figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,724
- 55,906
THEKLA MCHAURU
MWANAMKE WA KWANZA KUWA MWALIMU NGAZI YA CHETI KUSINI MWA TANZANIA.
Ni huko kusini mwa Tanzania maeneo ya Masasi, ambapo inapata kusimuliwa kuwa kwa kipindi chote cha Ukoloni yaani kuanzia miaka ya 1890 mpaka 1960 Wananchi wa Masasi walijiwekea historia kubwa ya kuwa ma mahusiano mazuri na Wakoloni. Yaani kuanzia Wajerumani mpaka Waingereza.
Japo Wajerumani walikuwa Na ukatili kwa kipindi chao. Bado Wananchi wa Masasi walikuwa na mahusiano yao vizuri tu. Kitu ambacho kiliwavutia sana Wakoloni wa Kijerumani
Na hata kwa Waingereza pia licha ya kuwa na sheria za ajabu ajabu bado Wananchi wa Masasi walikuwa na mahusiano mazuri.
Inasimuliwa kuwa mahusiano hayo yalijengwa kwa njia mbili yaani Kupitia dini ya Ukristo na Elimu ya mkoloni
Hivyo mnamo mwaka 1936, Waingereza walianzisha shule ya Wasichana huko Masasi iliofahamika kwa jina la Kwitonji. Na mwaka huohuo Shule hiyo ilitoa Walimu wa Ngazi ya Cheti.
Na mwanamke wa kwanza kupata Ualimu wa Ngazi ya Cheti alifahamika kwa jina la Thekla Mchauru. Na kujiwekea historia ya Kuwa Mwanamke wa Kwanza wa Kitanzania huko kusini mwa Tanzania kuwa Mwalimu wa ngazi ya cheti na kulipwa mshahara wa Shilingi 40.
👉Jambo la msingi la kufahamu hapa ni kwamba. Uenda mwanamama huyu akawa ndio Mwanamke wa kwanza kuwa Mwalimu nchini Tanzania kwa ngazi ya Cheti.
Hivyo bado tunaendelea kufanya tafiti mbalimbali juu ya maendeleo ya Wanawake katika historia ya elimu nchini Tanzania....
Lakini pia kama kuna mwenye kufahamu habari za wanawake katika historia ya elimu pia maoni yako ni sehemu halisi ya Historia hii.
👉Bado tunakusanya historia ya Mwanamama huyu na kuweza kufahamu mambo mengi zaidi.
Na. Mayuni Josefu
+255755671568