Theory of Time "nyakati"

Theory of Time "nyakati"

dosho12

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2023
Posts
596
Reaction score
1,475
Nyakati,wakati au muda vyovyote unavyoweza kuita kuashiria muendelezo wa hatua au matukio yaliyopita ya sasa na yajayo, hivi ushawahi kujiuliza nini maana ya nyakti je ni kuzama na kuchomoza kwa jua na mzunguko wa mwezi vipi kama jua lisingezama liwe muda wote je tungeweza kupima muda. Je muda una mwanzo na mwisho kutokana na dini muda ulianza pale mungu alipoumba ulimwengu hivyo kabla ya hapo hakukuwa na muda na vipi mwiso wa dunia utapofika muda utaendelea, na kutokana na sayansi muda ulianza takribani miaka billioni 14 uliyopita kwenye tukio la “bing bang”

Utofauti wa muda tumezoa kutumia ambapo saa nane mchana kwa Tanzania, ni saa sita mchana kwa Uingereza hio ni cha mtoto hivi unajua mwanga wa jua tunaoutumia mchana unatumia dakika nane kutufikia sisi hivyo mwanga unauona toka kwenye jua ni mwanga uliopita kwa dakika nane, hiyo na kwa jua bado nyota tunazoziona angani ni picha ya hizo nyota vilivyokuwa dakika, masaa, miezi mpaka miaka iliyopita, mfano umepata darubini ya anga inayoweza kuona mbali zaidi na kwenye anga umeona ndege za angani”spaceship” kitu chochote kitachotokea kwenye ile ndege kwa anayetazama duniani ataona matukio ambayo yamepita dakika kadhaa hivyo yaliyopita kwake wewe ni ya sasa.

Kuna theory moja ya Elbert Einstein anasema muda unatofautiana kutokana na ukubwa ya sayari au mvutano uliopo kwenye space time na mwendo wa mwanga unaotumia unasababisha utafouti wa muda, masaa kwenye sayari ya jupiter yanaenda taratibu siku moja kwenye jupiter ni masaa kumi ambapo kwa dunia ni masaa 24

Wote tumezoea muda ni matukio ya leo kuelekea kesho na kwa kufanya hivyo tunatengeneza jana ila Kwenye dini tunajua kuwa matukio tulio yafanya, tunayo yafanya na tutakayo yafanya yote MUNGU anayajua ameshayandika hivyo utayofanya kesho kwako ni kesho au uliyofanya jana kwako ni jana ila kwa mugu yote anayaona sasa hivi mungu anaona ulicifanya jana wakati huo huo anaona utayofanya kesho kwa wakati mmoja

Kama tulivyoona jinsi muda ulivo ambapo kuna uwezekano yaliyopita na yaliopo na yajayo yote yakawa sehemu moja kama yasasa “now” hayo ni kwa maoni yangu kila mtu anaweza kuwa na maoni tofauti ya jinsi nyakati nini

Reference
 
muda hauendi mbele wala nyuma,tunapata muda kutokana na stillness of space!. kukua kwetu na ubongo unavyochukulia mambo ndio hufanya tuone muda unaenda mbele ila ukweli ni hauendi mbele ila sisi ndo tunatumia space ku kua nakufanya yote tunayoyaweza!..
that so called gravity and speed of light are things can affect space time..

ila nina kitu kinanipa mashaka hapa haswa hili la kudhorotesha umri kwa kutumia kasi ya mwanga!, ni kivipi kasi ya mwanga inaathiri mwili wa binadamu mpk muda udhoroteke...????? hili swali sijapata majibu mpaka leo!
 
Back
Top Bottom