The Official Azam FC Thread

TUMEOONGOZA!

Klabu ya Azam FC imeongoza kutoa wachezaji wengi wanaounda kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania- Taifa Stars. Azam imetoa jumla ya wachezaji 9,ikifatiwa na Yanga na Simba zenye wachezaji 6 kila moja , TP Mazembe ya DRC na Mtibwa Sugar zenye wachezaji 2 na JKT yenye mchezaji 1. Hii inaonyesha ni namna gani Azam FC kila uchao inazidi kuimarika na kuwa bora hapa nchini, inataoa mchango stahiki kwa Taifa na mapinduzi ya kweli kwenye soka la Tanzania. Wachezaji wa Azam walioteuliwa Stars ni;
Mwadini Ali
Erasto Nyoni
Waziri Salum
Aggrey Morris
Salum Abubakar 'sure boy'
John Bocco
Mcha Khamisi
Mudathiri Yahya
Aishi Salum

VIVA AZAM FC!!!!!!!!!
 
Namuona yule bubu wa simba aliyeamia yanga kwa mkopo..
 
Chini ya Kapeti..

Katika mpango wa Azam FC kuanzisha TV yake yenyewe, Bakhresa amepanga kumwaga Bil 1.5 kwa timu zote za Ligi Kuu mwakani ili kuonesha LIVE mechi zote za ligi mwakani. Simba na Yanga zimekomaa zikitaka mgao mnene zaid kuliko klabu zote za Ligi hiyo. Mitambo ya Azam FC inajengwa sehemu moja iliyopo barabara ya Mandela jijini Dar.
 
TANZIA

Tunasikitika kutangaza Msiba wa baba mlezi wa mchezaji wetu kipenzi Salum Abubakar Sure Boy Mzee Amidu Kigoda Abeid aliyefariki usiku wa kuamkia leo, kwa sasa ni mapema mno kusema taratibu za mazishi na msiba lakini pindi tutakapopata habari kamili tutawataarifu, NOTE: aliyefariki ni Baba Mlezi wa Salum Abubakar MZEE AMIDU KIGODA ABEID
 
Naamini Bakhresa kuonyesha ligi itazisaidia timu za Tanzania kuongeza kipato na kupunguza ukiritimba wa Simba na Yanga
 
Naamini Bakhresa kuonyesha ligi itazisaidia timu za Tanzania kuongeza kipato na kupunguza ukiritimba wa Simba na Yanga

kweli kabisa mkuu maana wanajifanya walipwe kama timu za ulaya wakati hawana vigezo ndio hapo sasa tuombe uzima na kufanikisha kwa hii mambo..
 
"HATUNA MPANGO NA KAPOMBE"

Wakati Simba na Yanga wakiendelea na usajili kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu ya vodacom, timu inayo leta changamoto kwa vigogo hao wa soka nchini Azam FC wao bado hawajaanza mawindo wa kusaka nyota watakao ongeza nguvu katika kikosi chao.

Azam FC wamekuwa wanavumishwa kuanza mazungumzo na beki wa Simba Shomari Kapombe sambamba na kipa wa simba Juma Kaseja ambapo tetesi hizo zimezimwa na uongozi wa Azam FC.

Msemaji wa Azam FC Japhari Iddi Maganga amesema kuwa bado hawajapokea ripoti ya kocha mkuu Stewart Hall, na kupelekea kutokuwa katika mawindo ya mchezaji wowote yule anaye vumishwa kusajiliwa na Azam FC.

Maganga alisema kuwa Azam FC bado hawajaanza mazungumzo na mchezaji yoyote kwa ajili ya msimu ujao, na hawafahamu yupi ataachwa mpaka pale watakapo pewa ripoti ya kocha mkuu.

Maganga amesema kuwa Hall bado yuko nchini na awezi kuondoka mpaka awakilishe ripoti yake na viongozi kuanza kufanyia kazi mapendekezo yake, aliyo yatoa kwa viongozi.

Akizungumzia suala la Kapombe Maganga amesema kuwa taarifa hiyo wamekuwa wakizisoma kwenye magazeti, na kuzisikia katika vijiwe mbalimbali vya michezo.
 
