The role of Charisma, Principle, Royality, Oportunity, and Ego in Leadesrship

The role of Charisma, Principle, Royality, Oportunity, and Ego in Leadesrship

Kama kawaida tutaangalia majina na weledi wa kupiga domo na si matokeo chanya na imara ya uwakilishi, uwajibikaji na uongozi makini!
 
Nimeshindwa kupamabanua iwapo iwe thread ya kiingereza au kiswhaili kwa vile nililikoroga nilipotumia title ya kiingereza ilihali post ikiwa ni ya kiswahili. Nadhani ni kwa sababu sijui tafrisi ya ya neno charisma kwa kiswahili. Hata hivyo nitaendeleza mada kwa kiswahili.

Ninaanza kwa kukumbusha kuwa maendeleo ya nchi yoyote ile duniani huletwa na wananchi wenyewe, siyo viongozi wala wafadhidili. Kiongozi mzuri ni yule atakayewaonyesha wananchi mambo ya kufanya na kuwahamasisha kuyafanya mambo hayo kwa maendeleo yao.

Tanzania imekuwa na viongozi wa aina kadhaa:

(1) Viongozi wa "vibaba:" Wanawaaminisha wananchi kuwa watawatafutia wananchi vibaba kutoka kwa wafadhili ili walete maendeleo. Kaulimbiu ya viongozi hawa ni ile ya "nitapata wafadahili sana."
(2) Viongozi wa "miujiza:" Wanawaaminisha wananchi kuwa watafanya miujiza ili maendeleo yaje yenyewe. Hawa utawasikiwa wakitumia mameno kama vile kinachoitakiwa nia "maamuzi magumu" tu kuleta maendeleo.
(3) Viongozi wa "shauri yenu:" Wanawaaminisha wananchi kuwa maendeleo yapo tayari ila wananchi wenyewe ni wajinga hawajui kutumia nafasi za maendeleo wao wenyewe. Mfano mzuri wa viongozi hawa ni yule aliyesema "sijui kwa nini wananchi ni maskini ilihali kila kitu kipo."
(3) Viongozi wa "kuna mchawi:" Hawa wanafanana na wale wa miujiza ila wanatofauatiana kidogo. Wao wanawaaminisha wananchi kuwa maendeleo ya wanachi yanakwamishwa na "mchawi" fulani ambaye wao tu ndio wana uwezo wa kumfichua mchawi huyo. Hawa utawasikiwa wanatumia maneno kama vile "mafisadi ndio wanaotukwamisha."

Wapo wa aina nyingi kidogo lakini hao nadhani ndio tunaowajua zaidi. Viongozi halisi wanaotakiwa Tanzania ni wale watakaowaambia wananchi kuwa maendeleo ya nchi yanatokana na juhudi zetu wote, uongozi wa nchi ni dhamana tu, kuna sheria za nchi zinazotakiwa kufuatwa na raia wote ikiwa ni pamoja na viongozi, na kila kipato cha mtu kitatokana na kazi halali. Kwa bahati mbaya viongozi wa aina hiyo hawapo kabisa; kwa nini?

..........to continue!
 
Interesting.....ngoja nitulie nikisuburi muendelezo.
 
Mwalimu Kichuguu,

Nashukuru kutuwekea "mafungu" ya hawa viongozi... kuna moja labda umelisahau Viongozi Miungu- wao wanajua kila kitu na kama Mungu hujidai eti kila kitu kina free will na ipo siku wanaweza kugadhibika na kuleta ile iliyo ya kweli ikiwa hatuamini wanachokisema!
 
Nimeshindwa kupamabanua iwapo iwe thread ya kiingereza au kiswhaili kwa vile nililikoroga nilipotumia title ya kiingereza ilihali post ikiwa ni ya kiswahili. Nadhani ni kwa sababu sijui tafrisi ya ya neno charisma kwa kiswahili. Hata hivyo nitaendeleza mada kwa kiswahili.

Ninaanza kwa kukumbusha kuwa maendeleo ya nchi yoyote ile duniani huletwa na wananchi wenyewe, siyo viongozi wala wafadhidili. Kiongozi mzuri ni yule atakayewaonyesha wananchi mambo ya kufanya na kuwahamasisha kuyafanya mambo hayo kwa maendeleo yao.

Tanzania imekuwa na viongozi wa aina kadhaa: ...........................................

..........to continue!

Asante kwa kuuleta huu uzi na kwa kufungua dimba kwa kutaja aina ya viongozi hapa Tanzania.

Nadhani ni vema huu uzi ubaki katika lugha ya Kiswahili kwa sababu mara nyingi nimeona watu wenye fikra nzuri sana wameshindwa kuchangia mada zinazotumia lugha ya Malkia.

Kabla sijaanza kuchangia ngoja tu niweke hapa chini tafsiri zangu za maneno ya Kiingereza uliyotumia kwenye kichwa cha mada. Naomba mwenye sahihisho au nyongeza asisite kuchangia.

Sijui kama ulimaanisha Royalty au Loyalty kwa hiyo nitatoa tafsiri ya maneno yote mawili.

Charisma = Haiba kubwa, Mvuto, Ngekewa
Principle = Kanuni, Maadili, Msimamo
Royalty = Ufalme, Umwinyi
Loyalty = Uaminifu, Uwajibikaji
Opportunity = Nafasi, Fursa, Wasaa
Ego = Ubinafsi, Ujivuni, Umimi

Nitarudi baadae kuendeleza mjadala.

cc. @Rev. Kishoka @Mwelewa
 
Back
Top Bottom