THRDC Kanda ya Mashariki na Pwani: Upelelezi tukio la unyanyasaji Yombo Dovya-Temeke sio wa kuchukua muda mrefu

THRDC Kanda ya Mashariki na Pwani: Upelelezi tukio la unyanyasaji Yombo Dovya-Temeke sio wa kuchukua muda mrefu

informer 06

Member
Joined
May 11, 2024
Posts
66
Reaction score
49
Wanachama wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Kanda ya Mashariki na Pwani wametoa wito kwa Jeshi la Polisi kuwakamata na kuwafikisha Mahakamani watuhumiwa wote ambao wanadaiwa kuhusika na tukio la unyanyasaji wa Binti mmoja mkazi wa Yombo Dovya Temeke jijini Dar es Salaam .
IMG_5583.jpeg

Katika tamko lao wamelitaka Jeshi la Polisi kuwakamata watuhumiwa na kuwafikisha Mahakamani mapema iwezekanavyo, ambapo wamedai kuwa upelelezi wa tukio hilo sio wa kuchukua muda mrefu kwa kuwa watuhumiwa walijirekodi na kusambaza video hizo mtandaoni.

Hayo yameelezwa katika tamko la pamoja ambalo limesomwa August 7, 2024 likijumuisha takiribani wanachama 70, kutoka mikoa ya Dar es salaam, Pwani na Morogoro wamesema kuwa wansikitishwa na kitendo hicho huku wakitaka pia mtuhumiwa anayetajwa kama bosi (Afande) naye akamatwe.

"Sisi watetezi wa haki za binadamu Nchini tumesikitishwa sana na ukatili huo na tunataka wahusika wote akiwemo huyo bosi wao (Afande) wakamatwe na kufikishwa Mahakamani kwa mujibu wa Sheria za Nchi yetu" amesema

Wamesisitiza kuwa Ibara ya 12 na 13 za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinalinda heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa Utu wa Mtu na kupinga ubaguzi wa aina yoyote hile.

Wameeleza kuwa nchini ipo Kanuni ya Adhabu ambayo katika kufungu cha 131 A(1) (2) kinatoa adhabu ya kifungo cha maisha jela kwa Mtu au Watu wakithibitika kufanya ubakaji wa kundi (gang rape), kama inavyodaiwa kutokea kwa binti huyo maeneo ya Yombo Dovya Temeke.

Wameongeza kuwa kwa kuwa Binti huyo alionekana kulawitiwa wamedai kuwa pia kitendo hicho ni kinyume na kifungu cha 154 (1) cha kanuni ya Adhabu na kuwa kifungo chake ni maisha jela au miaka 30. Lakini pia wamedai kuwa kitendo cha kusambaza video ni kosa kwa mujibu wa kifungu cha 14 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao.

Aidha wadau hao wametoa wito kwa jamii kutosambaza zozote kuhusu tukio hilo ambazo ni kinyume na Sheria ya Makosa ya kimtandao na Sheria ya kulinda taarifa binafsi.
 
police please see this,,,,,,,,,, only god can judge you
 
Back
Top Bottom