The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 1,967
- 4,267
View: https://youtu.be/cQ8my9Fu7jU?si=8G2_TzDMHKYELqgD
➡Huyu hapa ni Mkurugenzi Mtendaji wa asasi ya kiraia ya kulinda na kutetea haki za binadamu - Tanzania Human Rights Defenders Coalition (THRDC) Bwana Onesmo Olengurumwa akifafanua dhana dhima ya kauli mbiu ya kudai mabadiliko ya kikanuni, kisheria na kikatiba yanayochagizwa na kauli mbiu ya NO REFORMS, NO ELECTION ili kuwezesha kufanyika kwa chaguzi huru, za wazi na za haki hapa Tanzania...
➡Amesema, NO REFORMS, NO ELECTION haina maana ya kuwa kusiwepo na uchaguzi. Bali chaguzi zozote zijazo ukiwemo wa mwaka huu 2025, ni lazima ufanyike baada ya mabadiliko (reforms) muhimu ya kisheria, kikanuni na kikatiba kufanyika ili kuwezesha chaguzi huru na za kweli kufanyika ili kila mpiga kura aanze kuona thamani ya kura yake kwa kuhesabiwa na ikahesabika....
➡Anasema, kama hakutakuwa na mabadiliko hayo muhimu ambayo ktk maelezo yake ameyafafanua kwa kina, basi kwa kweli hakuna haja wala sababu ya kufanya chaguzi (maigizo ya uchaguzi) kama yale ya mwaka 2019, 2020 na 2024..