The Official Azam FC Thread

Rolling Stone Cup

azam academy 3 - 0 Eagle rangers ya tanga
 
[h=3]SURE NA KIPRE WAONGEZA MKATABA[/h]
Na Mahmoud Zubeiry


WASHINDI wa Medali za Fedha katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara mara mbili mfululizo, Azam FC wamewaongezea mikataba nyota wao watatu, viungo Salum Abubakar ‘Sure Boy Jr.', Kipre Michael Balou na mshambuliaji Kipre Herman Tchetche.

Mtoto wa kiungo wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Abubakar Salum ‘Sure Boy' aliyewika Yanga SC miaka ya 1980, Sure Boy Jr. ameongeza Mkataba wa miaka miwili na sasa atakuwa mali ya Azam hadi mwaka 2016.
[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Pacha wapendao; Kipre Tchetche kushoto akiwa ameshika tuzo yake ya ufungaji bora Ligi Kuu pamoja na mdogo wake, Kipre Balou. Wameongeza mikataba Azam FC.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Pacha kutoka Ivory Coast, Kipre Balou na Kipre Tchetche waliopishana msimu mmoja kuingia Azam nao wameongeza miaka miwili kila mmoja. Balou atakuwa mali ya timu ya Bilionea Alhaj Said Salim Awadh Bakhresa hadi mwaka 2016, wakati Kipre hadi 2015.

Katibu Mkuu wa Azam FC, Nassor Idrisa Mohamed ‘Father' ameiambia BIN ZUBEIRY mchana huu kwamba, uongozi wa klabu kwa kuzingatia ubora wa wachezaji hao, umeamua kuwaongezea Mikataba.

"Wazi tuna muda mrefu zaidi wa kuendelea kuhitaji huduma ya wachezaji bora kama hawa. Unapozungumzia watu kama Sure Boy, Kipre Tchetche na Kipre Balou, hawa ni wachezaji wakubwa sana katika Ligi ya Tanzania. Huwezi kuthubutu kuwa nao kwa Mkataba wa muda mfupi. Hizi ni bidhaa adimu,"alisema.
[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD="align: center"] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Fundi wa mpira; Salum Abubakar 'Sure Boy Jr.' ameongeza Mkataba Azam FC[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


Sure Boy ni kati ya wachezaji wanne tu waliobaki kati ya waliopandisha Azam Ligi Kuu mwaka 2008, wengine wakiwa ni John Raphael Bocco ‘Adebayor', Luckson Kakolaki na Malika Philip Ndeule.

Alijiunga na Azam FC mwaka 2006 ikiwa Daraja la Kwanza akitokea timu ya mtaani, Friends Rangers ya Manzese na sasa ni kati ya wachezaji tegemeo wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Azam FC imekuwa ikipokea ofa kadhaa kutoka klabu mbalimbali barani, ikiwemo El Hilal ya Sudan kutaka kumnunua Sure Boy, lakini imekuwa ikikataa kwa matumaini ya kumuuza Ulaya baadaye.

Tchetche alitangulia kujiunga na Azam mwaka 2010 kabla ya msimu uliofuata kufuatiwa na pacha wake, Balou na wote klabu ilivutiwa nao walipokuja na timu ya taifa ya vijana ya Ivory Coast kucheza Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge mwaka 2010 Dar es Salaam kama waalikwa wa kunogesha mashindano.

Tchetche aliibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu msimu uliopita kwa mabao yake 16 na mdogo wake, Balou kwa pamoja na Sure waliifanya Azam iwe na safu imara mno ya kiungo hadi kuukosa kosa kidogo tu ubingwa wa Ligi Kuu, ikizidiwa kete na Yanga SC.
[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: center"]Bado wapo sana Chamazi; Kipre Tchetche kushoto na Balou kulia wataendelea kufanya kazi Chamazi[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


Katika hatua nyingine, Nassor amesema Azam FC ambayo kwa takriban wiki nzima sasa imekwishaanza maandalizi ya msimu mpya, Jumanne itacheza mchezo wa kirafiki na kombaini ya timu za Majeshi ya Kujenga Taifa (JKT) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika sherehe za miaka 50 ya jeshi hilo.

Muungano wa wachezaji kutoka JKT Oljoro, JKT Mgambo, Ruvu Shooting na JKT Ruvu zote za Ligi Kuu dhidi ya washindi wa pili wa Ligi Kuu, Azam FC hakika itakuwa mechi tamu Jumanne.


source: BIN ZUBEIRY
 
Mchezaji wa zamani wa Afrika ya kusini na manchester united ya uingereza azuru chamazi complex ambaye anaitwa Fortune


 

Azam Academy leo asubuhi imeingia nusu fainali ya Kombe la Rolling Stone 2013 baada ya kuifunga timu ya Rolling Stone 2-0, magoli ya Azam Academy yakiwekwa wavuni na Baraka Mange na Kelvin Friday
Pongezi kwa wachezaji wote!
Mechi ya nusu fainali itachezwa kesho asubuhi kati ya Azam Academy na Coastal Union B.
 
