Inataka nyote muwe mnaaminiana sana ili kuishi mbali mbali pamoja na kuwa wana ndoa. Kuna vishawishi vingi sana ambavyo vinaweza kabisa kusababisha kutembea nje ya ndoa. Wapo wana ndoa ambao wanaishi mabara tofauti na ndoa zao zinaendelea bila matatizo lakini bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi.
Wengi wamesema hapo juu kwamba yule mwenye kipato kidogo ndiye anayestahili kuhama, na mimi nawaunga mkono. Pia kuna umuhimu wa kuangalia wapi kuna more opportunities, low crime rate, quality of life, mtakuwa mnaonana mara ngapi kwa mwaka, je, gharama za kusafiri kwenu mtaweza kuzimudu bila matatizo?
Kuna unafuu kidogo kama hamna watoto lakini mkishajaliwa watoto maisha yanakuwa magumu. Kila la heri.