The Official Azam FC Thread

Nchi imesimama, kila mtu anazungumzia mechi kati ya Azam FC na Yanga.... YANGA ni ileile, mabingwa wa kihistoria, timu ya wanachi, timu pendwa Tanzania.... Kilichoongezekahapa ni umaarufu na kiwango cha Azam FC..... Sasa mechi kati ya Azam FC na Yanga imekuwa El-Classico. Tukutana uwanja wa Taifa Kesho.... Kwa mlio mbali na jiji. Azam TV itawaletea mtanange huu live. Nunua kisimbuzi cha Azam TV usipitwe na uhondo huu

sosi:azamfc fb page
 
Tukiwa katika robo ya mwisho ya mechi za ligi kuu Tanzania, mechi ya leo ina nafasi kubwa ya kuamua bingwa. Azam FC ambayo hadi sasa haijapoteza mchezo hata mmoja tunajiamini kuwa tuna nafasi kubwa ya kushinda kutokana na maandalizi kabambe na viwango vya wachezaji wetu. Mashabiki wetu tunawaomba mjitokeze kwa wingi leo mkiwa vifua mbele kuishangilia timu yenu. Azam FC .... Tucheze pamoja kwa furaha
 

PICHANI Mkombozi; Kinda Kevin Friday kushoto akishangilia na Gadiel Michael baada ya kufungia bao la kusawazisha Azam leo Uwanja wa Taifa. Matokeo: Azam Fc 1 - Young Africans 1 : Source: KINDA WA B AINUSURU AZAM PUNGUFU KUZAMA KWA YANGA KAMILI - BIN ZUBEIRY

Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa askari wa jeshi la Polisi Tanzania, Hashim Abdallah wa Dar es Salaam aliyesaidiwa na Anold Bugado wa Singida na Florentina Zablon wa Dodoma, hadi mapumziko tayari Yanga walikuwa mbele kwa bao 1-0.

Bao hilo lilifungwa na mshambuliaji kutoka Burundi, Didier Kavumbangu dakika ya 14 aliyekutana na mpira uliorudi baada ya kupanguliwa na kipa Aishi Salum Manula kufuatia kutokea piga nikupige langoni mwa Azam.

Shambulizi lililozaa bao hilo lilianzia kwa kwa Simon Msuva aliyemtoka beki Gadiel Michael wingi ya kulia na kutia krosi iliyounganishwa na Kavumbangu lakini mpira ukagonga mwamba na kurudi uwanjani na kumkuta Hamisi Kiiza aliyepiga kipa akaokoa na kumkuta mfungaji aliyemaliza kazi.
Azam FC ilikosa mabao mawili ya wazi kipindi cha kwanza, wakati bao lililofungwa na Kipre Herman Tchetche refa Hashim alikataa kwa sababu mpigaji kabla ya kufumua shuti alimsukuma beki Kevin Yondan.

Pamoja na kubaki wachache, Azam waliendelea na jitihada za kusaka bao la kusawazisha na dakika ya 83 kinda aliyepandishwa kutoka kikosi cha pili, Kevin Friday aliipokea vyema pasi ya Salum Abubakr ‘Sure Boy’ na kumchambua kipa mkongwe Juma Kaseja.

Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Juma Kaseja, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Frank Domayo, Simon Msuva, Hassan Dilunga, Didier Kavumbangu/Mrisho Ngassa dk73, Hamisi Kiiza/Hussein Javu dk87 na Emmanuel Okwi.

Azam FC; Aishi Manula, Erasto Nyoni, Gadiel Michael, Said Mourad, Kipre Balou, Himid Mao, Salum Abubakar, John Bocco, Kipre Tchetche na Khamis Mcha/Kevin Friday dk49.

HABARI na PICHA kwa hisani kubwa ya : BIN ZUBEIRY KINDA WA B AINUSURU AZAM PUNGUFU KUZAMA KWA YANGA KAMILI - BIN ZUBEIRY
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…