Ndugu yahya wewe ni makini pamoja na star tv, kiujumla inaonesha mnataka kuweka legacy sahihi ya itv, kwanza nishukuru kwamba ulisoma mchango wangu kuhusu kwanini tunahitaji katiba mpya bila uchakachuaji ingawaje hukusoma maoni yangu kuhusu kombani -waziri. Okay kuhusu mjadala wa mchakato wa katiba mpya uweje, mimi maoni yangu ni kama ifuatavyo
1. Serikali iunde tume ya kuandaa rasimu ya katiba mpya-tume hii iwe na wawakilishi walioteuliwa na vyama vya siasa kutoka vyama vyao, wawakilishi kutoka bakwata, tec, cct, sabato, yaani dini, mwakilishi kutoka civil society, mwawakilishi kutoka vyuo vikuu, mwakilishi kutoka law society, mwakilishi kutoka haki za binadamu, mwakilishi kutoka mahakama, na mwakilishi kutoka balaza la watoto na vijana, mwakilishi kutoka media na baraza la habari, katika tume hii awemo jenerali ulimwengu, prof issa shivji, jaji amir manento,dr lwaitama, deus kibamba na ayoub lioba.
2. Tume hii ifanye uchambuzi yakinifu na kwa kukutana na vikundi mbalimbali ili iweze kutengeneza rasimu ya katiba mpya
3. Ikishatengeneza rasimu ya katiba mpya iweke hadharani rasimu hiyo ya katiba mpya kwa muda wa miezi sita wananchi kuijadili na kutoa mapendekezo yao
4. Ikishamaliza kupokea mapendekezo ya watanzania wote itengeneze final draft for preresentaion ipeleke kwa kamati ya bunge kwa ajili ya mapitio na mapendekezo.
5. Bunge lipewe nafasi yake kujadili na kutoa mapendekezo ya mwisho kabla ya kuifanya kuwa sheria.---angalizo bunge lisifanye maamuzi ya katiba kwa kupiga kura za kichama badala yake kamati ya bunge na tume vifanyie kazi mapendekezo ya bunge kabla ya kuipitisha.
6. Watawala wasiingilie mchakato huu manake katiba ya nchi inatakiwa kuwa huru na sustainable yaani tufikirie kuibadaili baada ya miika 50 mpaka 100 ijayo.
7. Tume isiwe ya watu wenye njaaaaaaaaa kali ndio maana nimependekeza kwa maoni yangu baadhi ya watu wanojua nini maana ya katiba.
8. Wananchi washirikishwe kutoa maoni wanachotaki kibadilike tukumbuke elimu ya uraia ni utata lakini kwa tume hiyo inawezekana kupata maoni yao, ni uzandiki eti kuwaambia watanzania tubadili au tusibadili wakati wengi wao hawaijui,
9. Tume hiyo iwe huru na uhuru uonekane siyo kama nec -tume pandikizi. Tume iwajibike kwa watanzania wa sasa na kesho
10. Mwisho star tv nawapa big up kama ninanvyo wafagilia mwanahalisi, raia mwema, tz daima na mwananchi