Tunaweza kufanya hivyo bila kujali mitaji yetu midogo tuliyo nayo. Kwa mfano, huyu x anamiliki shamba la miwa pale Korogwe, mwenzetu ameanza lini,kwa mtaji kiasi gani na amewezaje kulifikia soko. Vikwazo gani anapata/alipata na nini plan zake za siku za usoni.
Kipo kijarida kimoja nilisoma, dada mmoja wilayani Hai amefanikiwa kuwa na shamba la kuku zuri kutokana na zawadi ya kuku mtetea aliyopewa na bibi yake. Huyu ni mfano mzuri, kwa sababu mtaji wake unajulikana ulikotoka,alivyouendeleza na kuupanua hadi kufikia kiwango hicho, na maelezo yako wazi ya jinsi alivyopita hadi alipo. Je watu wetu tunaowasifia kama wajasiriamali wako hivyo?