Kutokana na maombi ya wadau wengi wa soka Tanzania kutaka kuona mazingira yote ya (miundo-mbinu )Chamazi sports complex ili kuona maendeleo makubwa ya uwekezaji katika michezo ndani ya timu ya Azam Fc ambao ni ndoto kwa washabiki wa timu 'kongwe' za soka Tanzania tuendelee kutizama clip hii maalum kila kona ya Azam Fc Chamazi Complex kwa hisani ya Azamfctv ya youtube: AZAM FC TV EPS 36 Azamfctv
 
Last edited by a moderator:
#Matokeo
Azam FC Leo imeifunga Ashanti United 5-1 katika Mechi ya kirafiki. Seif RASHID Karihe 2, Kipre tchetche, jabir na Umony wakifunga moja kila mmoja Wadogo zao Azam Academy wameshindwa kutwaa rolling cup baada ya kupoteza kwa penati 5-4 kufuatia sare ya 0-0
 
#Matokeo
Azam FC Leo imeifunga Ashanti United 5-1 katika Mechi ya kirafiki. Seif RASHID Karihe 2, Kipre tchetche, jabir na Umony wakifunga moja kila mmoja Wadogo zao Azam Academy wameshindwa kutwaa rolling cup baada ya kupoteza kwa penati 5-4 kufuatia sare ya 0-0
 
Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA JULAI 18, 2013 SAA 3:19 USIKU
KAMPUNI ya mpya ya Habari nchini, Azam Media Group, leo imeingia Mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya Sh. Milioni 331 na klabu ya Simba ya Dar es Salaam kwa ajili ya kurusha kipindi maalum cha klabu hiyo, kitakachojulikana kama Simba TV kupitia kituo kipya cha Televisheni, Azam TV.
Mwenyekiti wa Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage, kwa pamoja na Katibu, Evodius Mtawala na Mjumbe wa Baraza la Wadhamini, Hamisi Kilomoni waliiwakilisha klabu hiyo katika utiaji saini wa Mkataba huo mnono kwenye ukumbi wa Kibo, jengo la PSPF, Dar es Salaam.[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: left"]Utajiri huu; Mwenyekiti wa Simba, Alhaj Ismail Aden Rage (kushoto) akipeana mikono na Mkueugenzi wa Azam Media, Abubakar Bakhresa kulia baada ya kuingia Mkataba huo. Katikati ni Mwanasheria wa Azam Media, Shani Chrstoms.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Upande wa Azam uliwakilishwa na Mkurugenzi Mkuu, Abubakar Bakhresa, Meneja Mkuu, Said Mohamed na Mwanasheria, Shani Christoms ambao waliikabidhi Simba SC hundi za fedha hizo kwenye hafla hiyo.
Meneja wa Azam Media, Mzee Said alisema kwamba Mkataba huo ni mwanzo tu, lakini kampuni hiyo imejipanga kusaidia zaidi soka ya Tanzania kwa kuingia mikataba mingi yenye manufaa kwa mchezo huo nchini.[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: left"]Mkataba mnono wallahi; Rage akiusoma Mkataba huku akifurahi pembeni ya Abubakar Bakhresa
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Mzee Said alisema Azam Media inaleta mapinduzi na ukombozi katika medani ya michezo Tanzania na kwamba Watanzania wakae tayari kushuhudia mambo makubwa muda si mrefu kupitia Azam TV.
[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: left"]Wanamwaga wino;Shani kulia akiwashuhudia Rage na Mzee Kilomoni wakisani Mkataba
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: left"]Inakuja hivi karibuni; Bango la Azam TV lenye ujumbe inakuja hivi karibuni
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Alhaj Rage, pamoja na kuwashukuru Azam Media kwa Mkataba huo mnono, alisema klabu inategemea kujikomboa zaidi kiuchumi kutokana na mikataba ya udhamini kama hiyo na muda si mrefu wataingia mikataba mingine itakayokuza zaidi pato la klabu.[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: left"]Hundi za Milioni 331; Kutoka kulia Abubakar Bakhresa, Mzee Said Mohamed, Shani na Rage akiwa ameshika hundi zake
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

"Nimesikia pia mnataka kununua haki za Televisheni za Ligi Kuu ya Tanzania Bara, mimi nasema karibuni na katika hilo, natoa angalizo, mkinunua haki za TV za Ligi Kuu, naomba mtoe fungu sawa kwa kila klabu, hakuna kubagua eti huyu apate kidogo, yule apate zaidi, hapana,".[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: left"]Mbele ya bango; Kutoka kulia Abubakar, Mzee Said, Shani, Rage, Mzee Kilomoni na Mtawala
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: left"]Fedha hizi tunasajili mshambuliaji mwingine; Rage akiteta na Katibu wake, Mtawala mbele ya Mzee Kilomoni
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: left"]Tunaleta mapinduzi na ukombozi katika soka ya Tanzania; Mzee Said akizungumza pembeni ya Abubakar Bakhresa
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

