Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Baada ya andiko la Mwandishi wa Habari wa The Guardian kudaiwa kushambuliwa na Walimu, THRDC imetoa tamko, kusoma ilivyokuwa bofya hapa ~ Mwandishi wa Habari wa The Guardian anadai amepigwa na Walimu baada ya kupiga picha Wanafunzi wakisoma chini ya miti.
TAARIFA YA KUKAMATWA KWA MWANDISHI DICKSON NG’HILY
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) unakemea kitendo cha Mkuu wa Wilaya ya Ubungo kumkamata Mwandishi wa habari ambaye pia ni mhariri wa Biashara na Mkuu wa Kitengo cha Mtandaoni (Digital) kutoka Gazeti la the Guardian pamoja na walimu kadhaa ambao idadi yao bado haijafahamika kutokana na mwandishi huyo kuwapiga picha Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kwembe waliokuwa wanasoma chini ya miti.
Katika ujumbe wake aloutuma kwa njia ya WhatsApp, mwandishi huyo amedai kuwa amepigwa sana na kuumizwa kwenye mkono na simu yake imevunjika kioo.
Taarifa za awali zinaonyesha kuwa mwandishi huyo alipelekwa ofisi za Serikali ya Mtaa na kwasasa anashikiliwa katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo.
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) unafuatilia kwa ukaribu sana suala hili Lakini pia THRDC inaamini kwamba Mwandishi wa habari ana haki ya kutafuta na kusambaza habari kwa umma kwa mujibu wa ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kupiga picha ni jambo la kawaida.
Wito wetu.
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) unatoa wito kwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo kumuachia mandishi huyo mara moja kwani Mkuu wa Wilaya hana Mamlaka Kisheria ya Kumkamata mwandishi huyo kwa vyovyote vile.
Imetolewa na,
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),
Julai 10, 2024 Dar es Salaam, Tanzania.
Majibu ya Serikali ~ Madai ya Wanafunzi kusomea chini ya mti Shule ya Msingi Kwembe (Dar), Serikali yasema walikuwa katika programu maalumu