Those days when everything was real…..art was art and artists were artists aristablus elvis musiba a

kibavu

Senior Member
Joined
Oct 15, 2008
Posts
136
Reaction score
82
Dah leo nikiwa napanga panga vitabu vyangu nikakutana na riwaya za Musiba na nikaamua kusoma moja ya Riwaya za zaman za A.E. Musiba na mpelelezi mashuhuri Willy Gamba. Kweli Nyakati zimebadilika, ukiangalia namna ambavyo mwandishi alivyokua akiwaelezea wale majasusi na majahili wa Kikaburu, huwezi kuamini kwamba leo ndio tunawakumbatia na kuwaita wawekezaji.
Kweli kazi ya sanaa inaishi na kuakisi ukweli wa mambo hata baada ya miaka mingi kupita.
Hebu pata hii nukuu
“Kitu Kimoja unapaswa kutilia maanani Willy (Gamba); ni kwamba mtu mweusi hawezi kujitawala. Sanasana mtapata uhuru wa bendera, lakini uchumi wenu utatawaliwa na mtu mweupe daima dumu. Chukua mfano wa Tanzania, ni nani anayefaidi matunda ya uhuru kama sio mzungu na Mhindi? Mhindi akiendesha Benz, ni halali yake; thubutu mtu mweusi aendeshe Benz kama hakutiwa msukosuko! Sasa, kisa gani hata kupoteza maisha yenu kwa kupigania uhuru wa bendera ambao hauna faida? Kweli mtu mweusi hawezi….” F.K lakini alikatizwa…..
Hofu, uk. wa 121.
Ukisoma hii nukuu hapo halafu ukaangalia Tanzania ya leo, Afrika Kusini ya leo na Afrika ya leo kw aujumla, inatia hasira. Watu waliimbishwa nyimbo za uzalendo lakini leo yote hayo yanaonekana kazi bure tu.
Pumzika kwa Amani A.E. Musiba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…