Thriller Movies kwa Weekend: "What you wish For (2023)"

Thriller Movies kwa Weekend: "What you wish For (2023)"

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
26,961
Reaction score
77,890
Kwa wapenzi wa thriller movies, hii ni moja ya movie ya kuiangalia. Iko simple ila nzuri sana.
MV5BZGRiNzdmZWYtNmRkMy00ZjE0LTk2YjgtZDRjYmZmMzZmOGRiXkEyXkFqcGdeQXVyMzU0ODIwMQ@@._V1_.jpg


Kwa lugha nyepesi ipo hivi, kuna jamaa anaitwa Ryan alitoroka London na kwenda Latin America alikoalikwa na rafiki yake Jack walioachana miaka 12 iliopita. Ryan anasumbuliwa na madeni yaliyotokana na addiction za kubet.

Ryan na Jack walikua roommates kwenye culinary school (shule ya mapishi) kwahiyo jamaa ni professional chefs. Na wanajua kweli kupika. Jack ametusua anapika kwenye special occasions, very expensive restaurants ila mwamba Ryan yeye kabugi life. Hajatusua kabisa.

Hapo walipofikia ni nyumba iliopo Msituni (cottage) na Jac kaja kwaajili ya kuwapikia Big Dinner matajiri watano watakao kuja kula hapo, milo ya aina 4.

Siku ya 3 baada ya Ryan kufika, anaamka asubuhi anakuta Jac kajinyonga na kufa. Katika kucheki Laptop yake akakuta account ya bank inasoma £1,750,000 karibia Bil 4.5 za Kitanzania. Jamaa akaingia tamaa, akamzika Jac afu yeye akachukua personality akajifanya yeye ndio Jack.

Nadhani niishie hapa. Itafute nikiendelea itakua spoiler.

Kumbe Big Dinner matajiri wanakula nyama za watu, unaiandaa kama unavyoandaa nyama nyingine. Na Jac alitangulia uko kwaajili ya kutafuta mtu wa kumuua, na kumpika. Kwahiyo Jamaa akatakiwa ndio afanye ivo. Na iyo Agency ni kubwa na wana power huwezi wakimbia.

Noma sana. Ebu ukipata bando ishushe.
 
Hii movie sijaipenda kabisa... Maana matukio yako nusunusu pia haina uhalisia wowote anway Movie za sikuhizi hazieleweki Bora nitazame zile za adult
 
Hii movie sijaipenda kabisa... Maana matukio yako nusunusu pia haina uhalisia wowote anway Movie za sikuhizi hazieleweki Bora nitazame zile za adult
za adult zinapatikana wapi?
 
Back
Top Bottom