informer 06
Member
- May 11, 2024
- 66
- 49
Katika kulinda Utawala wa Sheria, Nafasi ya Asasi za Kiraia, na Uwajibikaji nchini Tanzania kupitia mashirikiano yaliyoboreshwa, Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umesaini mkataba wenye thamani ya Euro €1,500,000 kutoka Umoja wa Ulaya (European Union) kwa ajili ya mradi wa miaka minne unaoanza kutekelezwa kuanzia mwaka 2025 hadi 2028.
Mradi huo utatekelezwa kwa kushirikiana na mashirika mengine matatu ambayo ni Jumuiya ya Wanasheria wa Afrika Mashariki (EALS), Chama cha wanasheria wa Afrika (PALU) , na Chama cha Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA).
Imeelezwa kuwa lengo la mradi huo ni kuboresha utawala bora, kuimarisha nafasi ya kiraia, na kukuza uwajibikaji nchini Tanzania.
Aidha walengwa wakuu wa mradi huo ni Asasi za Kiraia (CSOs), Vyama vya Wanasheria na Taasisi za Serikali. Mradi unalenga kuwawezesha walengwa hao kwa kuboresha uwezo wao wa kushawishi mabadiliko chanya ya kisheria, kujenga mashirikiano ya kimkakati, na kutetea haki za jamii zenye mahitaji maalumu kupitia shughuli kama mafunzo, usaidizi wa kiutendaji, na mazungumzo ya kimkakati.
Ambapo utekelezaji wa mradi huu unalenga kuchochea na kuimarisha haki za binadamu kwa kujenga imani ya umma na kusaidia utawala bora na kuhakikisha mageuzi endelevu katika sekta muhimu nchini Tanzania.
Utekelezaji wa mradi unanza rasmi mapema mwaka huu, ukilenga kukuza haki za binadamu, kuimarisha uwajibikaji, na kuhakikisha mageuzi endelevu katika sekta muhimu nchini Tanzania.
Itakumbukwa THRDC ni shirika mwamvuli lenye takribani Wanachama 300 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar ambapo limekuwa miongoni mwa mashirika yanayowezesha utetezi wa haki za binadamu nchini ikiwemo uzingatiaji wa misingi ya Sheria, utawala bora ikiwa ni sehemu muhimu ya haki za binadamu.