Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 276
- 473
Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini (THRDC), Wakili Onesmo Olengurumwa amesema kuna umuhimu wa kutafakari kwa mapana kauli mbiu ya Siku ya Wanawake kwa mwaka 2023 isemayo “Ubunifu na mabadiliko ya teknolojia: Chachu kuleta usawa wa Kijinsia” ili katika utekelezaji wake isipekekee kutengwa kwa baadhi ya makundi ya watu wenye uhitaji maalumu ikiwemo watu wenye ulemavu.
Ameyasema katika maadhimisho ya siku ya Wanawake Dunia Machi 8, 2023, ambayo THRDC wameadhimisha kwa kuwakutanisha baadhi ya Watetezi wa Watu wenye uhitaji maalumu kwa kufanya mjadala ambao ulilenga kubaini changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika utekelezaji na kuangalia namna ya kuzikabili.
"Tunapaswa kuangalia je, uwepo wa teknolojia ya habari na mawasiliano ya na maswala ya mtandao imekuja kuongeza chachu ya nyinyi (watu wenye ulemavu) kufanya kazi au imekuja kuwatenga na jamii nyingine’’ amesema Mratibu THRDC, Wakili Onesmo Olengurumwa
Ameongeza kuwa “Je Mazingira ya Sherai, Sera na Mifumo yetu inazingatia kwamba kuna watetezi wa haki za binadamu wenye ulemavu katika mifumo na mazingira yote ya teknolojia ya habari na mawasialino pamoja mitandao”
Wakati mwingine uwepo wa mitandao tusipoangalia inaweza kuleta utengano au ubaguzi mkubwa kati ya jamii moja na jamii nyingine, yale makundi ambayo yana uwezo wa haraka wa kufikia teknolojia hii wakayaacha makundi haya mbali (watu wenye uhitaji maalumu) kwa sababu ya mazingira na kwa sababu za kiuchumi…” Mratibu wa THRDC, Wakili Onesmo Olengurumwa
Aidha Mkurugezi wa Tanzania Epilepsy Foundation, Fides Uiso ameomba wadau mbalimbali ikiwemo Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu kuendelea kuwaamini na kuwawezesha kwa kuwajengea uwezo wa kidigitali watetezi wa haki za watu wenye uhitaji maalumu ili waendelee kupata ujuzi zaidi wa kutetea makundi hayo.
Mkurugezi huyo kutoka Shirika hilo linalowahudumia watu wenye Kifafa ikiwemo Wanawake ameyasema amesema kuwa makundi hayo bado yana changamoto ya utumiaji wa mifumo ya kidigitali hali ambayo inapelekea ugumu katika utekelezaji wa majukumu yao.
Naye Mkurugezi wa Shirika la Sauti ya Wanawake wenye ulemavu Tanzania ( SWAUTA) ameshauri Serikali kuundwa kikosi kazi cha kuangalia kama mifumo ya kidigitali iliyopo kwa sasa inanufaisha Watetezi wa watu wenye uhitaji maalumu.
“Kitengenezwe kikosi kazi kutoka kwa wanawake wenye ulemavu ili kuweza kupembua sera za Nchi hii kuona mwanamke mwenye ulemavu amewekwa vipi na kama hajawekwa kwenye sera washauri nini kifanyike kwa kutoa mapendekezo kwa Serikali “-Stella Jailos