[h=3]TCHETCHE STRAKER ALIYEKUWA NA MALENGO YA KUFUNGA MAGOLI 20[/h]
MAISHA ni malengo na ndicho kinachomtofautisha binadamu mmoja na mwingine. Na ndiyo tofauti ya straika wa Azam, Herman Kipre Tchetche raia wa Ivory Coast na wachezaji wengine wazalendo wanaocheza nafasi kama yake.


Ni straika mwenye akili anayejua nini kimempandisha ndege kwa muda wa saa nane kutoka mjini Abidjan, Ivory Coast mpaka jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Alipoanza msimu malengo yake ilikuwa ni kufunga mabao 20 na amemaliza na mabao 17. Anasikitika kwa hilo lakini bado ndiye mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Amewaacha mbali wanaomfuata kama Mrundi Didier Kavumbagu wa Yanga mwenye mabao 10, Paul Nongwa wa JKT Oljoro ana mabao nane sawa na Amri Kiemba wa Simba, Jerry Tegete wa Yanga na Hussein Javu wa Mtibwa Sugar.

Kavumbagu ndiye alikuwa tishio mzunguko wa kwanza ambao alifunga mabao saba lakini mzunguko wa pili makali yake yakapungua na akafunga mabao matatu tu na kumpa mwanya Tchetche kuzidi kupaa kileleni.

Tchetche anakumbukwa na mashabiki wa soka alipokuja kwa mara ya kwanza jijini Dar es Salaam na timu yake ya taifa ya Ivory Coast kushiriki mashindano ya Cecafa.

Urefu wake ni wastani, lakini jamaa ana umbo lenye misuli mikubwa na amejazia vilivyo sehemu ya kifua, mikono, mapaja na vijumbulu hali inayomfanya kuwa tishio kwa mabeki wapinzani.

Ana sifa ya kupiga mashuti makali na aina ya mabao yake ni kupitia pembeni kwenye engo, kati na mbali.
Alipofanya mahojiano na Mwanaspoti, Tchetche anasema: "Namshukuru Mungu kwa kunifanya kuwa mfungaji bora, hii isingewezekana bila mchango wa wachezaji wenzangu, makocha na mashabiki," alisema Tchetche alipewa ruhusa ya kuondoka kabla ya mechi ya Jumamosi iliyopita na kocha wake mkuu, Stewart Hall pamoja na nyota wengine wa kigeni wa klabu hiyo ambao ni pacha wake, Kipre Bolou, Wakenya; Jackins Atudo na Humphrey Mieno pamoja na Brien Umony wa Uganda.

"Shukrani kwa Mwenyezi Mungu pamoja na wachezaji wenzangu na benchi zima la ufundi kwa ushirikiano wao,"anasema Tchetche, ambaye ni shabiki wa Manchester United.

"Nimeshindwa kitu kimoja tu, kufikisha malengo niliyokusudia. Nilitaka kumaliza ligi na mabao 20 lakini sikukamilisha nimeishia hayo 17, nachukulia hali hiyo kama changamoto yangu kwa ajili ya msimu ujao kuona nafanya vizuri zaidi,"anaeleza Tchetche.

"Na nafikiri nimeshindwa kufikia malengo yangu kwa sababu ya majeruhi. Nilikuwa sina wakati mzuri mzunguko wa kwanza kwa sababu ya kuandamwa na majeruhi nikawa nacheza mechi mara kwa mara


"Mzunguko huu wa pili ndiyo nimekuwa vizuri na kufunga mabao yote hayo, nashukuru sana,"anafafanua Tchetche ambaye wachezaji wenzake wamempa jina la Van Persie wakimfananisha na Mholanzi anayekipiga klabu ya Manchester United, Robin Van Persie.
Kocha anavyomzungumzia

Kocha wake, Hall anasema: "Tchetche ni mchezaji mzuri ana kipaji na nguvu za mpira kiujumla ni msaada katika timu. Anacheza kitimu na kwa ushirikiano dhidi ya wenzake na anafuata maelekezo unayompa,' anafafanua Hall.

"Matatizo ya Tchetche ni kama ya washambuliaji wengine. Kuna sehemu ambazo ni rahisi kufunga huwa anakosa na nyingine ni ngumu kufunga yeye anafunga na kwangu nachukulia ni kawaida tu,"anasema Hall.


