Gustanza, ndio maana kuna kitu kinaitwa mahakama. Kwanini hakulipa mahakama itaamua na kuona kama kuna sababu ya msingi. Malipo yanaendana na mkataba, NSSF ikifanya hivi THI itafanya vile. Sasa endapo mmoja anasema ametimiza sehemu yake na mwingine anasema si kweli, mahakama inaingilia kati ili kuamua kusiwe mtu wa kuonea kati ya NSSF au THI. Naona wewe unataka THI waonewe bila kujali kuwa kuna kesi ya msingi mahakamani. Kwa hiyo walipe tu wafute kesi na wakubali makosa yaishe ndicho unachopendekeza?