This is Kenya, ranked 125 in the World

joto la jiwe

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2017
Posts
26,117
Reaction score
46,617

Visa vya mauaji vimekuwa vikiripotiwa kila kuchao humu nchini hasa katika mtaa wa Kilimani jijini Nairobi, mauaji yake Kevin Omwenga yaliyotokea Jumamosi yaliyonyesha kuwa mtaa wa Kilimani unapaswa kuwa machoni mwa polisi kila dakika.

Kila mmoja amekuwa akiuawa kwa nia tofauti na sababu tofauti bali hayo yote ni mauaji, hii hapa orodha ya Wakenya waliopoteza maisha yao wakiwa mtaani Kilimani.

1. Kevin Omwenga
Mwanabiashara,28, huyo alikumbana na mauti ya kifoo chake mnmo Jumamosi usiku, huku nduru za habari zikisema kuwa alipigwa risasi kifuani mwake.


Waliohusika katika kifo hicho ni pamoja na Chris Obure, na Robert Ouko ambao wamefikishwa mahakamni hii leo.

2. Monica Kimani
Mwanabiashara huyo,29, alipatikana ameuawa nyumbani kwake katika juba la Dennis Pritt, Kilimani 2018, mshukiwa mkuu alikuwa Joseph Irungu almaarufu Jowie ambaye aliekwa jela kwa mwaka mmoja na nusu huku mwanahabari Jacque Maribe akiachiliwa kwa dhamana.


3. Careen Chepchumba
Mnamo mwaka wa 2012,14, Februari Careen alikumbana na kifo chake katika jumba la Santonia,Kilimani Nairobi mwendazake alikuwa mfanyakazi wa kampuni ya Kenya Power.

4. Sheila Murage
Murage aliaga dunia mnamo Juni 2020 baada ya kupatikana na wafanyakazi akiwa amelala kitandani baada ya kuwa na sherehe ya nyumbani.

Nduru za habari zilisema kuwa Sheila alikuwa anatokwa na damu puani, pia alikuwa amedhulumiwa kijinsia.


Washukiwa wakuu walikamatwa na kuachiliwa kwa dhamana.

Photo Credits: radiojambo

Ndio hawa! Wakenya waliopoteza maisha yao wakiwa Kilimani

=====

MY TAKE: Unfortunately the situation gets worse and there is nor hope.
 
Mauaji Kenya ni kama tunavyochinja mbuzi huku Tanzania, angalieni hiyo video.
 
😁😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…