Nje ya soka

Tchetche ambaye alifika nchini akiwa anazungumza lugha moja tu ya Kifaransa, lakini sasa anaongea kwa kujitahidi Kiingereza na Kiswahili.

Anasema, anafurahia maisha ya Tanzania kwa sababu ameshakuwa mzoefu na mazingira:" Awali ilikuwa ngumu kwa sababu ya ugeni lakini sasa nimezoea."

Tchetche amekuwa mpenzi wa chapati na mchuzi, ugali na kuku na anasema anakifurahia aina hiyo ya msosi.
Awali akiwa Ivory Coast alizoea chakula chao cha asili cha Aloco. Aloco ni ndizi zinazokaushwa wao wanakula na samaki.

Historia

Katika familia ya Tchetche wamezaliwa sita. Watatu kati yao ni wanaume na watatu ni wanawake.
Yeye ni uzao wa pili ambao wamezaliwa wawili pamoja na pacha wake, Michael Kipre Bolou. Kaka yao ni Oscar Kipre Patrick na ndugu zake wakike ni Kipre Larine, Kipre Josiane na Kipre Andrea.

Anatoka katika kabila la Bete na amezaliwa na kukua katika kijiji cha Issia, Daloa, Ivory Coast.
Anasema ana mchumba, lakini amegoma kutaja jina lake na mtoto mmoja mwenye miaka mitatu, Kipre Astride.


HERMAN KIPRE TCHETCHE
Kuzaliwa: Desemba 16, 1987
Mahali: Issia, Daloa, Ivory Coast.
Klabu: JCA Treich-ville 1997-2011,
Azam FC 2011-
Taifa: Ivory Coast



SOURECE; MWANASPOTI
 
[h=1]Azam TV wafanya kufuru kubwa Simba na Yanga[/h]

KAMPUNI ya SSB inayomiliki klabu tajiri ya Azam FC ipo mbioni kumwaga zaidi ya sh. 1.5 bilioni kwa timu zote za Ligi Kuu Bara msimu ujao na itarusha laivu mechi zao kupitia televisheni yao.

Lakini habari za ndani zinadai Simba na Yanga zinagoma zikitaka kuongezewa fungu kwa madai kwamba televisheni ya kulipia itakayoanzishwa na Azam itanufaika zaidi.

Azam imekusudia kuchukua tenda ya kuonyesha mechi zote za Ligi Kuu Bara kupitia kituo chake kipya cha televisheni (Azam TV) ambacho kitaanza kazi hivi karibuni na ujenzi wa mitambo hiyo unaendelea katika jengo moja lililopo Barabara ya Mandela, jijini Dar es Salaam.

Habari za uhakika zinasema Azam itauza ving'amuzi na inakusudia kutoa kiasi cha Sh. 100 milioni kwa kila timu kwa timu zote 14 zitakazoshiriki ligi msimu ujao.

Jumatano wiki hii Kamati ya Ligi chini ya Wallace Karia na viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) walikutana na klabu za Ligi Kuu kujadili mkataba huo ambao utazipunguzia mzigo klabu ndogo ambazo zimekuwa zikisumbuliwa na ukata kutokana na kutegemea udhamini wa Vodacom pekee.

Karia alisema: "Tulikuwa na kikao na kuna televisheni moja ambayo tunataka kuingia nayo mkataba."

Habari za ndani zinasema Azam TV wataingia mkataba wa miaka mitano kuanzia Agosti na itakuwa ikirusha pia ligi za nchi nyingine za Afrika kama inavyofanya Supersport ya Afrika Kusini.

Hata hivyo, uliibuka mzozo baada ya Simba na Yanga kutaka kupewa mgao mkubwa tofauti na klabu nyingine. Lakini hatma itajulikana wiki ijayo baada ya klabu hizo kukutana tena kujadili mkataba huo, ule wa Supersport pamoja na Vodacom.

Mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage alisema; "Hata Manchester United udhamini wake wa Ligi haulingani na Wigan wala Sunderland, wa Man United upo juu kwa vile ni klabu kubwa, sasa iweje sisi tupate sawa na timu nyingine?

