Thierry Henry mchawi mweusi kutoka La Desirade, 'Visiwa vilivyosahaulikka' Carribean

hamis77

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
13,628
Reaction score
20,992
.
Bonjour Mon Amies![emoji4] tuanze na visiwa flani vilivyotengwa, visiwa hivi kule Carribean Marekani ndipo nyumbani kwa Baba yake Mzazi Thierry Henry aliyekimbia ugumu wa maisha na kuangukia Les Ulis, viunga pale Paris.
.
Hakuna aliyewahi kujua kama Mtoto kutoka visiwa vile atakuja kutikisa soka la dunia, Babu Choggo, Henry yule wa namba 14 mgongoni[emoji119], kazi kubwa ilianzia pale visiwa vya Monaco akiwa na umri wa miaka 17 tu, aliyecheza na kuburudisha watu kupitia mpira
.
Henry hakupata sifa kubwa sana zaidi ya ujio wake pale Arsenal, 1999 mtoto mmoja akiwa na tabasamu pana kila muda akimwaga wino Highbury mbele ya Makamu Mwenyekiti David Dein, jioni ile mashabiki wa Arsenal walimuwaza zaidi Davo Suker kutoka Madrid kuliko Henry.
.
Ndani ya Highbury Henry alifanikiwa kushika hisia za mashabiki wengi wa soka, hakuwa tu mfungaji bali mkimbiaji bora zaidi wa mpira "balletic and athletic footballer" akizifanyia kazi pass murua za Mholanzi Dennis Bergamp, Dennis yule wa parabola na grasscutter passes[emoji119]
.
Shabiki wa Arsenal atakumbuka ile mikimbio ya mita 70 dhidi ya Spurs, aliugusa mpira mara kumi na kuweka mpira kambani, nakumbuka na vitumbua vyangu mkononi ile 2002, bado namuwaza Henry dhidi ya United na Real Madrid nabaki kufumba macho tu.
.
Licha ya mabao 228 pale Arsenal na ubora wote lakini Ufaransa hapewi heshma yoyote, licha ya kujengewa sanamu pale Emirates ila Paris waligoma kumpa heshma, wao wanakutajia Raymond Kopa, Michel Platini na Zinadine Zidane kama wachezaji wao bora wa muda wote.
.
Wafaransa wanasema "Je t'aime, non plus" kwa Kiswahili ni kuwa Nakupenda ila hunipendi, Henry alifanya makubwa kwenye soka ila Wafaransa wanasema hana hadhi kubwa kwa soka lao, sanamu pekee Ufaransa ni la Zizzou akimpiga kichwa Materrazi lilibuniwa na Abdel Abdessemed.
.
Henry hana furaha kubwa Paris, hana furaha kubwa na viunga alivyoazaliwa, dunia nzima furaha ya Henry ipo North London, pale Emirates ndio maskani yake, sehemu aliyopata umaarufu wake, alikua kipande kikubwa kwenye jengo la Invicibles ya 2003/04, ni straika bora zaidi kuwahi kutokea pale EPL.
.
Merci Beaucoup Henry 14',

 
Ni kama Mess na Argentina, wa Argentina wao Diego Maradona ni mtu mwenye heshima kubwa katika soka wakati Mess ana heshima kubwa Barcelona.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwamba juu ya Mwamba[emoji119][emoji119][emoji119]
 
Th14

Kwangu striker bora nyuma ya de lima

Ila ndio alikuwa mchezaji ninaemoenda zaidi kwa mimi, ndio alinifanya niwe mpenzi wa arsenal, kama si yeye basi steven gerrard angenifanya niwe Liverpool damu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…