This young man Uhuru Kenyatta has transformed Kenya

This young man Uhuru Kenyatta has transformed Kenya

flyingcrane

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2014
Posts
241
Reaction score
88
Siku UK alipochaguliwa nilikuwa na hofu kuwa nchi ya Kenya itakuwa kama shamba la bibi, nilidhani kuwa Kenya ingegeuka kuwa na ukabila pamoja na ulevi na madawa ya kulevya kushamiri.
UK ameshikilia uongozi na kuleta maendeleo nchini, sector mbalimbali sasa zinafanya vyema na kunawiri..ukabila pia umeanza kutokomea tukishuhudia maridhiano na uwiano baina ya wakenya.makabila kuanza kuaminiana na kuishi kwa amani, sheria kuanza kutekelezwa pasipo na siasi, utajiri, cheo wote ni kupandishwa kizimbani watakapofanya makosa. Jamaa ameyafanya yote haya ndani ya miaka miwili tu! Kenya imekumbatia teknologia kwa nyanja nyingi mno
Tunavyojua chanda chema huvikwa pete, UK nimempatia hongera kuwa rais wakipekee kwa kabila letu moja la "Kenya" na kuunganisha nchi.. tumejifunza mengi kwa fujo za 2007/2008 na hatutawahi fanya kosa hilo..tangu kimbunga hicho kitukumbe tumeibuka na mbinu za kutuwezesha kuishi kwa amani na kuaminiana, hivi sasa tuko mbioni kujenga nchi yetu. Niko na imani Kenya yetu ipo siku itafikia kiwango cha Dubai
 
Back
Top Bottom