"Pili tunataka kuja na mkakati wa kuhakikisha msimu ujao mechi ambazo tutaenda kuzichezea mikoani tunawaachia mapato yote na wao wakija Dar es Salaam mapato ya huku hayawahusu, na huu ni utaratibu wa kawaida tu unaofanyika hata kwenye nchi nyingine, haiwezekani tunatumia shilingi bilioni 2.3 msimu mzima halafu mapato tunayopata ni kiduchu,"alisisitiza Rage.
 
WATATU KUPANDISHWA AKIWEMO MUDATHIR





Na Mahmoud Zubeiry




WAKATI Simba na Yanga SC zinakwenda mbio kusajili wachezaji wapya, washindi wa pili mara mbili mfululizo katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Azam FC wao wamesema hawasajili hata mchezaji mmoja, zaidi watapandisha wachezaji kutoka katika akademi yao.

Katibu wa Azam FC, Nassor Idrisa ameiambia BIN ZUIBEIRY leo asubuhi kwamba, kocha Muingereza Stewart Hall amesema kwa sasa hakuna umuhimu wa kusajili, zaidi ya kuiangalia timu kwanza katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, unaotarajiwa kuanza Agosti.

Nassor amesema kwamba kocha amewaambia iwapo atagundua kuna mapungufu katika timu katika kipindi cha kuanzia Agosti, ndipo atasajili Novemba katika dirisha dogo.

"Unajua mwakani ndio tutakuwa na haya mashindano ya Afrika (Kombe la Shirikisho). Na pia ndio mbio za ubingwa wa Ligi Kuu (Bara) zinapamba moto. Kwa hiyo mwalimu ameomba hicho ndicho kipindi kizuri kusajili,"alisema.

Hata hivyo, Nassor alisema kwamba kocha amependekeza wachezaji kadhaa wasajiliwe kutoka katika akademi ya klabu hiyo, wakiwemo Mudathir Yahya ambaye yupo na timu ya taifa Ethiopia, kipa Hamad Kadebi na Dissmas ambaye kwa sasa yuko kwenye majaribio Ujerumani.

"Tuna vijana wengi wazuri katika akademi yetu, mwalimu anawapa nafasi sasa. Anaamini timu yake ipo vizuri na hana haja ya kuhangaika kutafuta wachezaji wapya,"alisema Nassor.

Mudathir pia alikuwa kwenye majaribio nchini Ujerumani, akarudishwa nchini kujiunga na timu ya taifa, Taifa Stars kujiandaa kwa mchezo wa kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Ethiopia.


SOURCE; BIN ZUBEIRY
 
[h=5]Azam FC haiachi walio na mikataba na haiongezi mchezaji mpya

Kama ilivyokuwa wakati wa dirisha kubwa la usajili 2012/13 ambapo Azam FC ilimuongeza George Odhiambo Blackberry pekee, safari hii tena Azam FC imeamua kwapandisha wachezaji wawili wa Under 20, Mudathir Yahaya na golikipa Hamadi Juma Yahya Kadedi na kufunga zoezi la usajili.

Kwa mujibu wa ripoti toka kwa Kocha mkuu wa Azam FC mtaalam Stewart Hall, hakuna sababu ya klabu kwenda nje kusajili wachezaji ambao viwango vyao havipishani na waliopo klabuni.

Mchezaji Abdulhalim Humoud amepata timu nchini Afrika ya Kusini, Abdi Kassim Sadala Babi mkataba wake umekwisha kama ilivyo kwa Deogratius Munishi Dida huku Uhuru Selemani akirejeshwa Simba SC baada ya kumaliza msimu wa mkopo na Azam FC.

Wachezaji wengine wote waliosalia wanabaki klabuni na kocha mkuu amependekeza baadhi ya makinda wa Under 20 walioonesha viwango vya juu wapandishwe timu kubwa, wapewe mikataba na kisha wapelekwe kwa mkopo ili wakapate nafasi ya kucheza. Wachezaji hao ni Omary Mtaki na Kevin Friday.

Azam FC ambayo imemaliza ligi ikishika nafasi ya pili kwa msimu wa pili mfululizo itaanza kambi ya kujiandaa na msimu mpya hapo June 24 kwa mujibu wa ratiba ya mwalimu na baada ya kumaliza kipindi cha pre season, kikosi cha Azam FC kitasafiri nje ya nchi kucheza mechi za majaribio kama ilivyo kawaida yake.

