Thread maalum kukumbushana michezo ya utotoni iliyosahaulika

Elvis Legacy

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2017
Posts
3,984
Reaction score
5,820
Mpira wa utotoni miaka ya 80s na 90s na 2000s (2000-2005) mwanzoni mambo yalikuwa supa.

Sijui nani alikuwa analeta mbinu(tactics) za kuujua na kuelewa vizuri mpira wa miguu ili mchezaji kuwa bora zaidi.

Nimekumbuka hii michezo;

1. SAFA(suffer) BWEGE
Hapa wachezaji mnakuwa kwenye mpagilio wa mzunguko(round) kisha mchezaji mmoja (BWEGE) anaingia kati na kutafuta mpira mpaka aupate.

Anayeupoteza kwa BWEGE ndiye ataingia kati na kuchezeshwa yeye kama BWEGE. Maana wachezaji wengine wanapasiana mpira wakiwa kwenye ule mzunguko wakati BWEGE [emoji2957] anautafuta ili auguse tu mpira [emoji460].

Mara nyingine BWEGE alikuwa anakimbiza mpaka anakata tamaa [emoji43] maana kuna wachezaji walikuwa na chenga za maudhi kabla ya kutoa pasi. Ukiwa BWEGE na hautumii akili utapigwa tobo au kanzu na kisha kusindikizwa na kofi la mgongoni [emoji23].

FUNZO: Kutafuta mpira wakati ukiwa kwa wapinzani (Marking)

Endeleza unayoijua
 
2. DANADANA [emoji460] [emoji460] [emoji460]

Huu pia ulikuwa ni mchezo wa mpira wa miguu. Hapa wachezaji walikuwa wanaoneshana uwezo wa kuwa na stamina na control ya mpira ukiwa mguuni kwa kuupiga piga pasipo kuanguka.

Lilikuwa linachorwa jadwari kwa kila mshiriki(mchezaji) ili kuhesabu idadi ya DANADANA(idadi ya kuupiga mpira pasipo kuanguka kwa kugusa chini).

Mnawekeana milestone(kipimo/ukomo) ili mtu kushinda. Kwa mfano danadana 1000. Kisha mnapiga kwa zamu wakati wachezaji wengine wakihesabu.

Kuna wachezaji walikuwa mahiri sana. Unaweza kuhamaki kapiga DANADANA zaidi ya 500 kwa mkupuo (round moja) [emoji23]. Ukiwa na matege au njaa hawezi kufika mbali maana utaishia DANADANA 50. Ilihitaji stamina kubwa kusimamisha mguu mmoja kwa muda mrefu wakati mwingine ukipiga DANADANA [emoji460]. Pia control na focus ili mpira ubaki karibu yako.

Kinara wa DANADANA kwenye kitongoji chetu alikuwa anaitwa JOFU SHIBE. Huyu jamaa aliweza kupiga hadi DANADANA 800 kwa mkupuo mmoja. Siku hizi umri umeenda na alishaoa wake wawili hata 20 hawezi kufikisha [emoji23].

Pia vijana wa hovyo wazee wa CHAPUTA dronedrake wasingeweza kupiga hata DANADANA 10 maana miguu ingeishia kutetemeka tu.

FUNZO: Stamina na Control ya miguu na Focus ya akili.
 
wakati niko primary kucheza gololi na kujipikilisha ndiyo vilikuwa kwenye chat.

Funzo
1. Gololi, concentration
2. Kujipikilisha, waliokuwa serious ndo machef hao [emoji16]
Safi sana. Umenikumbusha gololi. Zilikuwa na michezo mingi mingi. Pia tulijifuza kiingereza kupitia mchezo huo.

Mfano:
U-First.
U-Second
U-Last
Lift

Nikipata muda nitaelezea aina mbali mbali ya michezo ya gololi.
 
Sisi wengine hatukupata nafasi ya kucheza kabisa.
Pole sana. Michezo ilituunganisha sana watoto kwenye jamii. Pia talanta (talent) za watoto zilijulikana mapema kutokana na umahiri wao kwenye michezo fulani fulani.

Ninaye jamaa yangu kwa sasa ni fundi makenika mkubwa mjini Dar-es-salaam alikuwa mtaalamu wa kuunda magari ya mbao, makoa na nyaya. Alikuwa mbunifu sana miaka ile ya 90s mwishoni.
 
3. KOMBOLELA.

Huu mchezo wengi mnaujua. Mtu mmoja analinda(anazinga) kopo au mpira kisha wachezaji wengine wanajificha maeneo ambayo sio mbali na kopo au mpira ulipo.

Mchezaji akionekana na mlindaji(mzingaji) basi hutajwa kwa jina. Mfano "KOMBOLELA ELVIS". Mchezo huu ulinoga hasa muda wa jioni jua likianza kuzama.

Kila mchezaji atakayeonekana na kutajwa jina lake basi aliwekwa kizuizini kwenye duara maalum lililochorwa mpaka wachezaji wote wapatikane. Kuna wachezaji wakienda kujificha walikuwa wanapotea mazima mpaka giza linatanda [emoji35], basi ndio unakuwa mwisho wa mchezo.

Ikitokea mlizi wa mpira au kopo (Mzingaji) akajisahau basi hutokea mchezaji mjanja akabutua(kulipiga teke) kopo [emoji898] au mpira [emoji460] na kuwaokoa waliokwisha wekwa kizuizini na kwenda kujificha upya.

FUNZO: Mchezo ulikuza ushirikiano na kujuana baina ya watoto wa mtaa au kitongoji kimoja kwa kufahamiana majina wote.
 
Michezo ya haya matunda pori nani anaikumbuka?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…