The Tourist: Let's go to Bahamas, a way forwad to USA

Mla Bata

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2013
Posts
7,841
Reaction score
17,491
"This heart of mine was made to travel this world"

"Travel is my therapy"
"To travel is to live"

Wasalam,

Kama title ya uzi huu inavyoeleza, lengo la uzi huu ni kutoa dondoo kadhaa kwa wadau wenzangu wa kujilipua nje ya hii continent so called "shithole" (D.Trump, Jan 10, 2018) [emoji36], and this time specific to this "Caribbean Paradise" Bahamas.

Tuifahamu Bahamas.

Bahamas (mjumuisho wa visiwa) ni nchi namba nane kwa ukubwa kati ya visiwa (nchi) 26 vinavyopatikana kwenye bahari ya caribbean. Bahamas ina ukubwa wa kilometa mraba 13,878 na population ya watu wapatao 385,637 hii ni matokeo ya sensa iliyofanyika mwaka 2018.

Watu wa bahamas wanatambulika kama Bahamians, wakiwa ni asili ya mchanganyiko wa waafrika, wamarekani na waingereza, ndio kupatikana kizazi hiki cha sasaa, Lugha rasmi inayozungumzwa na Bahamians ni kiingereza na Asilimiaa zaidi ya tisini (90%+) ni watu wenye asili ya ngozi rangi nyeusi, kwahiyo ewe mzamiaji mwenzangu ondoa shaka katika swala la ubaguzi wa rangi.

Kijiografia nchi ya Bahamas imepakana na visiwa vya cuba, Haiti, Dominican Republic na kwa upande wa kusini-mashariki imepakana karibu kabisa na Jimbo la Florida marekani (nitaeleza kiundani zaidi hapa mbele).

Kwa upande wa Uchumi Bahamas ndio nchi namba moja inayoongoza kwa utajiri katika visiwa 26 vya Caribbbean ikiwa kwa asilimia kubwa ikitegemea Utalii kama chanzo cha kuingizia mapato ya nchi, Pesa inayotumika ni Bahamian dollar ikiwa sawa na Dollar moja ya kimarekani (1 B.Dollar=1 Us dollar = 2300 Tsh ). Mji mkuu wa Bahamas ni Nassau ambapo robo tatu ya raia wote wa Bahamas wanapatikana katika mji wa Nassau.

Twende sasa kwenye lengo la uzi wetu.

Kwa wale wadau wenzangu ambao either wana ndoto za kwenda kuishi US au nchi zenye mfanano wa kiuchumi/Maisha na US hii ni njia rahisi zaidi kutimiza malengo yako kupitia safari ya bahamas.

Kwanini Bahamas?

1. Visa Free country

Nchi ya Bahamas haihitaji Visa katika kuingia nchini humo kwa raia wa tanzania kama utakwenda kama mtalii ambapo utatakiwa kukaa kwa maximum siku 90, ( three months) ambapo kama kweli wewe ni fighter na unajua kutumia fursa hapa ndani ya siku 90 huwezi kukosa kazi ya kuzugia ambapo utapata work permit itakayokupa nafasi ya kuendelea kutafuta kazi nyingine ya maana (N:B its not guaranteed ).

kama nilivyosema awali Bahamas wanategemea sanaa uchumi wao kwenye Swala la tourism ambapo utalii wao umebase kwenye bahari so hapa beach boys ni fursa kwenu, kazi nyingine kama hoteliers etc unaweza kwenda kutupa ndoano yako ambapo kama bahati yako itakuwa vizuri basi utajihakikishia work permit ya Bahamas na utakuwa free kufanya shughuli zako za kila siku.

2. Ukaribu wa kijiografia kati ya Bahamas na USA (Florida)

Sikuambii ni rahisi lakini, how do you feel kukaa karibu na US just 1 hour flight to Florida. I mean chance ya kuingia US ni kubwa sanaa either kupitia meli za kitalii zinazofululiza kutoka na kuingia US kila uchwao, la sivyo upate mwanamke wa kibahamia ambapo ufunge nae ndoa ili ujihakikishie uraia wa bahamas hivyo swala la kuingia US halitokuwa tatizo tena ukifananisha na nchi zetu za Africa.

Tunafikaje Bahamas????

Hakuna njia rahisi isiyokuwa na gharama, hapa lazima ujiinvest vya kutosha kwenda kuanza maisha mapya ugenini,
Utahitaji si chini ya 3-4M madafu ya kibongo kama nauli ya go and return ticket (in case mambo hayajaenda vizuri, rudi nyumbani tu) ambapo ukifika una uwakika wa kuishi kwa siku 90 bahamas hapo andaa si chini ya 2M kwa uwakika wa kuishi kwa muda wote huo mpaka utapopata kazi ya kujishikiza (inategemea na bahati na skills za mtu)

Usafiri kwa Dar es salaam utafanya booking kupitia Turkish airline ambapo utatoka Dar mpaka Istanbul, Turkey hapo utaconnect flight mpaka Boston US , (utanusa hewa ya US kidogo) kabla ya kupanda ndege itakayokupeleka mpaka Nassau, Bahamas.
Pia unaweza kutumia Kampuni ya Qatar wao wana route yao Inaanzia Dar to Doha, Qatar then unaconnect ndege to New York ambapo utaconnect ndege nyingine mpaka Nassau Bahamas.

Hapo ukimaliza taratibu za immigration unainua mikono juu unamshukuru Mungu huku ukianza kupuyanga mtaani akili kumkichwa, unaanza kuchanga karata zako huku ukihesabu masaa yako 129600 (90 days).

Everything is possible for the one who believes!
let's meet at the top.

Cheers [emoji1635] Ramani ya visiwa vya Caribbean.


Ramani ya Bahamas ikionyesha ukaribu na Florida US,


Meli mojawapo ya kitalii, bahamas


Picha ikionyesha mandhari ya bahamas eneo la mji lililozungukwa na maji ya bahari.


Mrembo akiwa amepiga picha kwenye hoteli maarufu ya Atlantis paradise island Hotel.


Jamaa akipiga mzigo wa bartender, marufuku kuchagua kazi.


Watoto warembo kabisa wa kibahamian wakiwa kwenye parade na dance maarufu kama "Junkanoo"



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halafu huku eti kuna watu wanajiita warembo, unamiliki rangi mbili na wigi kwenye mwili wako halafu unajiita mrembo angalieni color hizo original hakuna sugu hapo wala dalili za kukomaa very very soft...
 
Halafu huku eti kuna watu wanajiita warembo, unamiliki rangi mbili na wigi kwenye mwili wako halafu unajiita mrembo angalieni color hizo original hakuna sugu hapo wala dalili za kukomaa very very soft...
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] daaah.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kutokea kwenye hiyo marked point ni kisiwa kikubwa miongoni mwa visiwa vya nchi ya bahamas kinaitwa "Grand Bahama" kikiwa umbali wa miles 55 kusini mwa jimbo la Florida ambapo hutumia takribani masaa mawili kwa njia ya maji kufika florida ambapo kuna kampuni moja tu inayotoa huduma ya usafiri wa kivuko inayokwenda kwa jina la "Balearia Calibbean"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…