The Saturday Night Massacre!

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
16,419
Reaction score
26,594
Of late, mambo hayaendi vizuri sana kwa Mh Rais John P. J. Magufuli na Baraza lake la Mawaziri.

Kuna mengi mazuri mh. Magufuli anafanya vizuri, lakini yafuatayo ni shiida sana na imebidi watu wachinjiliwe mbali.

* Biashara haziendi vizuri na siyo siri kodi inaendelea kupungua.
Wafanyabiashara wanaofunga biashara zao kihalali kutokana na kodi zisizoeleweka sasa wanaongezeka.

* Kuanzisha viwanda nchi hii ni kama dhambi. Mamlaka lukuki zitakuandama, iwe NEMC, OSHA, FIRE , JIJI na kodi zake, TRA, NSSF, WCF TBS na utitiri wa Mamlaka zenye kutaka kukutoa upepo.

*Wizara ya Kilimo , na hata Maji. Huko usiseme. Kinachofanyika hakieleweki na matokeo chanya hakuna.
Kwenye Kilimo suala la Korosho limeiumbua vibaya serikali. Na sidhani kama wananchi hasa wazalishaji korosho wataisamehe serikali kirahisi.

Nani mwenye makosa si rahisi kusema lakini seriksli imekuwa ikikaidi ushauri wa Bunge mara kwa mara.
Watu imebidi wawajibishwe, ingawaje ukweli uko wazi.
Wa kubeba lawama ni washauri wa karibu na rais, Mawaziri.

The Saturday Night Massacre imewakumba hasa mawaziri wenye dhamana ya Bishara na Viwanda, Mzee wa Kupiga Sound, Ndg Mwijage m na Waziri wa Kilimo ndg Tizeba.

Ushauri wangu.

Waziri usipoweza kupata na kuzingatia ushauribwa wananchi, kupitia Bunge lenye uwakilishi wa wananchi hao, heri kujiuzulu kuliko fadheha ya kufukuzwa madarakani.
 
Sasa nimeelewa kwanini wadau wamechinjia mbali huu uzi[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]dah jf viburi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…