This will be my biggest risk! Kilimo cha alizeti Singida


Go for it and all the best. Usisahau kutupa progress ya mambo yanavyokwenda.
 
Ni takribani mwaka sasa, hebu tupe ushuhuda namna ulivyoangukia pua.
 
Kama ulivyosema mwenyewe unakuwa mwenyewe shambani,nategemea utafanikiwa mwezi wa 12 ndo mvua hasa na uzuri alizeti haitaki mvua nyingi hakika utafanikiwa,kila la kheri.
 
Mwaka huu ulilima alizeti?
 
Millionea wa kesho lete mrejesho babaaaa, mana n thread ya miaka kadhaa ilopita. Alipata io kitu alojaribu kutupigia hesabu au namna gani.....
Kama alilima kwel ekari 40 kwa mwaka 2019/2020 alitoboa maisha na ndo mana hayupo activ humu....
Maana gunia 1 liliuzika hadi 95000 and dumu 1 la mafuta ya kula lilifika 130000.
Japo katupuliza kdg kwa suala la gunia moja la mahindi kutoa dumu 2 za mafuta....... Ratio huwa n gunia 1 kwa kilo 19.5 za mafuta ambazo ni sawa na lita 31 ambalo ni dumu 1 na lita 1.5.......
Niongeze jambo, katika hesabu yake hajahusisha mashudu baada ya kukamua alizeti yake.... Ambapo kwa gunia, roughly hukosi kilo 50 za mashudu ambayo utauza 300 kwa kilo.
Angepata faida nene sana.
 
Hiyo running cost inahusisha na gharama za kukodi na kulima hayo mashamba? Technically costs zote ziwe 10 ml sawa unaweza jitahidi kufikia hiyo 20 maana michakato ni mingi kwenye kilimo.

Kuhusu mvua inabidi ufanye timing Sana kwa kuzungumza na wenyeji wa hayo maeneo.

Kuhusu bei ya alizeti sio kesi ni uhakika ila shida ni kufaulu uzalishaji.

Mwisho hizo mbegu xinapatikana wapi?
 
Hizi certified mbegu xinapatikana wapi hasaa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…