Thierry Henry apewa kandarasi ya miaka mitatu kuinoa Klabu ya Monaco

3llyEmma

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2017
Posts
6,172
Reaction score
6,884
Mchezaji na nyota wa zamani wa Arsenal na Fc Barcelona THIERRY HENRY amesaini miaka mitatu(3)kuwa kocha mkuu wa As Monaco ya Ufaransa.
Henry ambae pia ni mshindi wa kombe la dunia1998 akiwa na timu ya taifa lake la UFARANSA amechukua nafasi ya LEONARDO JARDIM ambae amekuwa na matokeo mabaya tangu kuanza kwa msimu Huu.
Henry ambae alikuwa kocha msaidizi wa UBELIGIJI chini ya ROBERTO MARTINEZ amekuwa na ndoto pia za kuifundisha klabu ya Arsenal siku za usoni.
Kocha Leonardo Jardim atakumbukwa kwa kuipa ubingwa wa LIEGE 1 AS MONACO mwaka 2016-2017 na kuwaduwaza wapinzani wake PSG.. PIA katika msimu huohuo wa 2016-2017 JARDIM Aliwafikisha Monaco nusu fainali mashindano makubwa ya ulaya UEFA.
MONACO inatawa kupoteza makali yake baada ya kuwauza wachezaji wake tegemeo kabisa kama,..
KYLIAN MBAPPE
BENARDO SILVA
MARTIAL
THOMAS LEMAR
BAKAYOKO
FABINHO
BENJAMIN MENDY
.. Leonard Jardim amekuwa kwenye wakati mgumu UEFA baada ya kupoteza mechi dhidi ya ATLETICO MADRID na BORUSSIA DORTMUND.
 
Team imekuwa ya kuuza vifaa tu na kutovireplace sawasawa. Wasipoangalia hata Thierry Henry atasukumiwa nje tu baada ya muda mfupi
Monaco kwa kuuza tu hawambo.. ishu inakuja kununua hawatak, wanaibua tena vipaji academy
 
Utauzaje vifaa vyote hivyo afu uwe salama?
 

Thierry Henry takes over as manager of Monaco
 
Watu wanalaumu kuwa timu ilikuwa inauza sana wachezaji , sasa unafikiri unabrige vipi gap versus timu kama PSG ambao wana revenue ya Zaidi ya pauni milioni mia nne kama huuzi wachezaji? Unajiwekaje katika mizani au ubaki huna hela maana Ligue one sina shaka kuwa revenue za Broadcasts ni ndogo kuliko revenue za kushiriki UEFA
 
Wamemuonea tu kocha,haiwezekani timu kila Msimu inaanza upya
 
Jardim ndiyo mbadala wa Mourinho pale OT siyo Zidane
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…