matumbo
JF-Expert Member
- Jul 9, 2011
- 7,224
- 3,951
Wakati watu leo wako bize kuthrowback ishu mbali mbali ghafla nimemkumbuka mkali wa hizi kazi,Kibra Msitu wa vina a.k.a Juma Nature.
Nakumbuka mara ya kwanza namuona anachana kipindi hiko mie bwana mdogo ,anashika kipaza anapanda jukwaani na washikaji zake wawili mmoja Dolo mwingine simkumbuki mpaka kesho.
Ilikuwa ni mara yangu ya kwanza naona msanii anabeba kijiji kinadata ...anapiga mistari ya kiswahilini hatari alafu watu wanamuelewa ,anakwambia wimbi la njaa matatizo umaskini chanzo cha nguo kupwaya kufunga na pini,,,watu heeeeeeee .
Baada ya hapo nashuhudia maajabu juu ya maajabu mara kachukuliwa na majani,mara katoa singo yake hili game ikaja jinsi kijana mpaka album nzima..Album haufowadi ata nyimbo moja..Huku sonia kule kigetogeto album ilipofika kanda ya ziwa ikaisha ndani ya week.
Akaja na album ya Ugali ikavunja rekodi ya mauzo bongo akaijaza Diamond Jubilee mpaka watu wakazuiwa kuingia.
Msanii wa kwanza wa bongofleva kumiliki Benz kwa mauzo ya muziki.Kawatoa wasanii kibao,kuna kipindi Tmk yote aliibeba yeye.
Kaimba karibu na kila msanii mkali bongo.Kama haitoshi akatumiwa na Ruge Mutahaba ,Sebastian Maganga na Joseph Kusaga kuokoa jahazi la Fiesta lililozama baada ya Lil Kim kuchemsha.
Kajenga nyumba mbili kwao uswazi na anaishi huko mpaka kesho.Bongofleva wa kwanza kuuza magazeti ya Shigongo kwa drama zake na mbongo muvi Sinta.
Hapo sijazungumzia maajabu yake, maana server ya JF haitatosha...Huyu ndio Nature, Bob Marley wa bongo fleva.
Nimejikuta namkumbuka kidogo leo.