..sababu hasa itakuwa nini? hii hali ngumu au?
..bado hatujafika huko,ila kwa mtaji huu tunaweza elekea!
Ndugu yangu,
Nilipolonga ya Wapanda Farasi wanne, tuuze Ikulu, Serikali haramu na Boiling Point, na hapo bado hujazungumzia Screw Muungwana, Kikwete Hang the gloves, CCM Pambalama na mengine, yote yalikuwa ni kuepusha hili zali linalokuja.
Sasa si umesikia la Pemba, umewasikia UVCCM, je ni dalili gani tunahitaji zaidi kujua kuwa iko siku tutaamka na kubaini kuwa kila mmoja wetu anaandamana kudai Uongozi na Serikali ambayo ni Fanisi, Makini, Adilifu, yenye Juhudi na Maarifa ili kuleta Maendeleo kuondoa Umasikini, Ujinga na Maradhi?
Je siku hiyo itakapofika kama vurugu za Wanafunzi, Zanzibar 2001, Mwembechai, Mererani, Buzwagi na zile kelele za 1993-94 za Mtikila za kupiga vita Magabacholi na tukaandamana kwa amani kudai haki yetu, je Serikali itaturuhusu tuendeleze libeneke letu kupiga vita Ufisadi na ukosefu wa Uongozi au watachukua hatua madhubuti mithili ya mikwala ya Mkuu wa Wilaya David Hollela kwa Wabarabaig kuwa wao ni Dola na wana Polisi na Jeshi?