anajiamini, ana umbo zuri na kipaji kikubwa sana. Ndiyo maana haishangazi kwa nini yeye ni golikipa namba moja wa timu za vijana za taifa na chaguo namba tatu la Taifa Stars ya kocha Kim Poulsen

HIMID MAO; Ana miaka 20 tuu lakini ni mkongwe ndani ya kikosi cha Azam FC, Himid ni kiungo mwenye sifa za kukaba ambaye sasa anacheza kama beki wa kulia wa Azam FC. Hakuna aliyeshangaa jina lake lilipoitwa na Kim Poulsen kuwa sehemu ya wachezaji 30 bora nchini wanaonyemelea nafasi za walio timu ya Taifa. Himid Mao aliibukia kwenye mashindano ya Copa Cocacola na baadaye kuwa nahonda wa timu za taifa za Tanzania chini ya miaka 20. Kabla ya mwalimu wa wakati huo wa Azam FC Itamar Amorim kumpa nafasi kwenye kikosi cha kwanza akitokea Azam Academy. Himid anafanya vizuri sana kwenye kikosi cha Azam FC hadi sasa.

WAZIRI SALUM; huenda ndiye mchezaji mwenye kipaji kikubwa cha kumiliki mpira kuliko wachezaji wote nchini Tanzania kwa sasa. Waziri Salum, naye yumo kwenye daftari la kocha Kim Poulsen na ni mwanachama wa kudumu wa kikosi cha Zanzibar heroes. Mguu wake wa kushoto ni kama mkono wa paka kwani anaweza kufanya lolote na mpita kwa kutumia mguu huu. Ana mbinu za kukaba, ana krosi za hatari na chenga za maudhi. Ni hadhina kubwa kwa Azam FC na taifa la Tanzania

JOCKINS ATUDO; beki bora wa ligi kuu ya Kenya KPL msimu uliopita Jockins Atudo alitua Azam FC wakati wa dirisha dogo la Disemba mwaka jana ili kuimarisha ukuta wa Azam FC kwa ajili ya mashindano haya. Tangia atue Azam FC Atudo amethibitisha kuwa waliomchagua kuwa beki bora hawakukosea. Kocha wa zamani wa Harambee Stars James Nandwa alisema wakati tunataka maoni yake juu ya atudo kabla ya kumsajili kuwa ukiwa na beki kama Atudo unapata vitu viwili, kwanza uongozi ndani ya uwanja pili beki mwenye kipaji, nguvu, kimo na kujitolea… hakika kila kocha angependa kuwa na Atudo kwenye kikosi chake

LUCKSON KAKOLAKI; labda ndiye mchezaji mwenye busara zaidi kwenye kikosi cha Azam FC kiasi kwamba wachezaji wenzake wanamuheshimu na kumkubali kama kaka. Busara hizi za nje ya uwanja pia unaweza kuziona ndani ya uwanja mbapo Luckson amekuwa mhimili mkuu kwa Azam FC hasa pale eneo la ulinzi linapokabiliwa na majeruhi. Kiwango chake cha uchezaji kimekuwa cha uhakika wakati wote na hili alilithibitisha kwenye mechi ya awali dhidi ya AS FAR ambapo aliingia katika dakika ya sita baada ya Atudo kuumia na kucheza kwa ustadi mkubwa sana Luckson ni mchezaji mmoja wapo ambaye tunaweza kusema ana damu ya bluu (yaani ana damu yenye rangi ya Azam FC)

DAVID MWANTIKA; Tanzania tumejaaliwa kuwa na mabeki wazuri lakini hatujawahi kuwana beki wa kiwango cha David Mwantika tangia kuondoka kwenye ramani ya soka kwa Boniface Pawasa. Mwantika hapitiki kwa namna yoyote ile… Mwantika ana nguvu za asili na mwili uliojengeka. Wenyewe wanyakyusa wanamuita Bedui… Mwantika ana spidi ya upepo na amekuwa maarufu ndani ya wachezaji wa Tanzania lakini alikuwa na umaarufu mdogo nje kutokana na timu yake ya Prisons kutopewa nafasi sana na vyombo vya habari. Lakini ukikutana na washambuliaji wa ligi kuu watakuambia kuwa beki wanayemuogopa zaidi nchini ni David. Juzi kim Poulsen amemjumuisha kwenye kikosi chake na bila shaka wala wasiwasi Mwantika atavuka kwenye kikosi cha Young taifa Stars na kuingia kwenye kikosi cha kwanza cha Taifa Stars muda si mrefu

Katika makala zijazo, tutawaletea maelezo ya wachezaji waliosalia wa kiungo na ushambuliaji pamoja na sababu nyingine nne zilizosalia za kwa nini Azam FC itaifunga AS FAR ambazo ni UONGOZI BORA, BENCHI BORA LA UFUNDI, MIPANGO MIZURI, na DHAMIRA
 
TIMU IMEFIKIA KATIKA HOTEL HII YA GOLDEN TULIP

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…