THRDC: Serikali na Kanisa la Ufufuo na Uzima wakae meza moja wamalize mvutano

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
524
Reaction score
829
DMtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umetoa wito kwa Serikali, kupitia Waziri wa Mambo ya Ndani na Jeshi la Polisi, kukaa meza moja na uongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima kwa lengo la kuhitimisha mvutano unaoendelea kwa njia ya mazungumzo ya amani na maridhiano.

Pichani; Viongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima wakiteta jambo na Mratibu wa THRDC, Wakili Onesmo Olengurumwa

Wito huo umetolewa leo June 20, 2025 na Wakili Onesmo Olengurumwa, Mratibu Kitaifa wa THRDC, kufuatia sintofahamu iliyoibuka kati ya kanisa hilo linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima na vyombo vya dola, hali iliyosababisha kusitishwa kwa baadhi ya shughuli za kiibada katika matawi ya kanisa hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwapokea viongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima katika ofisi za THRDC, Wakili Olengurumwa amesema ni muhimu kwa pande zote mbili kufikia mwafaka kwa njia ya majadiliano ili kulinda haki za kidini na kuimarisha amani ya kijamii.

Soma Pia: Serikali yalifutia usajili Kanisa la Askofu Gwajima kwa kuingilia masuala ya siasa kwa nia ya kuichonganisha Serikali na Wananchi

Kwa upande wake, Askofu Amos Paul, akizungumza kwa niaba ya uongozi wa kanisa hilo, alisema kuwa wameamua kuomba msaada kutoka kwa THRDC ili kusaidia kulinda haki yao ya kikatiba ya kuabudu, ambayo kwa sasa inaonekana kukiukwa kutokana na hatua zilizochukuliwa na baadhi ya vyombo vya dola.

Amesema kuwa katika siku za karibuni, askari polisi wamevamia baadhi ya matawi ya kanisa hilo, kuwaondoa waumini kwa nguvu na kusitisha ibada, hali iliyozua hofu, taharuki na maswali mengi kutoka kwa waumini na jamii kwa ujumla.

Mgogoro huo unadaiwa kuibuka baada ya taarifa ilivyodaiwa kutolewa na mamlaka kutuhumu kanisa hilo kukiuka Sheria.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…