"Lazima mpira wa miguu katika nchi hii maendeleo yafike kila sehemu na tuondoe ubinafsi wa kujifikiria eti sisi Simba ndiyo tupate zaidi, hapana. Hiyo si haki, lazima na zile klabu ndogo pia nazo zinufaike sawa na sisi kwa kuwa tunacheza ligi moja,"alisema Rage ambaye pia ni Mbunge wa Tabora Mjini (CCM). Source: Bin Zubeiry wa Bongostaz.blogspot.co.uk
 
source: Azam Fans Club Kocha Stewart Hall akiongoza mazoezi kwa vitendo kwa vijana wake kuanzia kulia Mwaikimba, Ndeule, Wandwi, Atudo na Mwantika katika ufukwe wa pwani ya bahari ya Hindi jijini Dar-es-Salaam Julai, 2013.
 
Azam Media Group na Simba SC jana usiku kwenye ukumbi wa JB Belmont NSSF Golden Jubilee Tower waliingia mkataba wa miaka mitatu wa kuzalisha vipindi vya klabu ya Simba na kurushwa kwenye ving'amuzi vya Azam Media, Kwa sasa mazungumzo kati ya Azam Media na Yanga SC yanaendelea ili kufikia makubaliano. Huu ni ukombozi kwa soka la bongo
 
[h=3]AZAM FC WAPAA JUMAMOSI KWENDA AFRIKA KUSINI KUWEKA KAMBI YA KUJIANDAA NA MSIMU[/h]
Na Mahmoud Zubeiry, IMEWEKWA JULAI 30, 2013 SAA 2:44 ASUBUHI
AZAM FC inatarajiwa kuondoka nchini mchana wa Jumamosi kwa ndege ya Shirika la Afrika Kusini, kwenda Johanesburg, Afrika Kusini kuweka kambi ya wiki mbili kujiandaa na msimu mpya.
Timu hiyo yenye maskani yake, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, itaondoka na kikosi chake kizima kasoro wachezaji wawili tu majeruhi, kiungo Mkenya, Humphrey Mieno na mshambuliaji Mganda, Brian Umony.
Meneja wa Azam FC, Jemadari Said ameiambia BIN ZUBEIRY asubuhi ya leo kwamba, timu inaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wake wa Azam Complex, Chamazi kwa ajili ya safari hiyo, wakati majeruhi Umony na Mieno wanafanya mazoezi ya gym.[TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD="align: center"] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: left"]Azam wakijifua ufukweni[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Mshambuliaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Kariakoo United ya Lindi, amesema kwamba timu ikiwa Afrika Kusini pamoja na kuweka kambi ya mazoezi, pia itacheza mechi nne za kujipima nguvu dhidi ya timu kubwa za huko.
Ingawa bado ratiba ya mechi za Azam nchini humo haijajulikana, lakini inafahamika miongoni mwa timu zitakazocheza na Azam ni Orlando Pirates, Supersport United, Kaizer Chiefs na Mamelodi Sundowns.
Kuna uwezekano Azam ikacheza mechi zaidi kulingana na namna ambavyo timu zaidi nchini humo zitavuwiwa kucheza nayo.
Azam inatarajiwa kurejea nchini siku moja kabla ya kucheza mechi ya kuwania Ngao ya Jamii kuashiria kufungua pazia la msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Yanga SC, Agosti 17, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Safari hii Azam, washindi wa pili mara mbili mfululizo wa Ligi Kuu wamepania kutwaa Ngao mbele ya Yanga, baada ya mwaka jana kufungwa na Simba SC na kocha Muingereza Stewart Hall anajiandaa kikamilifu kwa ajili hiyo.
 

Mwaka Insrael Nkongo mtahonga kiasi gani? Million kumi zile zile au zaidi? Mkong'oto wake pia utaongezeka!
 
Mwaka Insrael Nkongo mtahonga kiasi gani? Million kumi zile zile au zaidi? Mkong'oto wake pia utaongezeka!

hapa ni mpira tu haongi mtu na gemu iliyoisha ile ya moja bila mkampa hela refa sie poa tu ila mtakaa tu.. mnabana bongo afrika wanaachia..
 
Azam FC inasafiri jumamosi hii kuelekea afrika ya kusini kwa maandalizi ya ligi kuu na itacheza michezo minne kama ifuatavyo

Tarehe 5 August, Azam Fc vs Kaizer Chiefs, Tarehe 7 August Azam Fc vs Mamelodi Sundows, Tarehe 9 August Azam Fc vs Orlando Pirates, Tarehe 12 August Azam Fc vs Moroka Swalows
 
Leo Matokeo mechi ya Kirafiki

Keizer CHiefs 3 - 0 Azam fc

huu ni mchezo wake wa kwanza nchini Afrika kusini kati ya mechi tatu, timu imeanza kwa kupoteza mchezo wake wa kwanza..

Forza Azam FC
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…