Thread maalumu ya mchezo wa Masumbwi (BOXING)

Crawford kashinda kwa TKO 6th Round
mkuu yaelekea we mdau wa ndondi kweli kwel nafurah sana nikipata sapoti, kuna bingwa anaitwa Loma the matrix cheko hajapigana muda sasa em tupe ufafanuzi kidogo[emoji23][emoji23]
 
mkuu yaelekea we mdau wa ndondi kweli kwel nafurah sana nikipata sapoti, kuna bingwa anaitwa Loma the matrix cheko hajapigana muda sasa em tupe ufafanuzi kidogo[emoji23][emoji23]
Bondia ambaye naturally anapigana katika uzito wa lightweight, anapendwa sana kutokana na style yake ya upiganaji inayoburudisha, yuko vizuri technically na anarusha ngumi kwa speed, Team ya Mayweather 'TMT' wamekuwa wakimkwepa sana, maana alishaomba pambano maranyingi na kijana wao 'TANK' ila wamekuwa wakileta siasa, wanamlinda kijana wao asijepoteza pambano maana wanamjua vizuri Loma[emoji3][emoji3]. BTW, Loma kacheza pambano lake la mwisho April 12 mwakahuu na kushinda kwa KO Round ya 4 dhidi ya Anthony Crolla
 
Baada ya pambano la AJ na Miller kushindwa kufanyika kutokana na Miller kufail drug test mara3, bondia ambaye amewahi kupoteza pambano mara1 tu Andy Ruiz amethitibishwa kuwa mbadala hapo June1 mwakahuu, akihojiwa na SkySport AJ alijibu kwanini ameamua kumchukua Ruiz kama mbadala, alisema ni kwa sababu Wilder na Fury ambao ndio mapambano ambayo mashabiki wanatamani kuyaona wako bize wana mapambano mengine, pia Ortiz walishindwana kwenye maswala ya mkwanja, so mtu anayefatia kwa ubora na yuko tayari ni Ruiz
 
Kesho May 4 Kuna pambano la kukata na shoka la uzito wa kati litakalowakutanisha bondia mmexico anayesadikika kuwa ndio 'face' of boxing baada ya Mayweather kuretire na bondia mwingine mahiri Daniel Jacobs kutoka Marekani. Pambano hili linatabiriwa kuwa ni another big challenge kwa Canelo, kwani Jacobs ni bondia tough sana...
 

Attachments

  • Screenshot_20190503-133721_1556879911152.jpeg
    100.5 KB · Views: 60
Na hili pambano wameghairi au maana kila nikiingia net naona ni tar4 now tushafika tar5 sasa sielewi na hata link za live streaming sijakutana nazo kabisa
 
Na hili pambano wameghairi au maana kila nikiingia net naona ni tar4 now tushafika tar5 sasa sielewi na hata link za live streaming sijakutana nazo kabisa
Linachezwa alfajiri kwa saa zetu,mida ya saa 12 hivi
 
Pambano gumu lkn Jacobs atapigwa
 
Wilder, first round KO[emoji3][emoji3]
Your browser is not able to display this video.
 
Gennady 'Goodboy' Golovkin almaarufu kama GGG, bondia wa kiwango cha juu sana duniani wa uzito wa kati anatarajia kupanda ulingoni usiku huu kuzichapa na mcanada Steve Rolls. GGG ambaye anasifika kwa kuwa na roho ya paka (hata umpige ngumi 800 mfululizo huwezi mdondosha [emoji3][emoji3][emoji3]) ana jumla ya mechi 38, kati ya hizo ameshinda 36 moja akitoa sare na nyingine kupoteza kwa Canelo Alvez via UD, Kwa upande wa Steve Rolls ambaye si jina maarufu kwenye ndondi (underdog) ana jumla ya mechi 19 na hajawahi kupoteza.Je, anaweza kufanya maajabu kama ya Ruiz wiki iliyopita? Let's wait n see, bado masaa machache tu...

 
Kumbe thread yenyewe bado mpya mpya 👊👊
 
Mkuu nimekutana na debate kali sana sehemu kuhusu AJ vs Wilder.... Kwa mtazamo wako nani anamkalisha mwenzake.
Huo mjadala haupo tena tangia AJ alivyokalishwa na Mmexico Andy Ruiz. Baada ya lile pambano wadau wengi hawatamani tena kuliona hilo pambano maana ni wazi AJ atadharirishwa. Kabla ya kufikiria kupigana na Wilder, ashinde kwanza Rematch yake dhidi ya Ruiz, tena ashinde kwa KO ndio anaweza akarudisha imani kwa mashabiki
 
Mkuu screpa kumbe unaujua huu mchezo tumebaki wachache sana wacha tuzidi kupeana updates za hapa na pale lakini mm pia ni mshabiki sana wa mma.
 
Mkuu screpa kumbe unaujua huu mchezo tumebaki wachache sana wacha tuzidi kupeana updates za hapa na pale lakini mm pia ni mshabiki sana wa mma.
Mimi pia huwa nafatilia MMA japo si sana, Nalisubiria pambano la Khabib kama ataendelea kuwa unbeaten ama nayeye ataanza kuchezea vichapo kama Mc Gregor. Kwa wanawake namkubali sana Amanda Nunes, yule demu hatari sana majuzi hapa kapiga KO kwa sekunde kadhaa.Tuwe tunapeana updates pia!
 
Habari inayotrend sasa kwenye Boxing inamuhusu Mrusi Maxim Dadashev aliyefariki baada ya kupata brain damage kwenye pambano lake lilofanyika ijumaa iliyopita. R.I.P brother
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…