Leonard Robert
JF-Expert Member
- Apr 22, 2011
- 11,125
- 7,373
kweli mkuu, me nawafaidi sana hawa WAPEMBA.. Njoo tupate huduma za simu zilizonakshiwa na marashi ya karafuu.!Mie natafuta ule mtandao wa WAPEMBA, hawaibi wale
mimi pia nahama.sijajua coverage ya huu mtandao wa wapemba,kule kwenye miteremko ya mlima kilimanjaro tarakea unapatikana?
dah, toka mobite, buzz hadi tigo. Bado na imani sana na tigo hivyo siwezi kuhama kabisa maana wao ndio wakali wa promotion mtarudi wenyewe huko mlipoenda kupanga.
Haka kahuduma cha voice msg wamekaanzisha kinyemela kwa namna hata kama mtu hataki kuacha ujumbe wa sauti pesa itakatwa tu na mpigiwaji atapokea msg ya ujumbe hewa wa sauti. Kampuni ya TIGO ina njaa mpaka inachajisha wateja wakiwa wanapiga simu customer care kuomba misaada ya shida mbalimbali za kimtandao.
Kuanzia hivi sasa najitoa Tigo na line hii nitaitumia kama phone book.
Nachagua mtandao mwingone, TIGO mmezidi.
Tukija wote huko zantel na wenyewe si watakusubirisha? labda uzungumzie ghalama ya kupigazantel wapo poa sana halafu ukiwapigia hausubiri hata dakika tatu unakuwa ushaunganishwa. hamieni ZANTEL.
hata voda nao wamepandisha bei hadi sh 2.6/sec tena bila kuwaarifu wateja.
mimi kwa sasa natumia laini mpya ya ZANTEL raha sana kutumia huu mtandao. wanaJF twanga kotekote.
Huo mchezo wa voda!mi nilituma sms kwa jamaa yangu jana saa mbili usiku ime deliver leo saa nne asubuhi....sijui waliituma kwa basi