Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,478
- 3,659
Ndivyo alivyoitwa, kwa wake umaarufu
Kwa yale aliyopatwa, nyoyo zimepatwa ufu
Maini yetu yakatwa, kwa uchungu maradufu
Mola nae akulaze, pale unapostahili
Ni mengi uliyafanya, kupitia yako fani
Watu tukajawa chanya, leo twakukosa masikini
Wa rika zote wakumanya, kila kona duniani
Mola nae akulaze, pale unapostahili
Petu nchini ulifika, nyumbani kwako Afrika
Nasi tukahamasika, kwa namna ulivyotushika
Tulikupenda hakika, upendo usio mipaka
Mola nae akulaze, pale unapostahili
Kwa kweli yashangaza, utendaji wake mola
Weza dhani atukwaza, tuache tafuta hela
Hakika yote miujiza, jua Mola hana hila
Mola nae akulaze, pale unapostahilia
Wachache hawakukupenda, ninawaona wakicheka
Ni wale uliowapenda, haiba yao ukaitaka
Ila bado twakupenda, una damu ya Afrika
Mola nae akulaze, pale unapostahili
Dunia nzima yakutaja, kwa yote mema, mabaya
Na jina lako liwe tija, kwa yako ndogo kaya
Tuombe pasiwe mirija, ili wanao wasijepwaya
Mola nae akulaze, pale unapostahili
Hakika sitamalizia, nyoyo zauma dunia
Sauti nyingi zalia, macho yamevilia
Kifo sote twapitia, hakuna mbadala njia
Mola nae akulaze, pale unapostahili
Courtesy of mziwanda
Last edited: