The World Is Not Fair (Viujinga Vingi)

The World Is Not Fair (Viujinga Vingi)

zagarinojo

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2020
Posts
2,622
Reaction score
2,846
The World is Not Fair.Dunia haina huruma au haina usawa.Hivi ni viujinga na vioja vya kidunia ambavyo watu wananiaminisha kuwa dunia haina usawa wala huruma.

1. Mwanamke akivaa nguo za kivulana itaonekana kama fashion na wala sio ajabu kwa msichana kuvaa nguo za kivulana mfano t-shirts na suruali
Ila mwanaume vaa nguo za kisichana mfumo vibody na skin jeans utaona dunia chungu.

2. Kichaa mwanaume akimbaka mwanamke mwenye akili timamu yule kichaa hafungwi wala kufunguliwa mashtaka.
Ila mwanaume mwenye akili timamu akimbaka kichaa mwanamke atafunguliwa kesi ya unyanyasaji na ubakaji.

3. Mwanaume mwenye umri mkubwa hata akioa msichana mwenye kumzidi miaka 10 yuko sawa
Ila mwanamke mkubwa kiumri akiolewa na mwanaume mdogo tunasema mwanaume amejichanganya.

4. Maskini wasio na elimu wanafanya kazi ngumu na kulipa kodi ambazo ndio hutumika kama mikopo kwa wanafunzi wa vyuo Ila mwisho wa Siku anayepewa heshima ni mwenye elimu..

5. Walimu wanalipwa mshahara mdogo licha ya kazi ngumu wanayoifanya ya kuwarithisha maarifa wanetu Ila wanaolipwa mishahara mikubwa ni maafisa wa serikalini na makampuni.

6. Mkulima analima kwa bidii lakini ndio wa kwanza kupata njaa Kutokana na kukosa chakula baada ya kukiuza mjini.

7. Ukiishi mjini ndo unaonekana mjanja wakati unalishwa na wakulima wachache waliojitolea kuishi vijijini.
 
eenhe labda mkuu kwa ushauri wako ulitaka tufanye mbinu gani mbadala ili dunia iwe na huruma mkuu🤷🏻‍♂️
 
Back
Top Bottom