Wachezaji wanaounda kikosi cha Azam FC ni

Magolikipa; Mwadili Ally, Aishi Salum na Hamad Juma Yahya

Mabeki; Himid Mao, Erasto Nyoni, Waziri Salum, Samih Nuhu, Luckson Kakolaki, Aggrey Morris, Said Moradi, David Mwantika na Jockins Atudo

Viungo; Kipre Bolou, Salum Abubakar, Jabir Aziz, Ibrahim Mwaipopo, Humphrey Mieno na Mudathir Yahya

Washabuliaji; John Bocco, Gaudence Mwaikimba, Khamis Mcha, Kipre Tchetche, Brian Umony na Abdallah Seif Karihe[/h]
credit: azam fc facebook page
 
***Makala na Edo Kumwembe***

Ukubwa usiishie kwenye Haki za Televisheni

MAJUZI ilisikika tena kwamba kuna kituo cha televisheni cha AZ TV kinataka kununua mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara. Nasikia Azam wana mpango wa kutoa shilingi 100 milioni kwa kila timu kwa ajili ya kuonyesha moja kwa moja mechi za Ligi Kuu. Simba na Yanga zinagomea mpango huo na kutaka zilipwe fedha zaidi kutokana na dili hilo.

Hii ni kwa mujibu wa hisia kwamba barani Ulaya timu kubwa huwa zinalipwa zaidi. Ina maana kwamba Simba na Yanga ndio timu kubwa zetu na zinataka zilipwe zaidi. Hispania, Real Madrid na Barcelona zinalipwa zaidi kuliko timu nyingine. England, timu ambayo mechi zake zinaonyeshwa mara nyingi zaidi huwa zinalipwa zaidi. Mara nyingi, Manchester United inajikuta ikilipwa zaidi.

Unapokuja mpango kama huu, Simba na Yanga huwa zinajiamini kuwa wao ni timu kubwa. Viongozi wake hutoa povu mdomoni kusema kwamba wao ni timu kubwa na walipwe zaidi. Inawezekana si jambo baya. Lakini nataka nionyeshwe ukubwa wao katika mambo mengine.

Nataka nionyeshwe ukubwa wao katika viwanja vya mazoezi. Nataka nionyeshwe ukubwa wao katika kufanya biashara zao binafsi. Majuzi nilikuwa natazama mazoezi ya Simba katika Uwanja wa Kinesi. Asilimia 90 ya uwanja waliokuwa wanafanyia mazoezi hauna nyasi. Kwanza uwanja si wao, pili ni mbovu. Ni kama ilivyo kwa ndugu zao wa upande wa pili. Mara nyingi mazoezi wanafanyia uwanja wa Shule ya Msingi Loyola. Ukiangalia viwanja walivyokuwa wanafanyia mazoezi Uturuki na kisha ukiangalia uwanja wa Loyola inakuwa sawa na mtu aliyekuwa anakula halafu ghafla akawekewa kinyesi.

Kuna viongozi katika timu hizi. Kumbe wanajua kwamba wanaongoza timu kubwa pindi linapokuja suala la haki za televisheni. Lakini linapokuja suala la kuwaza kwa mapana katika masuala mengine ya ukubwa wa klabu inakuwa kichekesho. Ukubwa wa Simba umebakia katika mabasi, majengo na idadi ya mashabiki. Huduma za mazoezi na mengineyo, inakuwa vigumu kuitofautisha na Coastal Union, Mtibwa Sugar (ambayo ina uwanja wake), Kagera Sugar na nyinginezo.

Katika soka, mwaka wa soka umeisha Mei. Sasa hivi tunakwenda Agosti na Ligi itaaanza. Maisha yatakuwa yale yale, watu wale wale, mashabiki wale wale, viongozi wale wale na hisia zile zile. Ahadi za ujenzi wa uwanja wa Simba Goba zitaendelea. Ujenzi wa mauzo ya jezi za Yanga zitakuja. Lakini mpaka sasa mashabiki wa Yanga wanavaa jezi za Afrika Kusini kwa sababu ni za njano na kijani, wale wa Simba wanavaa jezi za Arsenal, Manchester na Liverpool. Ili mradi iwe nyekundu.

