TIANGONG-1 CHOMBO CHA ANGA ZA JUU CHA CHINA KINACHOTATAZAMIWA KUINGIA KWENYE MZINGO WA DUNIA MUDA WOWOTE APRIL-1

TIANGONG-1 CHOMBO CHA ANGA ZA JUU CHA CHINA KINACHOTATAZAMIWA KUINGIA KWENYE MZINGO WA DUNIA MUDA WOWOTE APRIL-1

PatriceLumumba

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2016
Posts
426
Reaction score
581
Chombo cha anga za juu cha China Tiangong-1 kilirushwa kwenda kwenye anga za juu septemba 29,2011 kikiwa kinaendeshwa na guvu za jua Kikiwa angani kina uzito wa Tani 8.5(8,506 kg) na urefu wa mita 10
Chombo hicho kilitengezezwa na shirika la Anga la China
(The China National Space Administration (CNSA))
Chombo hicho ni kati ya vyombo vyenye kusafiri kwa kasi kubwa huko angani kwa kasi ya kilomita 28,000 kwa saa na kukifanya kuweza kuzunguka dunia nzima kwa dakika 87 tu zaidi ya kilometa 200 angani.
Mpaka kufukia sasa tarehe 1 april Tiangong-1 kimeshaweza kuzunguka dunia mara 37,387.
Chombo hicho kimeshatembelewa mara tatu na wana anga wa china na mara ya mwisho ni mwaka 2013 lakini baada ya hapo china walikiongezea muda chombo hicho kukaa angani na kukitumia kwa utafiti mbalimbali kwani muda wake wa kutumiwa angani ilikuwa ni miaka miwili tu toka kirushwe.
Mwaka 2016 china walitangaza kupoteza mawasiliano kwa zaidi ya asilimia 70 na kushidwa kabisa kukiongoza na kupelekea chombo hicho kuanza kushuka taratibu huku kikiendelea kuzunguka dunia.
Tarehe 30March chombo hicho kilikuwa kipo umbali chini ya kilomita 167 angani huku kikiwa kinasafiri kwa kasi ya kilomita 28,000 kwa saa kuzunguka dunia.
Kwa duru za wanaanga wanatarajia sana chombo hicho kuangukia kati ya Amerika ya kaskazini,Uraya ya kaskazini,Australia,America ya kusini au kati ya bahari ya Pasific na Atlantic kutokana na kasi na mzunguko wake kwa sasa.
Kiasi kikubwa sana cha chombo kicho kinategemewa kuteketea angani kwasababu kikiwa kinaingia kwenye mzingo wa dunia kitakuwa kikiwaka moto kutokana na msuguano mkubwa,Jua kwamba kipindi kinaporushwa huwa kimefunikwa kwenye kifaa maalum kinachokilinda ili kisiweze kutekete kwa moto na kikifika anga za juu kifaa hicho maalum hufunguka na kukiachia chombo hicho angani.Sehemu yenye msuguano mkubwa kati ya dunia aridhini na angani inapatika kati ya kilomita 100 angani.Wanasayansi hao wanasema kwamba kuna uwezekano mkubwa kwa mabaki ya chombo hicho (space debris) kama asilimia 10-40% yasiungue na kudondoka chini ikiwa na maana ya tani 3-4 ya mabaki ya chombo hicho ila wanaimani itakuwa baharini ila wametoa tahadhari kwamba inawezekana pia yakadondokea hata kwenye makazi ya watu inategemea eneo chombo hicho kitakapokuwa wakati kikiingia kwenye mzingo wa dunia.

LUMUMBA
 
"...kusafiri kwa kasi kubwa huko angani kwa kasi ya kilomita 28,000 kwa saa na kukifanya kuweza kuzunguka dunia nzima kwa dakika 87 tu zaidi ya kilometa 200 angani..."
Sijaelewa hapo jombaa
 
Back
Top Bottom