Think Tanks in Tanzania!!!!!!

mpiga domo

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2013
Posts
852
Reaction score
1,507
Habari Zenu Wakuu,

Ningependa kupata msaada wa kujua kama hapa nchini Tanzania kuna hizi organizations ambazo nchi za wenzetu wanaita "Think Tanks"

Nchi za wenzetu hizi "Thinks Tanks" zimekua ni very influential kwenye ku'advocate varieties of public and social policies na pia kufanya research na kutolea utatuzi juu ya masuala mbali mbali ya kijamii ikwemo ya kiuchumi, kisayansi na mengineyo mengi.

Think Tanks kwa nchi zilizoendelea imetoa ajira kwa vijana wengi ambao wamemaliza elimu ya juu. Pia nina uhakika hata hapa Tanzania inaweza kuwa msaada mkubwa katika kutoa ajira na kuwapa uzoefu kwa vijana wengi waliomaliza elimu ya juu ambao wana uwezo kiakili lakini hawana kazi.

Msaada wangu hasa kutoka kwenu wakuu ni haya yafuatayo;

1) ningependa kujua structure yake kama unataka kuanzisha according to local laws inatakiwa iweje na vitu gani specific hasa ambapo kisheria hizi "Think Tanks" zinaruhusiwa kufanya.

2) Au kama zipo sema hapa Tanzania zinapewa majina mengine pia ningependa kufahamishwa

Asanteni Sana.
 
Mara nyingi hizi think tanks zinakuwa zinakuwa organized na managed by proffesional associations. Hapa bongo tatizo hakuna proffesional associations nyingi. Na zile zilizopo zimekaa kisiasa ni week na zina strong affiliation na serikali hivyo kufanya zisiwe influencial katika maswala mbalimbali. Kazi ya advocacy hapa kwetu inafanywa na NGO's ambazo pia zinategemea ufadhili na hivyo kufanya kazi kwa masilahi ya wafadhili.

Sioni uwezekano wa mtu mmoja mmoja kuanzisha think tank ambayo itakuwa na influence. Option iliyipo ni kusajili kama NGO.

Lakini tungeweza kuwa na proffesional associations zenye nguvu ni rahisi ku move forward kwenye kuinfluency. Maana vyama vya kitaaluma vinatambulika kiserikali.

Kipo chama kinaitwa Tanzania Proffesional Network -TPN. Kinafanya kazi kwa msimu labda ungewasiliana na wahusika kuona kama mnaweza kuanzisha different interest groups within TPN ambazo ndo zitakuwa na wataalamu tofauti tofauti wa nyanja mbalimbali.
 
Nenda online kazicheki Cato Institute, Council on Foreign Relations, Heritage Foundations etc.
Kama alivyosema mkuu mmoja hapo juu, kwa mazingira ya bongo inakuwa ni vigumu kuwa na think tanks zenye credibility. Wasomi wenyewe ndio hao akina Benson Bana, Max Muya etc njaa tupu, hawawezi kuikosoa serikali kwa sababu zao wanazozijua wenyewe moja wapo ikiwa ni NJAA.
By the way, mkuu Kiranga hapa JF, ni think tank tosha na ana weledi na connections nyingi za shindigs kule NY.
Cheki na mkuu Kiranga atakusaidia.
 

Thank you so much mkuu,

Nafikiri ili tupige hatua sisi kama nchi masikini ni muhimu sanaaa kuwa na organization kama hizi "think tanks" ambazo hazipo biased na itikadi au falsafa zozote za kisiasa

Primary goal iwe ni kufanyia utafiti wa kisayansi masuala muhimu ya kijamii na kuyatolea solutions ambazo ni sustainable.

Pia labda kungekuwa na Publications ama Journals that are freely accesible to the public ambapo kutakuwa na articles mbalimbali za baadhi ya masuala ambayo yamefanyiwa research na kutolewa viable solutions ili kuwe na open public discussion kabla ya policy yoyote kuwa impelemented
 

Hahahahaha it's a sad truth mkuu kwamba wasomi wetu wengi ni wasomi njaa, they are after what is best for themselves and not the country.

Lakini mimi nafikiri pia tatizo ni mfumo mzima wa kiutawala.

Hamna mazingira ya kisheria yaliyotengenezwa ambayo yanaruhusu open discussion na utafiti huru. Hata kama mazingira haya yapo, majibu ya utafiti yanapokuja basi yanatupiliwa mbali na yanakuwa classified reports tu.

And thank you for mentioning "Mkuu Kiranga" i will try to get as much information as possible before i consult him.

Thank you, Thank you, Your assistance is highly appreciated
 
Chondechonde usijekutwa umeng'olewa kucha na meno porini.
Good luck!
 
Nakubaliana na wadau hapo njaa kitu kibaya sana ma prof wetu wanatoa takwimu na maoni ambayo wao wenyewe hawaviamini ESRF na REPOA zinatumika Kama think tank
 
Chondechonde usijekutwa umeng'olewa kucha na meno porini.
Good luck!

Hahahaha mkuu hizi bado ni plans tu , ofcourse it will take a lot of time hadi kufikia kwenye impelementation taking into account lazima awareness ifanyike kuanzia grassroot level hadi kwa decision makers on the importance of these "think tanks"
 
Nakubaliana na wadau hapo njaa kitu kibaya sana ma prof wetu wanatoa takwimu na maoni ambayo wao wenyewe hawaviamini ESRF na REPOA zinatumika Kama think tank

Mkuu ndo maana na'suggest kwamba kutengenezwe sheria ambayo itatoa mwangaza on how these think tanks should operate. I think it would be better off kama hizi thinks tanks zitapewa legal obligations za kuweka public interests first before anything else.

Hii itaondoa mambo ya urasimu na rushwa kwenye masuala ya msingi kama haya.
 
Kwenye sekta ya lT kidogo naona kama wanahivyo vitu kwa kuwatumia Costech na Kinu.
 
Kwenye sekta ya lT kidogo naona kama wanahivyo vitu kwa kuwatumia Costech na Kinu.

Lakini mkuu ndo watu wanasema kwamba hizi ambazo zipo Tanzania kwa mfumo huo hazi'adress issues openly since zipo karibu sana na serikali

kwa mfano wanafunzi wengi kwenye sekondari nyingi wanakosa maabara za computer na vitu kama digital public libraries ambazo zingeongeza access ya knowledge kwa wanafunzi

Lakini hutasikia hizi issues zikiwa adressed na haya mashirika.ambayo yapo since mfumo wao wote hauwabani sheria kuweka public interest before anything else
 
Tume ya Taifa ya Mipango ndio National Think Tank ya Tanzania,kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya serikali.
 
Tume ya Taifa ya Mipango ndio National Think Tank ya Tanzania,kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya serikali.

Lakini si ipo chini ya ofisi ya raisi..???

Correct me if am wrong
 
Tume ya Taifa ya Mipango ndio National Think Tank ya Tanzania,kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya serikali.
A think tank is supposed to be an independent institution. Sasa ukisema tume ya taifa ya mipango ndio think tank ya Tanzania, labda ni kibongobongo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…