The Whirwind: assasination of the president

The Whirwind: assasination of the president

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2016
Posts
4,701
Reaction score
11,920
Eeeeh wakuu,

Mnaotaka kuzielewa siasa nyuma ya pazia na michezo michafu inayochezwa na wanasiasa pamoja na wafanya biashara wakubwa kuitawala nchi na kuiweka mfukoni.

Kuteka mihimili yote serikali, bunge na mahakama bila kuisahau idara ya ujasusi (NIS) huku wanasiasa wakijifanya ni wazalendo kwenye camera na usoni kwa wananchi, mbaya zaidi wananchi wakichezeshwa mchezo wa kisaikolojia kuandamana na kumsifia raisi mla rushwa fisadi na waziri mkuu ambaye ndie mchezeshaji.

Bila kusahau baadhi ya wabunge ambao ni majasusi wa nchi jirani ealiojivika uzalendo wa taifa.

Raisi mwenye maradhi ya moyo ya muda mrefu anayeishi kwa kujidunga dawa za kushusha presha huku akilindwa na ulinzi mkali, ana fanyiwa jaribio la kuuwawa na waziri wake mkuu ambaye anambadilishia chupa ya dawa kiujanja na kumuwekea nyingine yenye kufanana na ile iliyopo lakini hiyo chupa ina dawa ya kuongeza zaidi kasi ya mapigo ya moyo🥺

Raisi anaanguka ghafla na kuperekwa ktk hospitali ya taifa ya kijeshi, waziri mkuu anakaimu uraisi kulingana na katiba ya nchi.

Picha ndio linaanza

Kama unapenda story za namna hii basi tafuta tamthilia ya kikorea inayoitwq THE WHIRWIND: DEATH OF THE PRESIDENT.

staring ni Park Don Ho ambaye ndiye waziri mkuu

Utanishukuru baadae hasa hasa huu msimu wa sikukuu.

Ahsanteni
 
1735212827201.png
 
Nimekimbilia kufungua nikijua huenda ni Classified Information zime leak. Kumbe Tamthilia.?
 
Back
Top Bottom