Kabla sijawatetea Simba na Yanga katika kupata mapato zaidi ya Coastal, Azam, JKT Ruvu, Kagera Sugar na wengineo, nadhani ni wakati mwafaka wa kubadilika na kuonyesha ukubwa nje na ndani ya uwanja.

Vinginevyo timu kubwa itaendelea kuwa Azam huku Simba na Yanga zikibaki kuwa timu kongwe. Ni tofauti ambayo unaweza kuiona kwa macho na si kusikiliza kelele za mashabiki. Mchezaji mmoja anasajiliwa kwa shilingi 50 milioni, sawa na nusu ya bei ya kiwanja kikubwa kando ya jiji la Dar es Salaam. Lakini mpaka sasa hakuna viwanja vya kisasa.

credit: Mwanasppoti
 
Ndetichia, habari hizi ndo tunapenda sera ya 'kusema na kutenda' ndiyo uongozi na wadhamini wa AZAM FC walivyo , tofauti kabisa na klabu 'kubwa' na 'kongwe' ambao kusema ni kwingi lakini vitendo vichache mfano Young Africans na Simba kuwa na viwanja vyao vya soka wamesema sana lakini mpaka leo hii hakuna kitu. Ngoja AZAM FC na wadhamini wake waendelee kuleta mapinduzi katika tasnia ya michezo hususan uendeshaji na udhamini ndani ya vilabu vya soka nchini Tanzania.
 
TANZIA
Himid Mao Mkami amepata msiba wa baba yake mkubwa Mr Juma Mkami, Azam FC inaungana na Himid Mao wakati huu wa msima na majonzi kwake... tunamuombea kwa mwenyezi mungu ampe ujasiri wa kustaahimili mitihani hii ya maisha. Mwenyezi Mungu alilaze roho ya marehemu Juma Mkami mahali pema peponi Amin

 

Mkuu kiuhalisia Edo yupo sahihi Simba na Yanga ni timu kongwe na si timu kubwa haaingii timu inajiita timu kubwa halafu hata uwanja tu wa Mazoezi hawana halafu eti wanajifananisha na Man Utd huu ni upuuzi, inatakiwa waendeshe timu zao Kisasa kama ambavyo Azam wamefanya ndo waanze kujiita timu kubwa. Kiuhalisia SIMBA na YANGA zinachingia kwa kiasi kikubwa kuporomosha soka letu.
 

thanks mkuu kwa kuliona hilo..
 
Tuzo za Sputanza mwaka huu 2012/13

Abubakar Salum Sure Boy kawa mchezaji chipukizi..

Hongera zako..
 
bakharesa kanunua timu ya bandari..

Baada ya mafahari wa biashara ya usafirishaji katika bahari ya Hindi wakiwa wamejiimarasha katika kuunganisha visiwa vya Pemba, Unguja na jiji la Dar es salaam, Said Salim Bakharesa kukamilisha ukarabati wa bandari ya Zanzibar sasa wamenunua timu ya Banari FC. Kampuni hiyo inayomiliki timu ya Azam FC inayoshiriki ligi kuu ya Tanzania Bara, wameamua kujikita pia katika soka la Zanzibar ambalo limetoa wachezaji wengi katika timu ya Azam FC. Kwa mujibu wa taarifa iliyotufukia mtandao huu na kudhibitishwa na watu wa karibu, zinasema kuwa Kampuni hiyo ya Said Salim Bakharesa wamenunua timu hiyo ya Bandari ambayo teyari ilikuwa imeshauza nafasi yake ya ushiriki wa ligi kuu ya Zanzibar kwa kuwauzia Malindi, na hivyo Azam mpya kuanzia katika daraja la kwanza. "Azam wamenunua timu ya Bandari na Malindi wameuziwa nafasi ya Bandari, kwa hiyo nafasi ya Bandari kucheza ligi Kuu itachukuliwa na Malindi ambao walikuwa wameteremka daraja, na Azam wataanzia daraja la Malindi, hivyo Azam wameuziwa timu ambayo tayari imeuza daraja." ili eleza moja ya chanzo chetu.

sosi: azam fans blog
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…